X ameninunia!!!

X ameninunia!!!

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
378
Habari jf?
Jamani mimi ni mwanamke ambaye nilikuwa na mpenzi wangu toka 2014 mpaka 2016 ambapo mwanzo tulipendana sana na kujaliana. Mwaka 2016 tuliachana tena aliniacha kwa kunichoka tu kwani hakuwa na sababu ya maana aliyonieleza.
Nililia na kupitia kipindi kigumu hadi kufikia kuwekwa chini na ndugu zake ili kunifariji kwani nilijulikana kwao.
Baada ya mapito hayo nilikaa sawa. Undugu kati yangu na ndugu zake haukukatika. Tulijuliana hali na kusaidiana.
Toka 2016 hadi sasa maisha yetu kati yangu na x yalikuwa ni anaweza kukaa mwezi pasipo kunitafuta but inatokea siku ananipigia na kunijulia hali.
Mwaka huu aliniomba msamaha na akanijulisha kuwa amepata girl wake wanayependana nae sana. Hivyo hataki tukae kwa ugomvi na tuendelee kusaidiana kila inapobidi.
Binafsi kusameheana ilikua ni nzuri kwangu lakini suala la ukaribu nae sikuona umuhimu wa kuwa karibu na x na ukizingatia huyo girl wake hajawahi kumuona zaidi ya kuongea nae kwa simu na wanaishi mikoa tofauti.
X niliamua kumchukulia kama rafiki wa kawaida na sio kumpa special care kama mwanzo. But kwa jinsi anavyotaka ni ile special care kwani anaweza kuniambia kitu cha ndani ambacho naamini anapaswa kumwambia girl wake.
Nimejaribu kumpuuza kila anaponitengenezea mazingira ya kumpa special care mfano kufanya nae maendeleo au akipata tatizo niwe wa kwanza kumjali kabla ya mtu yoyote.
Nimemuignore kwenye vitu vingi sana namjibu kama rafiki wa kawaida ambaye siku yoyote naweza nisiwe nae wala kumuona but ameninunia from no where.
Kuna mzigo wake alipaswa kuchukua toka kwangu ila hapokei simu wala kujibu msg.
Jamani mtu kama huyu ananichukulia kama mama huruma au bado anataka niendelee kumjali kwa kuwa mpenzi wake hamjali ivo au ni kitu gani?
Naombeni mnisaidie mawazo yenu.
 
Me mwenyewe nimemnunia bidada 2 yrs now.Ila anapiga simu sn et niwe rafiki tu.Na niwe nampa ushauri.
 
Kitendo cha kukubali kuwasiliana ex wako et rafiki tu wa karibu ndio ulipokosea, ndio alijua kua anaweza akarud kwako siku yoyote ukakubali,sasa huo mzigos uupeleke kwa nduguze?? Lazima aje achukue yeye? Binti move on kama hataki s basi
 
Wanaume tuna mbinu nyingi sana, nimependa swaga za jamaa.

Amekupiga chini, katafuta demu mwingine, ila karudi kwako kwa gia hiyo na anaendelea kula huku na huku.
 
Habari jf?
Jamani mimi ni mwanamke ambaye nilikuwa na mpenzi wangu toka 2014 mpaka 2016 ambapo mwanzo tulipendana sana na kujaliana. Mwaka 2016 tuliachana tena aliniacha kwa kunichoka tu kwani hakuwa na sababu ya maana aliyonieleza.
Nililia na kupitia kipindi kigumu hadi kufikia kuwekwa chini na ndugu zake ili kunifariji kwani nilijulikana kwao.
Baada ya mapito hayo nilikaa sawa. Undugu kati yangu na ndugu zake haukukatika. Tulijuliana hali na kusaidiana.
Toka 2016 hadi sasa maisha yetu kati yangu na x yalikuwa ni anaweza kukaa mwezi pasipo kunitafuta but inatokea siku ananipigia na kunijulia hali.
Mwaka huu aliniomba msamaha na akanijulisha kuwa amepata girl wake wanayependana nae sana. Hivyo hataki tukae kwa ugomvi na tuendelee kusaidiana kila inapobidi.
Binafsi kusameheana ilikua ni nzuri kwangu lakini suala la ukaribu nae sikuona umuhimu wa kuwa karibu na x na ukizingatia huyo girl wake hajawahi kumuona zaidi ya kuongea nae kwa simu na wanaishi mikoa tofauti.
X niliamua kumchukulia kama rafiki wa kawaida na sio kumpa special care kama mwanzo. But kwa jinsi anavyotaka ni ile special care kwani anaweza kuniambia kitu cha ndani ambacho naamini anapaswa kumwambia girl wake.
Nimejaribu kumpuuza kila anaponitengenezea mazingira ya kumpa special care mfano kufanya nae maendeleo au akipata tatizo niwe wa kwanza kumjali kabla ya mtu yoyote.
Nimemuignore kwenye vitu vingi sana namjibu kama rafiki wa kawaida ambaye siku yoyote naweza nisiwe nae wala kumuona but ameninunia from no where.
Kuna mzigo wake alipaswa kuchukua toka kwangu ila hapokei simu wala kujibu msg.
Jamani mtu kama huyu ananichukulia kama mama huruma au bado anataka niendelee kumjali kwa kuwa mpenzi wake hamjali ivo au ni kitu gani?
Naombeni mnisaidie mawazo yenu.
dah
 
Huyo jamaa hakuoi wewe wala huyo demu wake mpya, kiufupi jamaa ni muhuni tu, na hiyo mbinu ya kukuchunia ndio huwa mbinu yetu ya mwisho ambayo hakuna kiumbe cha kike kinaweza kuruka hiyo, kama ni salaha basi jamaa hapo kavuta silaha ya nyuklia, na kadri utakavyoendelea kushangaa anavyokuchunia ndo jamaa anafurahi hapo.
 
kuna movie ya kihindi.niliiona.
Kuna jamaa alimwambia mwenzie.
WANAWAKE WANA HURUMA KUWASHINDA WANAUME.
Leo ndo nayaamini Yale maneno.
 
Back
Top Bottom