Mkuu acha huu utani ndugu! Unayoyaandika I wish ningekubaliana nayo.
Hivi unafikiri katika hiyo population ya raia million 900 ya Africa..ni wangapi wana purchasing power? mfano..ni wangapi wanakula kitu kama siagi au jibini? Reality is..Africans never learn. Unless we create middle class yenye uwezo wa kununua..we are doomed!
WTO is an instrument of the big powers to make their deals easy. Na wala I can assure you..hawa jamaa hawamezi bitter pills wala nini kwa sababu uchumi wao hautegemei kilimo as we do. Makampuni makubwa sasa yanajikita katika kuprocess chakula wakati sisi tunahangaika kulisha watu wetu na kuexport mali ghafi.
Chakula kinachokosa soko ndicho hicho...wanawapa UN wanaokuja kugawa misaada kwenye "makambi ya wakambizi na sehemu zenye maafa ya njaa" hivi unafikiri ukisikia serikali fulani imetoa msaada wa millions kwa nchi fulani..you think wanatoa pesa $$$ perse? no way..wanadump hata vyakula vyao...its scary man..
Hivi kweli masikini na maskini mtafanya biashara gani? Tanzania analima kahawa..Burundi analima kahawa..so is Kenya..sasa tutaexport na kuimport nini? Can Tanzania import flowers from Kenya? tuyafanyie nini maua?
China na India wanatuchezea shere just like the rest..sisi tunafurahi kwa sababu tunaona China kamkatalia US..si kwa sababu tutafaidika..tunafurahi tuu ilmradi aliyegomewa ni US na EU ambaye tunamuona ni adui yetu. But China hana NIA NJEMA NA SISI.
Ukweli ni kwamba Afrika tumeshindwa kustrategize kilimo cha kutufaa (hata Green revolution ya Kofi Anani) haijatusaidia chochote. Hebu fanya survey yako uangalie nchi za Africa zinatenga kiasi gani kwa ajili ya bajeti ya kilimo na ujiulize EU wanaspend kiasi gani kwenye subsidies..utapata jibu.
All in All I say hii WTO ilianzishwa kwa mbwembwe nyingi sana...na mazungumzo hayawezi kufanikiwa kwa sababu itaumiza maslahi ya wakubwa....Its only Africa ambayo haifikirii maslahi ya raia wake in whatever they do.
Bila kuwa na strong middle class, Africa can never achieve anything. we need to set our priorities. Product za ulaya zinapata soko kwetu kwa sababu ziko cheap..na kwa sababu wananchi wetu walio wengi ni maskini, what do you expect? si mara mia ule frozen kuku wa shillingi elfu mbili from France kuliko fresh kuku wa elfu tano from Muheza?
Africa, bado saaana...safari ndefu!
Nadhani kwanza nianze kwa kusema pitia tena niliyoandika vizuri. Kuhusu purchasing power nimeliongelea sema kwa kiswahili. Uwezo ndio ni mdogo lakini je ni mdogo kama ambavyo wanataka tuamini? kama tunauwezo wa kununua vilivyokuwa processed magharibi vya kwetu kwa nini tushindwe?
pili swala kujenga jamii ya kati (middle class) inahitaji kuamsha uzalishaji wa ndani ya nchi zetu. hili halitatokea tukiendelea kuzalisha kwa masoko ya nje. ambayo unakuta wote kwa wakati mmoja (kutokana na ushawishi wa magharibi) tunazalisha kitu hicho hicho, hivyo kufanya bei kuwa ndogo. Mfano wako kwa maua ya Kenya ni mfano mzuri sana. sasa ni nchi ngapi za africa zinasafirisha maua? na sio hizo tu na nyingine zinazoendelea? mwisho wake ingawa uzalishaji huku kwetu ni nafuu wingi wa bidhaa nafanya bei ziwe kushoto.
swali sio kama tunaweza kununua maua ya kenya bali ni je tunahitaji kununua maua ya kenya?
Unaposema nchi zao hazitegemei tena kilimo, na wakati huo huo unasema makampuni makubwa yanajikita katika kuprocess chakula naona kama unajikanyaga. chakula (iwe ni kulima, kuprocess au reprocessing) bado unakuwa unajishughulisha na bidhaa ya kilimo (
Agribusiness). nadhani itabidi tuweke na maana ya neno biashara kilimo ili tuwe sawa. kwa kifupi tu kilimo bado kinachangia kwa kiasi kikubwa sana katika uchumi wa magharibi. Kumbuka kuanzia kulima shambani, makapuni yanayo fanya usindikaji, migahawa, mahoteli, nk. Vyoote vinaingia kaitka Agribusiness. Na ukitaka kupima mchango wa kilimo inabidi uangalia ungoezeko la dhamani huku kote. Kwa hiyo kusema uchumi wa nchi za magharibi hautegemei tena kilimo kama sisi sio ukweli. Tofauti iliopo ni kwamba kwetu ongezeko la dhamani katika kilimo ni ndogo
sio umuhimu wake
Tatu nakubaliana kabisa na wewe kwamba kama wote tunazalisha kahawa inakuwa ngumu kuuziana kahawa. Lakini sio kwa ajili ya umaskini wetu, hapana, bali kwa ajili wote tuna bidhaa inayofanana. Nadhani utakubaliana na mimi hii mifumo ya uchumi tumeridhi toka kwa hao hao wa magharibi. Lakini swali ni Je nilazima tuendelee nayo hata kama haitupi maslahi yoyote au yakutosha? Swala linabaki pale pale kuangali na kukimbilia soko moja la magharibi. Mfano uliotolewa wa wakongo au Uganda kutaka mchele wetu ni mzuri sana. Jiulize kwa nini tusiweke nguvu katika kuzalisha huu mchele na kuuza? Au mpaka tuuze kahawa US na Tokyo ndio biashara? We are too conversional na inaonekana hatutaki kubadili huu mfumo wa kinyonyaji (usiniulize kwa nini maana sina jibu kwa sasa)
Mwisho kabisa, ninapoongelea bitter pill simaanishi kwamba wanaimeza kwa sasa. Bali ukisoma fresh utaona nasema wao kubadili uwanja uwe flat ni ngumu sana ten asana. We need a middle class. This we agree. But I go further and say WE HAVE TO STOP SEEING DEVELOPED COUNTRIES AS THE ONLY POSSIBLE MARKET FOR OUR PRODUCE. Mnaijeria natumia sana viazi vikuu, magimbi, mihogo n.k. na sisi tuko katika sehemu nzuri kuzalisha kuliko yeye, kwa nini tusiangalie kuzalisha kwa ajili ya hilo soko? Tunaweza kusema hivyo hivyo kwa masoko mengi. Kinachotakiwa lazima tuanzie mahali fulani. Middle class haidondoki toka juu bali inahitaji kufanyiwa kazi kubwa.
Eddy, unayoyasema yanamake sense, lakini kumbuka kuwa lile suala la purchasing power linamatter pia. Kumbuka hata masuala ya pertnership hizi ndogondogo (SADC, COMESA, ECOWAS) vinatuletea matatizo sana.
Iwapo tunashindwa kuendesha mambo haya huku kwetu, unadhani tutakuwa katika nafasi gani tunapoenda WTO bila kuwa na ajenda na mkakati unaoeleweka?
Mimi siamini yametushinda, bali watu wanataka tuamini yametushinda. Ukiangalia Ujazo wa biashara katika haya masoko utakuta kwa kiasi kikubwa unakaribiana na what we export to US, na EU. Kwa hiyo kikubwa hapa ni namna gain ya kuyatumia zaidi haya masoko. Mpaka sasa bado Tanzania tunavutana kurudi au kutokurudi COMESA. Ni jambo la ajabu kabisa. Wafanyabiashara ambazo nyingi zilikuwa katika bidhaa za kilimo kama Unga nk. Wanasema wanalihitaji hili soko, lakini bado tunajivuta sana. Ukiangalia sababu za kujitoa huko zote ni siasa tupu. Hakuna sababu hata moja yakichumi inayoonyesha tumefaidika vipi tangia tutoke COMESA. Ndio maana anayosema Masanja ya siasa za zamani naunga mkono. Maamuzi ya kisiasa yasiyo na backing ya report za kitaalamu katika fani husika hayatatufikisha kokote.
Eddy, Soko ni muhimu mno...kama leo tunalia na EAC, SADC, COMESA..tutaweza kwenda Juba kweli? lazima tuwawezeshe wananchi kuwa na uwezo wa kununua! thats what China has aggressively done! bila kuwa na tabaka la kati..hata kama ungekwenda kuinvest wapi..huwezi fanikiwa.
Sasa hapa ndio penyewe. Swali je wao wamewezaje? Au na wao middle class ilikuwepo siku zote? Au kwa mataifa ya East Asia yanayojulikana kama Big Tigers yamewezaje? Kikubwa ni biahsa kati yao, pamoja na mambo mengine. Kwa sasa zaidi ya asilimia 75 ya export za china malighafi zake zinatengenezwa na nchi jirani. Kwa hiyo kama ni suti, nyusi anasokota Fulani namwuzia mwingine, kifungo nchi nyingine yeye anamalizia. On that way the benefits of value added along various value chains zinafaidhisha watu wengi na hivyo kuinua vipato vyao. Nadhani kwa sisi sehemu nzuri sana ya kujifunza ni huko East Asia maana miaka 30 iliyopita walikuwa kama sisi au chini yetu.
Na pia tukumbuke kuzalisha kwa gharama za chini na kwa ubora wa juu ili bidhaa tunazozalisha ziweze kushindana katika soko la kimataifa. Tukifanya hivyo tunaweza kuwapiku wachina wanaosambaza bidhaa duni duniani kote lakini zinagombea kwa sababu zina bei ya chini.
Hivi tulishaamua kuwa foreign policy yetu inajikita kwenye economic diplomacy? What happened to mkakati wa kutekeleza hilo?
Kwa sasa ukiondoa ruzuku za magharibi tunazalisha katika garama ndogo sana sana. Mfano garama ya kuzalisha hekta moja ya pamba Tanzania ni dola za marekani 178, wakati kuzalisha the same SA ni US$ 256, India ni US$ 359, na USA kwenyewe ni dola 932. kwa hiyo kama ni kuzalisha kwa garama ndogo, bidhaa zetu nyingi ziko katika medani hio.
Swala ni hilo la ubora, Hili ni soo, maana wanalitumia kama nyenzo ya kuweka masharti katika masoko yao. Hapa ndipo ambapo tunarudi haswa kwenye Mada ya kwa nini WTO negotiations haziwezi kufanikiwa.
Nimefurahishwa sana na michango ya watu kwenye hili swala. Msimamo wangu ni kwamba tanahitaji kutengeneza mbadala wa soko la magharibi. Natutaweza kufanya hivyo kwa kuanza kuangalia mahitaji yetu na kuyajeuza yawe bidhaa ambazo tutauziana. Taratibu tatajenga sio soko tu bali pia the famous middle class. Mjadala uendelee