Wydad kuishtaki Simba kwa kumtangaza Seleman Mwalimu kuwa mchezaji wao

Wydad kuishtaki Simba kwa kumtangaza Seleman Mwalimu kuwa mchezaji wao

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Klabu ya Wydad Casablanca imekanusha taarifa ya kufikia makubaliano na Simba SC juu ya mshambuliaji Selemani Mwalimu 'Gomez' kusalia kwa Wekundu hao wa Msimbazi kwa msimu mmoja zaidi wa mkopo ikidai taarifa hiyo haina ukweli wowote na kwamba klabu hiyo haijasaini makubaliano yoyote ya mkopo kuhusu mchezaji huyo baina ya vilabu hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa yake ya leo Julai 22, 2026 kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Wydad AC imesema Mwalimu bado ana mkataba na klabu hiyo na kwamba yupo kwenye mipango ya klabu hiyo na kubainisha kwamba benchi la ufundi la klabu hiyo linamtegemea kwa ajili ya kampeni zijazo na anatakiwa kurejea kwenye timu hiyo.

Zaidi ya hayo, Wydad imesema ina haki zake zote za kuchukua hatua inayoona inafaa kulinda maslahi yake huku ikiwakumbusha mashabiki kuthibitisha habari za uhamisho na kikosi kupitia njia zao rasmi ili kuepuka taarifa potofu.

Haya yanajiri masaa kadhaa baada ya Simba SC leo Julai 22, 2026 kutangaza kuwa Mwalimu ataendelea kusalia klabuni hapo kwa mkopo wa mwaka mmoja mwingine akitokea Timu ya Wydad Casablanca ya Morocco.
 
Wydad wanapenda kesi kama wahaya hapo mnyama kayakanyaga
 
Back
Top Bottom