Wydad watamkamia Denis Kibu

Wydad watamkamia Denis Kibu

Dhihaka zilikuwa nyingi dhidi ya Denis Kibu ila katika wachezaji ambao wamekuwa wanacheza kwa kiwango kikubwa kwa miezi minne na zaidi Kibu ni mmoja wao. Najivunia kuwa mmoja wa watu ambao nimekuwa namtetea. Hayo tuyaache kidogo maana ni kibwagizo tu.

Katika mechi ya Raja vs Simba kule Morocco, Kibu alicheza gemu ya hali ya juu na Wydad walimuona live bila chenga. Baada ya hapo zimepita game kadhaa ikiwemo dhidi ya Ihefu na Yanga na huko kote amekiwasha akitoa maassist na kufunga pia. Huko kote Wydad wamemuona pengine tena live bila chenga.

Nina uhakika ataanza gemu ya kesho na Wydad watamuwekea target kwenye kichwa chake. Inabidi tahadhari zichukuliwe kwa sababu Kibu anacheza mpira wa nguvu na kuna wakati wa kugombea mipira huwa anakataa kabisa kushindwa na kupelekea kupata kadi. Napendekeza akipata kadi ya kwanza, akumbushwe kuongeza tahadhari au ikibidi afanyiwe sub ili kuepuka kadi nyekundu.

Tahadhari ni bora kuliko shari.

Inawezekana.....

Anaebisha kuimarika kwa Kibu asubiri mechi ianze kisha akamuulize Sakho pale benchi: NI KWANINI AMEPANGWA KUANZA KWA WACHEZAJI WA AKIBA?
😃😅😄😂

Ni rahisi tu
 
Wamempiga vipepsi na mabuti hadi Kibu Mkandaji kashindwa kumaliza gemu.
 
Back
Top Bottom