X Vs Y

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
[emoji112][emoji112]

Maisha ni safari na hapa duniani katika hiyo safari huwa tunakutana na mengi sana ,tunakutana na vitu vya tofauti tofauti.

Hapa duniani vitu vingi hutofautiana kitu X unakuta kipo tofauti na kitu Y tena yawezekana vyote vikawa ni vya jamii moja lakini havifanani.

[emoji39]....X Vs Y twende mjomba nchumali....[emoji39]
 
Azam Complex Stadium
  • Unapatikana Mbagala
  • Unachukua mashabiki 10,000
  • Ulijengwa 2010
  • Ni artificial turf
  • Mmiliki ni Azam

Vs

Mkapa Stadium
  • unapatikana Temeke
  • Unachukua mashabiki 60,000
-Ulijengwa 2007
  • Ni wa nyasi asili
  • Mmiliki ni serikali
 
Mchepuko
  • wana gharama
  • Wanakuwaga na mahaba sana yawe ya uwongo au ukweli
  • Wanapenda pesa
  • Wakimshika mume wa mtu hawamuachii
  • Wanatumia sana ndumba
  • Kama huna hela mapenzi hakuna
Vs

Mke
-Hana gharama
  • Akishawekwa ndan mahaba hupungua
  • Hata kama huna hela sio ishu sana yupo ndan tayar
  • Ndumba sio sana
  • Huu ni uwanja wa nyumbani hata kama hela hamna mtaishi tu
 
Mwenye kitambi
  • Raia wanajua hela ipo
  • Wavivu
  • Wengine hushindwa kufunga kamba za viatu wakiwa wamesimama
  • Wanapenda sana kuchomekea
  • Wanachoka mapema kwenye game

Vs

Mti mkavu
  • Hata kama una hela hadi raia wakujue kama zipo
  • Wazee wa mazoez
  • Kamba ya viatu inafungwa kivyovyote vile
  • Hawa n wazee wa kupeleka moto
  • Wanakula sana lakin hawanenepi
 
Mvulana
  • bado anaendelea kukua hajajielewa bado
  • hajui maisha yalivyo practically
  • anakula na kulala kwa wazazi
  • kila kitu anajua yeye
  • anavaa mlegezo na kupaka shedo
  • Marioo
  • anashinda kijiweni
  • ana nyoa kiduku na minyoo ya ajabu ajabu

Vs

Mwanaume
  • ameshakuwa na anajielewa
  • maisha anayajua yalivyo
  • anajitegemea hata kwa kupanga
  • ana sikiliza ushauri na kuufanyia kaz kama n mzur
  • ana vaa kiheshima
  • anaenda kazini au kwenye kibarua kama kijiweni ni baada ya kutoka huko
  • ana nyoa kistaarabu
  • ana tafakar kabla ya kunena na kutoa maamuzi
 
Leaders Vs Manager

Leaders hutengeneza vision, managers hutengeneza goals.

Leaders hawa ni change agents, managers hawa humaintain status.

Leaders ni unique, managers wazee wa kucopy.

Leaders wapo tayar kuchukua risks, managers hawa hu control risk .

Leaders hufikiria vitu vya muda mrefu, managers hufikiria vitu vya muda mfupi.

Leaders hawa hukua wenyewe na kujiamini zaidi wenyewe, managers hawa hutegemea zaidi ujuzi uliopo na ambao umeshawahi kutoa matokeo chanya.

Leaders hawa hutengeneza mahusiano, managers hawa hutengeneza mifumo na michakato.

Leaders hawa hufundisha, managers hawa huelekeza.

Leaders hutengeneza mashabiki wao watakao wakubali, managers hawa huwa na waajiliwa.
 
Management
  • Ni ule ujuzi wa kuweza kuorganize watu,lasilimali na kuhakikisha kazi inafanyika
  • kuhakikisha sera za sehemu husika zinafuatwa
  • ipo chini ya administration
  • Hapa Key person ni manager
  • Huamua nani atayefanya kazi na itafanywaje hiyo kazi
  • Hutumiwa sana na zile taasisi ambazo zipo kwa ajili ya faida zaidi

Vs

Administration
  • Hupanga malengo ya taasisi husika pia huandaa sera muhimu za hiyo taasisi
  • Huunda sera za sehemu husika
  • Hucontrol shughuli zote za hiyo taasisi
  • Hapa key person ni administrator
  • Hupanga na kutoa maelekezo nini kifanyike na kwa wakati gani
  • Hutumiwa na maofisa wa serikalini,jeshini,hospital,club, taasisi za kidini,mashuleni.
 
Android TV Vs Smart TV

- Android TV ina utajiri wa Application kwa sababu unasapoti play store , Smart TV yenyewe haina application nyingi kutoka kwenye app store yake utapata zile maarufu kama YouTube,prime video,Netflix.

- Android TV yenyewe ina update apps zake mara kwa mara developers wanahitaji kwenye hilo , Smart TV yenyewe update zake ni vigumu kidogo kuzipata.

- Android TV ina kitu imetengenezewa ikijulikana kama deeply integrated Chromecast feature ambayo ni very useful inayofanya raisi zaid kuunganisha smart phone yako na tv ambapo hii feature unapata full screen mode,sauti na kubwa zaidi picha haipungui ubora wake , Smart TV yenyewe ina feature yake pia ya screen mirroring ambapo hii inaugumu kidogo kwenye kuunganisha ukilinganisha na ile ya android tv shida ya hii kitu inapunguza ubora wa picha.

- Android TV yenyewe ina feature matata pia ya voice assistant(Google Assistant) ambapo inasaidia sana kuto kutype mara kwa mara , Smart TV yenyewe haina hii kitu yenyewe inakuja na full size keyboard ambapo inabid utype pale unapohitaji kutafuta kitu.

- Android TV yenyewe ina ugumu flan hivi kwenye ku navigate na kutumia ukilinganisha na Smart TV , Smart TV yenyewe ni rahisi ku navigate pamoja na kutumia.

- Android TV yenyewe kwenye ufanyaji kazi/performance ipo slow kidogo ukilinganisha na Smart TV , Smart TV yenyewe ipo vizur kwenye performance kutokana na ile leya/lining yake ya silver.

- Android TV yenyewe kwenye upande wa firmware update haiji mara kwa mara lakini utaendelea kutumia updated apps kwa vile update yake huwa na uwezo wa kukaa muda mrefu, Smart TV yenyewe ni tofauti itabidi usubir kwa muda hiyo firmware update yake hadi wajamaa watakapotoa nyingine au unaweza ukaupdate kupitia Android TV set-top box or dongle na kuweka kwa Smart TV yako lakini hata ukiweka hii haiabadili firmware (Tizen OS or webOS) yako na kuwa update kwa vile hivi ni vitu viwili tofauti
 
LCD Vs LED

- LCD kirefu chake ni liquid crystal display ,LED kirefu chake ni light emitting diode

-LCD inatumia mwanga wa fluorescent ,LED yenyewe inatumia diodes ambazo ndizo hutoa mwanga

- LCD hii miale ya fluorescent kwenye LCD TV huwekwa nyuma ya kioo ,LED hutofautiana hizi diodes ambazo ndizo hutoa miale kwenye LED TV inaweza wekwa nyuma ya kioo au pembezoni.

- LCD hutumia na huitaji Mercury katika uzalishaji wao hii mercury sio rafiki kwa mazingira ,LED haihitaji mercury kwenye uzalishaji wao kwa maana hiyo n rafik kwa mazingira.

- LCD yenyewe ni bei nafuu ukilinganisha na LED ,LED yenyewe ni gahli kuliko LCD.

  • LCD screen zake zina ukubwa wa 13 hadi 57 inches ,LED screen zake huenda mpaka 90 inches.
  • LCD TV husave umeme kati ya asilimia 30 hadi 70 ,LED TV zenyewe husave umeme asilimia 50.

- LCD TV hazitoi picha nzuri iliyonyooka kama ilivyo kwa LED TV ,LED TV zenyewe zinatoa picha nzuri na bora zaidi na ndiyo maana siku hizi TV nyingi ni LED.

- LCD hutumika kwenye portable electronic games,l cameras na camcordersIn,video projection systems,electronic billboards,Computer monitors,Flat-panel television LED hutumika kwenye digital watches,digital computers,cell phones,bulbs and tubes,automotive heat lamps,camera flashes,calculators,aviation lighting,microprocessors,burglar alarms systems,traffic signals hivi ni baadhi tu na vinginevyo.
 
Iphone Vs Android
- Iphone ipo vizuri sana kwenye swala zima la ulinzi kwa sababu apps nyingi zinakuwa monitored na apple wenyewe na unaruhusiwa kupakua apps kutoka app store pekee, Android yenyewe ipo wazi kwenye swala la ulinzi haiko poa huku app unaipata popote pale sio lazima play store.

- Iphone apps zake hazicrush mara kwa mara kama android , Android yenyewe saa yoyote app inacrush.

- Iphone home screen yake hauwezi kuiboresha(not customizable) , Android yenyewe ina uwanja mpana utakavyo wewe.

- Iphone apps store yake ipo better organized kulinganisha na android, Android ni kinyume chake.

- Iphone kuna baadhi ya apps kwenye app store zipo vizuri zaidi ukilinganisha na android , Android yenyewe ipo kinyume chake.

- Iphone kwenye app store kuna apps nyingi za kulipia na zenye matangazo machache , Android yenyewe free apps za kumwaga ila jipange kwa matangazo.

- Iphone zile default apps zake zinazokuja na IOS yake huwa ziko less advanced kulinganisha na Google apps za kwenye android , Android ni kinyume chake.

- Iphone sio rahisi kusafirisha mafile ya mziki na video kutoka kwa iphone kwenda kwenye windows PC hadi upakue na kuweka itunes kwa pc yako kwanza , Android kwenyewe unapeta tu mwendo mdundo bila shida yoyote.

- Iphone haina kitufe cha kurudi nyuma (back [emoji774] button) , Android kitufe cha kurudi nyuma kipo.

- Iphone update zake ni za mara kwa mara na ziko vizur zaid ukilinganisha na android , Android ni kinyume chake.

- Iphone wapo vizuri sana kwenye swala zima la usiri wa taarifa zako na wanazilinda haswa tofauti na Google kwa upande wa android kwa sababu google anapata pesa kupitia matangazo kulingana na interest zako unazozibainisha lakini apple wenyewe hawategemei matangazo bali pesa wanapata kupitia mauzo ya simu zao , Android yenyewe ni kinyume chake sasa.

- Iphone hawana option ya kuongeza nafasi ya kuhifadhia simu kama ilivyo kwa Android na ndiyo maana wanajitajidi sana kuweka storage kubwa kwenye simu zao huwezi kuta iphone ina 2GB storage , Android yenyewe inayo option hiyo wanakuwekea sehemu ya memory card ambayo itakusaidia kuongeza storage yako ya simu hata kama simu yako ina storage 1GB kupitia microSD hakuna tatizo itakubusti.

- Iphone yenyewe kwa upande wa battery hawana battery zenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chaji wanaweka battery ndogo nyembamba ili simu zao zisiwe nene ziwe na muonekano mzuri ,Android yenyewe wako tofauti hata kama simu itakuwa nene vipi hawajali sana huku battery zao zina uwezo wa kuhifadhi chaji muda mrefu kwa sababu ni kubwa utakuta 5000mAh.

- Iphone imewekeza sana na inajua thamani yake kwenye soko wapo vizur na ndiyo maana miaka na miaka wapo tu na thamani yao ile ile , Android wenyewe sio kivile na ndiyo maana kuna kampuni nying sana na nyingine zimeshakufa.
 
X Chromosome Vs Y Chromosome
*Vina saba hivyo ndivyo mahususi kwenye swala zima la jinsia ya mtoto.

- X Chromosome yenyewe mahususi kwa jinsia ya kike ,Y Chromosome mahususi kwa jinsia ya kiume.

- X Chromosome ipo kote kote kwa mama (XX genotype) na kwa baba pia (XY genotype) ,Y Chromosome yenyewe ipo kwa baba tu.

- X Chromosome yenyewe ni kubwa ,Y Chromosome yenyewe ni ndogo.

- X Chromosome inatawala kwa kuwa na uwingi ikiwa na 5% ya binadamu wote ,Y Chromosome yenyewe ipo chini ikiwa na 2% ya binadamu wote.

- X Chromosome kwa vile haina XY genotype haina pia SYR gene ,Y Chromosome yenyewe inayo SYR gene ambayo ni mahususi katika ukuaji wa testes(kiungo kinachotengeneza shawaha).

- X Chromosome kwa Idadi ya genes yenyewe inayo 1000genes ,Y Chromosome kwa Idadi ya genes yenyewe inayo 70genes.
 
Choo Cha Kukaa Vs Choo Cha Kuchuchumaa

- Cha Kukaa chenyewe unakaa , Cha Kuchuchumaa chenyewe unachuchumaa.

- Cha kukaa ni rafiki kwa wagonjwa na wazee ambao hawawezi Kuchuchumaa ,Cha Kuchuchumaa chenyewe ni kinyume chake.

- Cha kukaa hasa cha jumuiya ni rahisi sana kupata magonjwa hasa UTI kwa wanawake ,Cha Kuchuchumaa chenyewe ni tofauti kina uwanja mpana tofauti na Cha kukaa.

- Cha kukaa kisayansi sio rafiki kwa afya ya mtumiaji haya kubwa haitoki kirafiki ,Cha Kuchuchumaa chenyewe haja kubwa inashuka vizur sana bila nguvu yoyote kwa urahisi na ndiyo njia ya asili gravity inakurahisishia kazi .

- Cha kukaa unaburudika kipo comfortable wakati unashusha vitu hata kuchat unachati na gaazeti unasoma kabisa ,Cha Kuchuchumaa chenyewe mtihani maana ukichuchumaa mda mrefu misuli ya miguu inauma na kutokuwa comfortable.

- Cha kukaa chenyewe ni gaharama lazima uwe na maji ya kutosha pia ,Cha Kuchuchumaa chenyewe hakina gharama
 
TikTok Vs Likee

- TikTok makao makuu yake yapo china ,Likee makao makuu yake yapo Singapore.

- TikTok aina yake ya platform ni PGC (Profession Generated Content) ,Likee aina yake ya platform ni UGC (User Generated Content).

- TikTok machaguo yaliyopo kwenye kuedit video kuna emoji,text,flames,video trimming na mengineyo ,Likee machaguo yaliyopo kwenye kuedit video kuna filters zake za nywele zinauhalisia kama wa nywele za ukweli vile,4D magic na pia ina effect super sana.

- TikTok machaguo ya muziki wakati unaedit video yako ni up to date kwa sababu third party apps huweka nyimbo zao ,Likee machaguo ya muziki wakati unaedit video yako kuna built-in library ya nyimbo ambayo ipo limited lakini pia unaweza kuongeza nyimbo yako mwenyewe kutoka kwa kifaa chako cha simu

- TikTok yenyewe lengo lake limejikita zaidi kwenye ujamaa wa kidigitali kwa wateja wake kupost videos ,Likee yenyewe watumiaji huweza kuona video live na kutengeneza marafiki wa karibu.

- TikTok yenyewe ina watumiaji wengi ,Likee yenyewe ina watumiaji wachache.

- TikTok yenyewe imeanza kutumiwa 2016 ,Likee yenyewe imeanza kutumiwa 2017.

- TikTok ni kama pombe ikikuingia kwenye damu kuchomoka sio rahisi ,Likee yenyewe pia sio mnyonge ila haizidi TikTok.

- TikTok yenyewe ukiwa maarufu ndipo utatengeneza hela kupitia hii app kwa sababu ina angalia sana likes na views ,Likee yenyewe hata kama sio maarufu kutengeneza hela sio ishu sana kwa kupitia virtual gifts kutoka kwa mashabiki wako.
 
Sex Vs Gender

- Sex ni ule utofauti wa kibaiologia na muonekano wa macho kati 6 mwanamke na mwanaume mfano homoni na viungo vya uzazi

Vs

- Gender ni zile tabia zinazotazamwa kijamii zaidi kati ya mwanaume na mwanamke mfano majukumu na mahusiano kati ya baina ya makundi ya wanawake na wanaume.View attachment 2104017View attachment 2104018
 
Computer RAM Vs Computer ROM
- RAM kirufu chake ni Random Access Memory ,ROM kirefu chake ni Read Only Memory.

- RAM hii ni muhimu sana kwa sababu operation system, program zote na data hii ndiyo inahusika katika ufanyaji kazi wa hizo ,ROM yenyewe inaprogram ambayo hutumika pale computer inapowaka na pia inafanya uchunguz wa awali pale computer inapowaka kujua kama kuna shida au Iko poa.

- RAM hapa zile data za kwenye RAM zinaweza kuboreshwa,kubadilishwa au kufuta ,ROM hapa zile data za kwenye ROM ziko fixed yaan hauwez kuzifuta wala kuziboresha(read only memory).

- RAM yenyewe huifadhi kumbukumbu kwa muda mfupi wakati unatumia program fulani na ndiyo maana unashauriwa kusave isije potea pale computer inapozima ,ROM yenyewe ni huifadhi kumbukumbu za system na zipo fixed ( virtually indestructible ).

- RAM yenyewe hupoteza kumbukumbu pale umeme unapokata ,ROM huifadhi data hata wakat ambapo umeme umekatika.

- RAM hutumia nafasi kubwa sana hadi GB inafika kulingana na programs zinazofanya kazi muda huo ,ROM hapa haitumii nafasi yoyote kwa sababu ROM haitumiki kwenye hizo program zinazofanya kazi muda huo.

- RAM ni bei nafuu ,ROM ni ghali.

- RAM yenyewe ipo fast ,ROM memory yenyewe ipo extremely fast kuliko ROM.

- RAM aina zake ni dynamic RAM & static RAM ,ROM aina zake ni PROM (programmable read-only memory) like CD ROM, EPROM, (Erasable Programmable Read-only Memory) EEPROM.(Electrically Erasable Programmable Read-Only Memory) .

- RAM hapa chips zinazopatikana ni kama vile 2GB, 4GB, 8GB na kuendelea na kampuni zinazotengeneza ni kama vile Corsair, Kingston ,ROM mfano wa ROM ni cartridge za video game consoles na computer BIOS.

- RAM yenyewe huifadhi data zake kwa MBs ,ROM yenyewe huifadhi data zake kwa GBs.
 
Photography (photo) Vs Picture

- Photo ni mojawapo ya picha , Picha inaweza ikawa tofauti zaidi ya photo.

- Photo hii inaweza kuchukuliwa na yeyote yule kwa sababu unatumia kifaa kama kamera kupiga , Picha yenyewe sio wote wenye uwezo nayo kwa sababu inapatikana kwa kuchora,kupakwa rangi na ikatengenezwa kwenye computer.

- Photo ni picha ,Picha inaweza ikawa photo.

- Photo hii hutoa kitu halisi kama kilivyo katika mazingira halisi , Picha yenyewe ni tofauti.

 
Sperm Vs Semen
- Sperm hii ni seli ya kiume ya uzazi ,Semen haya ni majimaji(fluid) ya kiume ya uzazi ambapo hizi sperm hupatikana humo.

- Sperm hii huzalishwa na wote wanyama na mimea pia ,Semen hii huzalishwa na wanyama wa kiume pamoja na wale wanyama wenye jinsia zote mbili(hermaphrodites).

- Sperm huzalishwa na spermatozoa kwenye korodani ,Semen huu ni mkusanyiko wa kumiminika(fluid) ambapo huzalishwa na vesicles, prostate gland, and bulbourethral glands.

- Sperm hii ni seli ambayo huwezi kuiona kwa macho yenye umbo la mviringo(oval),kichwa na mkia mrefu ,Semen hiki ni kimiminika ambacho huvutika chenye rangi ya whitish-gray ambacho huonekana kwa macho.

- Sperm hii ni seli ambayo ndiyo huunda semen ,Semen hiki ni kimiminika ambacho ndani yake kuna sperm.

- Sperm hii ndiyo seli kwa maana hiyo ndiyo iliyobeba vile vina saba vya uzalishaji kwa upande wa mwanaume kwenye urutubishaji wa yai la kike ,Semen hiki ni kimiminika ambacho kinabeba hiyo sperm kwenda kurutubisha yai.

- Sperm haonekani kwa macho yetu haya ya kawaida ,Semen huonekana kwa macho yetu haya ya kawaida.
 
Mkuu @iwambof07 umeamua hasaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…