X Vs Y

X Vs Y

LCD Vs LED

- LCD kirefu chake ni liquid crystal display ,LED kirefu chake ni light emitting diode

-LCD inatumia mwanga wa fluorescent ,LED yenyewe inatumia diodes ambazo ndizo hutoa mwanga

- LCD hii miale ya fluorescent kwenye LCD TV huwekwa nyuma ya kioo ,LED hutofautiana hizi diodes ambazo ndizo hutoa miale kwenye LED TV inaweza wekwa nyuma ya kioo au pembezoni.

- LCD hutumia na huitaji Mercury katika uzalishaji wao hii mercury sio rafiki kwa mazingira ,LED haihitaji mercury kwenye uzalishaji wao kwa maana hiyo n rafik kwa mazingira.

- LCD yenyewe ni bei nafuu ukilinganisha na LED ,LED yenyewe ni gahli kuliko LCD.

  • LCD screen zake zina ukubwa wa 13 hadi 57 inches ,LED screen zake huenda mpaka 90 inches.
  • LCD TV husave umeme kati ya asilimia 30 hadi 70 ,LED TV zenyewe husave umeme asilimia 50.

- LCD TV hazitoi picha nzuri iliyonyooka kama ilivyo kwa LED TV ,LED TV zenyewe zinatoa picha nzuri na bora zaidi na ndiyo maana siku hizi TV nyingi ni LED.

- LCD hutumika kwenye portable electronic games,l cameras na camcordersIn,video projection systems,electronic billboards,Computer monitors,Flat-panel television LED hutumika kwenye digital watches,digital computers,cell phones,bulbs and tubes,automotive heat lamps,camera flashes,calculators,aviation lighting,microprocessors,burglar alarms systems,traffic signals hivi ni baadhi tu na vinginevyo.View attachment 2101653View attachment 2101654
Gusia na Plasma
 
Home Theatre vs Soundbar

- Home theater tukianza na ubora wa sauti yenyewe ipo better ukitaka kupata ile clear, crisp, impactful sound and a deep bass hii ndiyo yenyewe sasa na pia mziki wake husikika kila kona ya chumba , Home theater yenyewe ni kinyume chake.

- Home theater yenyewe sio rahisi kubeba kama ukitaka kuhamisha toka sehemu moja kwenda nyingine na ina nyaya nyingi , Soundbar yenyewe ni rahisi kubeba ni kipotabo na haina nyaya nyingi hata uzito pia sio nzito kama ilivyo home theater.

- Home theater kwenye gharama ipo juu kutokana na ile ubora wake wa sauti,ubora wa picha na features nyingine iliyonayo pia ina viunganishio(connectivities) vingi , Sound bar yenyewe bei yake ni rahisi haina viunganishio vingi na pia hutoa saut ya kiwango fulani.

- Home theater sio rahisi na sio wote wenye uwezo wa kuunganisha pale wanapotaka kuitumia kutokana na nyaya kuwa nyingi na spika nyingi wengine humuita mtu mwenye ujuzi ,Soundbar yenyewe ni simple na kuunganisha kwake ni rahisi pale mtumiaji anapotaka itumia.

- Home theater tukija kwenye customization yenyewe ina machaguo mengi kuna 2.1 ,3.1 ,5.1 ,7.1 ,9.1 so ni wewe tu kutegemeana na ukubwa wa chumba chako na mfuko wako unavyoruhusu ,Soundbar kwenye customization ipo simple na ina limitation zake.

- Home theater inachukua nafasi kubwa ya chumba so kama unakachumba kadogo bora uchukue soundbar ,Soundbar yenyewe inachukua nafasi ndogo na pia unaweza kuiweka ukutani na ikatulia bila shida.

- Home theater je unataka cinematic experience?? kama jibu ni ndiyo basi home theater system ndiyo jibu lako utaenjoy kwenye hilo ,Soundbar yenyewe ni tofauti haina hiyo kitu.
FB_IMG_1644173052389.jpg
FB_IMG_1644171605319.jpg
FB_IMG_1644173269061.jpg
FB_IMG_1644173362380.jpg
 
LED TV Vs Plasma TV

i.)Unene
- LED TV huwa nyembamba mara nyingi chin ya nchi moja ,Plasma TV huwa chini ya nchi 1.2 .

ii.)Matumizi ya umeme
- LED TV hutumia umeme kidogo ukilinganisha na Plasma TV.

iii.) Ukubwa wa kioo
- LED TV hii huenda hadi nchi 90 na huanzia nchi yoyote ambayo kiwanda kinataka ,Plasma TV yenyewe huanzia nchi 42 hadi 65 Panasonic wana model kubwa hadi inchi 152.

iv.)Muda wa kuishi(Life span)
- LED TV hii huenda hadi masaa 100,000 , Plasma TV hii huenda kati ya masaa 20,000 hadi 60,000.

v.)Gharama
- LED TV hii ipo juu kidogo ukilinganisha na Plasma TV.

vi.)Angle kwa mtazamaji
- LED TV yenyewe hutegemea sana na jinsi mtazamaji alivyokaa ule muonekano(brightness and color) wake wa screen hubadilika kulingana na mtazamaji angle aliyokaa ,Plasma TV yenyewe muonekano hubaki vile vile hata kama mtazamaji atabadili angle ya utazamaji.

vii.)Uwiano wa mwanga(contrast ratio)
- LED TV uwiano wake sio mzuri sana kama ilivyo kwa plasma tv hii hutoa mwanga mweupe mkali lakini pia hutoa miale mweusi inayong'aa ambayo humfanya mtazamaji awahi kuchoka macho anapotizama tv yake hasa kwenye chumba cha giza ,Plasma TV hii hutoa miale mweusi yenye giza na mweupe iliyofifia ambayo mara nyingi humfanya mtazamaji kuwa comfortable zaidi haiumuuzi macho anapoangalia tv na kwenye mwanga mkali plasma tv hautaona vizur kwenye mwanga hafifu hii ndiyo yenyewe macho yanachelewa kuchoka.

viii.)Uzito
- LED TV zenyewe ni nyepesi ukilinganisha na Plasma TV ambazo ni nzito.

ix.)Unene wa kioo(screen)
- LED TV kioo chake ni chembamba ,Plasma TV kioo chake ni kinene.

x.)Matumizi ya energy
- LED TV hutumia energy kidogo ukilinganisha na Plasma TV.

xi.)Watengenezaji(kampuni)
- LED TV hutengenezwa na makampuni yote ya TV ,Plasma TV hutengenezwa na Panasonic,LG,Samsung.

xii.) Ufanyaji kazi katika mazingira magumu
- LED TV chini ya nyuzi joto 50f contrast hupungua ,Plasma TV urefu wa futi 6500 huathiri Ufanyaji kazi wake kwa sababu ya gesi iliyopo ndani husumbuliwa na kufanya itumie nguvu ya ziada inapofanya kazi.

xiii.)Teknolojia inayotumia
- LED TV hii hutumia diodes ambazo hutoa mwanga ambapo baadhi ya hiI mianga huzuiliwa na liquid crystals ambazo huwa zipo kwa wima au mlalo na kuunda picha au taswira halisi ambayo hutokea kwa kioo na mtazamaji kuweza kuona ,Plasma TV hii taswira hutengenezwa kwa kutumia phosphors ambapo vyombo vidogo/tiny vyenye plasma huwekwa katikati ya sheets mbili za glass na kuzalisha mwanga wa ultraviolet kwa kioo kwenye maeneo ya phosphor ambazo huglow na kutengeneza picha ambayo sisi tunaiona.

xiv.)Ubora wa sauti
- LED TV kwa vile nyembamba hata speaker zake huwa ni ndogo ambapo hutoa sauti isiyo na ubora ukilinganisha na Plasma TV.

xv.)Umaarufu
- LED TV zenyewe zinajulikana sana na watu wengi hutumia hizi , Plasma TV zenyewe sio maarufu sana kwa watu wengine hata hawajui kama zipo mfano tu hapa Tz kama zipo basi zinahesabika lakini pia hizi ni maarufu sana kwa kuwa na size kubwa ya kioo/screen.
FB_IMG_1644181973216.jpg
FB_IMG_1644182045412.jpg
 
FBG Vs RBG

- FBG ni Fasting Blood Glucose ,RBG ni Random Blood Glucose.

- FBG ni ile sukari ambayo mteja anapimwa kabla hajala kitu chochote kile zaidi ya maji pekee ,RBG ni ile sukari mteja anapimwa baada ya kula kitu chochote chenye sukari iwe ya asili au viwandani.

- FBG hupimwa asubuhi ,RBG hii hupimwa muda wowote baada ya kula.

- FBG hii kwa kawaida inatakiwa iwe kati ya 3.9 hadi 5.6 mmol/L kwa wasio na kisukari kwa wenye kisukari huenda hadi 7 ,RBG hii kwa kawaida inatakiwa iwe kati ya 4.0 hadi 7.8 mmol/L kwa wenye kisukari huenda hadi 9.
FB_IMG_1644330237037.jpg
 
Premier league Vs La Liga
- Premier league inatumia sana nguvu na kusafirisha mipira kwa haraka haraka ,la Liga huku mchezaji ana uhuru mpana sana wa kuonesha utundu na ujuzi wake nafasi hiyo anayo ila premier league mabeki hufika kwa haraka sana na kuharibu mipango mapema mara nyingi hawatoi hiyo nafasi kwa washambuliaji mfano lile goli alilofunga Messi kwenye finale ya champions league dhidi ya Man U kwa sababu beki hazikumzuia mapema(defenders failed to close him down quickly) .

- Premier league wapo vizuri sana kwenye ugawaji wa haki za matangazo baina ya vilabu vikubwa na vile vya chini mfano msimu wa 2010 - 2011 Man u aliondoka na 60 millions euro huku Blackpool akisepa na 40 millions euro ,La Liga wanazingua kuna gap kubwa sana mfano 2011 - 2012 Madrid na Barca wakasepa si chini ya 116 millions euro huku Valencia akasepa na 40 millions euro na hiyo Valencia sio team ndogo kama ilivyo Blackpool na ndiyo maana Madrid na Barca wanatesa sana hivi vilabu vya chini vinapata pesa ndogo sana.

- Premier league vilabu vyake hushiriki mara nyingi sana kwenye michuano ya Europe na hufanya/vimefanya vizuri pia tofauti na vilabu vya La Liga.

- Premier league kuna ushindani sana wa vilabu vikubwa na vidogo mara nyingi vilabu vidogo huwapa changamoto vilabu vikubwa na vikikaa vibaya ubingwa hawachukui mfano mzuri alichokifanya Leicester city ,La Liga huku ni mteremko Madrid na Barca ndiyo wanabadilisha tu kuchukua kikombe cha ligi.

- Premier league ndiyo league pendwa duniani ,La Liga wanajitajidi ila hawajawafikia premier league na tena kama hivi Messi na CR7 hawapo imepoteza mvuto.

- Premier league wenye vibanda umiza huwa wanapiga hela sana kutokana na kupendwa kwa ligi hii ,La Liga huku ni tofauti kina game zake za kupiga hela.
FB_IMG_1644328525331.jpg
FB_IMG_1644328496002.jpg
 
BMW Vs Mercedes

Hebu ngoja tucheki kidogo tofauti ya hizi kampuni mbili maarufu na hii vita ya ipi bora ni ya miaka na miaka na hii vita haitakuja kuisha hebu ngoja tucheki kwa mwaka jana 2021.
i.) Matoleo mbalimbali waliyotoa
- Kampuni zote zimetoa matoleo mbalimbali ni mteja tu chaguo lake BMW wakatoa 3,5 na 7 series zikiwemo machaguo unique kama vile M,I,X na Z4 bila kusahau na SUVs , Mercedes naye hakuwa nyuma amatoa mbalimbali zikiwemo na SUVs lakini sedans zikapendwa zaidi na kujulikana zaidi kuanzia C class mpaka opulent S class kwa hili Mercedes alitoa matoleo mengi zaid

ii.) Performance
- Kampuni zote ni kubwa na zote ziko vizuri reliability ndiyo msingi wao miaka nenda miaka rudi.BMW wana faida moja wao hutengeneza injini ndogo na nyepesi mfano 3 na 4 series,M na X5 ni motor ndogo lakini ni powerful. Kama ni mpenzi wa injini kubwa na zenye high power basi nenda na Mercedes kama vile CLS - Class Sedan.

iii.)Vipi kuhusu mafuta
- BMW kwa vile injini zao ndogo sio tu nyepesi husaidia pia kusave mafuta ukija kwa Mercedes ni tofauti injini zao kubwa zinatoa power ya kutosha ambayo huitaji wese kwa wingi.

iv.)Usalama
- Kampuni zote zipo vizuri sana kwenye swala zima la usalama kwa watumiaji wake wanawajali wateja wao lakini Mercedes yupo vizuri zaidi kwa sababu wanatumia mfumo wa pre safe katika matoleo yake mengi ya magari anayotoa.

v.) Muonekano wa ndani
- Kuna tofauti kubwa sana baina ya hawa wawili Mercedes yeye emejikita zaidi kwenye utengenezaji wa cabin zilizo comfortable na luxury tukija kwa BMW wao hujikita sana kwa mteja kuhakikisha dereva anapata kile anachohitaji pale anapoendesha mfano mzuri ni 3 series lakin 7 series ndani ziko vizuri sana.

v.)Tekinologia
- Kampuni zote zipo vizuri kwenye hili sema kidogo Mercedes amemzidi BMW anatumia mfumo wa M-Brace ambao hutoa ulinzi,burudani na connectivity features ambapo kwenye gari kwa kutumia smartphone tu mifumo mingi ya kwenye gari unaweza kuicontrol(ana high tech features nyingi). BMW yeye anatumia mfumo wa iDrive ambao hucontrol vitu vingi kwenye gari pia kwa baadhi ya matolea kuna head up display na unaweza kucontrol vitu vya kwenye gari kwa sauti.

vi.) Ile feeling wakati unaendesha
- Kwa vile BMW zina injini ndogo so hufanya gari kuwa jepesi hata kukata kona huwa rahisi zaidi kama upo kwenye gari ya mashindano vile pia kuna manual transmission kwa Mercedes ni tofauti.

vii.) Gharama za awali
- Kampuni zote zipo juu ni kati ya $35,000 na $160,000 lakini Mercedes wapo juu kidogo.

viii.) Gharama za uendeshaji
- Vitu vizuri vina gharama hili halikwepeki kama haupo vizuri wala usijihangaishe wewe kachukue tu IST yako uwe na amani ,BMW insurance premium ni ghali kuliko Mercedes kwa sababu vifaa vyake ni ghali na husumbua kuvipata kwa zote mbili service yake inabidi umpate mtu mwenye ujuzi na haya magari sio kila fundi anajua ukimpa bora fundi atakuingizia hasara zaidi.Kwa nyongeza BMW hushuka thamani yake haraka zaidi ya Mercedes so ukikaa nayo mda mrefu itakugharimu zaidi.

ix.) Soko lake
- BMW inapendwa zaidi na vijana professional kutokana na stylish yake na high performance ila Mercedes wazee professional ndiyo wateja wakubwa ila walivyotoa toleo la A - Class vijana nao wamelikubali.

Kampuni zote ni nzuri haijalishi ni BMW au Mercedes inategemeana na muhusika mwenyewe anapenda kampuni ipi na model/toleo gani hata Pepsi haifanani ladha na CocaCola
FB_IMG_1644400383830.jpg
FB_IMG_1644400454874.jpg
FB_IMG_1644400489417.jpg
FB_IMG_1644400473664.jpg
 
Dell computer Vs Hewlett Packard(HP) computer

- Dell ziko vizuri ni better kuliko HP hawa jamaa wanaofa premium lines kwa upande wa CPU,RAM na video cards na wako na ujuzi mwingi kwenye hii sekta japokuwa HP nao wanazo nzur ila Dell yupo vizuri sana ukizungumzia swala zima la ubora.

  • Dell gharama zao zipo chini kwa iwe kwa matumizi binafsi,makampuni na biashara basi nenda na hii kampuni na pia hata zile pc za chini(low end series pc) unakuta zipo vizuri ukilinganisha na HP ,Dell's alienware pc kwa upande wa performance kwenye upande wa uwezo wa kucheza game zipo vizuri na raia wamezipokea kwa mikono miwili.
  • HP yupo vizuri kwenye swala la betri zake zinadumu muda mrefu.

- Kwenye swala zima la innovation Dell wapo vizuri japokuwa HP nao so wachovu kivile siku hizi wanajitajidi kwenye pc HP amewekeza sana kwenye scanners na printers ila Dell yeye amewekeza zaidi kwenye pc/computer.

- Asilimia 95 ya dell hutengeneza kwenye nchi za Asia ,HP nyingi hutengenezwa United States kama pc zote maarufu kama vile HP Envy, Elitebook, Pavilion na HP Omen zatengenezwa US lakini baadhi ya vifaa hutengenezwa China, Thailand, Malaysia na Philippines ila uundwaji mzima wa pc unafanyikia US na wanafanya hivi ili waendane na soko.
FB_IMG_1644347356790.jpg
FB_IMG_1644347397297.jpg
FB_IMG_1644347542697.jpg
FB_IMG_1644347796378.jpg
FB_IMG_1644347823185.jpg
FB_IMG_1644348055784.jpg
 
ZIP Code Vs Postal Code

*Hivi ni vitu viwili ambavyo vinafanana sana vyote vikiwa na lengo moja kumrahisishia mtu kujua eneo husika pale anapotaka kwenda au kutuma mzigo *

- ZIP Code kwa kirefu chake ni Zonal Improvement Plan ni mfumo wa namba ambao husaidia kutambua eneo husika na kurahisisha mzigo au mtu kufika eneo hilo husika bila ya kupotea na kwa urahisi zaidi , Postal Code huu ni muunganiko wa namba ambao huunda namba maalum ya utambuzi wa maeneo hutumika kutrack maeneo kwa ajili ya kusambaza barua au nyaraka na mizigo mbalimbali kwa urahisi.

- ZIP Code ilianzishwa na inatumika huko Ufilipino na USA Postal Code hii ilianzishwa na inatumika huko United Kingdom na nchi nyingine isipokuwa USA na Ufilipino.

- ZIP Code ilianzishwa mwaka 1963 wakat Postal Code ilianzishwa mwaka 1959.

- ZIP Code hii inaundwa kwa namba wakat Postal Code inaundwa kwa namba au muunganiko wa namba na herufi.

- ZIP Code hutumika katika kutambua na kutanabaisha yale meneo ndani ya nchi , Postal Code hii hutumia kutanabaisha yale meneo yaliyopo ndani ya miji kwa ajili ya usambazaji wa nyaraka.

- ZIP Code tarakimu zake huwa 5 hadi 9 , Postal Code zinaweza zikawa fupi au ndefu.

- ZIP Code husaidia kupata reference na utambuzi wa eneo , Postal Code husaidia kupata reference,utambuzi wa eneo,sensa na kwenye kupanga ruti.

Huku kwetu Bongoland ndiyo naona tunaanzaanza haya mambo.
IMG-20220208-WA0003.jpg
images (4).jpg
FB_IMG_1644486761307.jpg
 
Aerial TV (antena) [emoji687]VS Satellite Dish (Dishi au ungo) [emoji341]
- Antenna kwenye manunuzi gharama yake ipo chini kwenye kuifunga haina gharama ,Dish hii kwenye manunuzi gharama yake ipo juu na pia kwenye kuifunga itakubidi umlipe yule atayekufungia.

- Antenna haihitaji ufundi mwingi sana kwenye kuifunga hata mtu wa kawaida anaweza ifunga ,Dish hii inahitaji mtu mwenye ujuzi sio kila mtu anaweza kufunga.

- Antenna hupokea matangazo yake ya TV kutokea ardhini ambako TV husika huweka transmitters ambazo husambaza mawimbi yake na ndiyo maana inabid antenna iwe ndefu na huwekwa juu ya paa kuepuka vizuizi vyovyote kama vile miti ili kupata signal kwa urahisi ,Dish yenyewe hupokea matangazo yake kutokea angani kwenye space kwa maana hiyo dish linaweza kufungwa hata chini kusiwe tu na kuzuizi kitakachozuia mawimbi ya satellite [emoji2930].

- Antenna ukitaka kuunga tv zaidi ya moja kwa antenna signal zinaweza kugawanywa kwa kufunga kifaa maalum cha kugawa hizo signal kutoka kwenye central point bila kusahau na amplifier kuzuia upotevu wa cable wa zile zinazotawanya mawimbi/signal kwenda kwenye TV nyingine vile vile gaharama yake ni nafuu ,Dish huku gharama ipo juu kwa sababu inabidi ununue kifaa maalum kulingana na wewe unataka uunge tv ngapi na pia inabidi uunge kwenye dish moja kwa moja kwenye LNB mfano kwa tv 4 unahitaji quad LNB, kama unataka kuunga tv 8 basi unatoa quad LNB unaweka Octo LNB ambayo unaunga cable 8 na ukitaka zaidi ya tv 8 basi utaweka Quattro LNB ikiwa na cable 4 pamoja na multi - switch amplifier.

- Antenna huwa haziathiriwi sana na hali ya hewa hata mvua ikinyesha unadunda tu kula burudani ,Dish huathiriwa na hali ya hewa hasa mvua kubwa mvua ndogo ndogo haziathiri na ikiwa inasumbua basi kuna vitu viwili Dishi halijawekwa vizur au zile coaxial cables haziko vizuri na haziwezi kuhimili hali ya hewa (not weatherproofed properly).

- Antenna hasara yake kuna kampuni nyingine ya ving'amuzi havina antenna ,Dish kwa sasa asilimia kubwa ya kampuni za ving'amuzi zina dishi.

- Antenna kama king'amuzi kimeongeza channels mpya itabidi ufanye manual scan mwenyewe ili ziweze kuingia lakin kwa dishi huwa zinajiapdate zenyewe.

- Antenna coverage yake ni ndogo inategemeana na eneo unaloishi ukiwa mbali na minara inayorusha mawimbi basi utapata picha nzuri au ukapata picha isiyoonesha vizuri au ukiwa bondeni ambako mawimbi hayafiki vizuri hautoona pia ,Dish ina coverage kubwa kama upo eneo ambalo antenna inasumbua basi weka dish utapata kile unachohitaji haijalishi ni wapi hata kama ni vijijini kule ndani ndani kabisa utapata picha nzuri kama yule aliyepo mjini.

- Antenna hata ukiwa unahama ni rahisi kusafiri nayo ila dish inakuwa mtihani kidogo pia ukitaka kuhamisha TV yako kutoka chumba kimoja kwenda kingine ni rahisi tofaut na Dishi kama waya haufiki basi itakugharimu inabidi uingie mfukoni.
FB_IMG_1644560741151.jpg
FB_IMG_1644560792517.jpg
 
Mfano mzuri Kanye West kabla hajawa na mahela alikuwa anatupia vitu vya thaman sana yaan show off za kutosha kwa sababu gani mtu yoyote ambaye hana hela atanunua vitu vya thaman ili kuwaonesha watu kuwa ana hela lakini mwenye hela tayari watu wanajua anazo so hana show off halafu kwake ni vitu vya kawaida tu anaona
 
Mfano mzuri Kanye West kabla hajawa na mahela alikuwa anatupia vitu vya thaman sana yaan show off za kutosha kwa sababu gani mtu yoyote ambaye hana hela atanunua vitu vya thaman ili kuwaonesha watu kuwa ana hela lakini mwenye hela tayari watu wanajua anazo so hana show off halafu kwake ni vitu vya kawaida tu anaona
kanye mdogo sana

sema billgate
 
Debit card [emoji388] Vs Credit card [emoji388]
- Debit card hii hupunguza au hutumia zile ambazo ziko kwa akaunti yako , Credit card hii inakuruhusu kuazima hela na ukafanyia manunuzi na huduma nyingine.

- Debit card chanzo cha hela ni zile zilizoko kwa akaunti yako , Credit card ina wigo mpana chanzo cha hela ni zile ulizonazo kwa akaunti yako na pia unaweza pata hela kwa kuchukua mkopo wa muda mfupi.

- Debit card kwenye matumizi hii inamipaka kwa sababu huwez tumia zaid ya kile ulichonacho kwenye akaunti yako ,Credit card ni kinyume chake unaweza tumia zaid ya hela zilizopo kwa akaunti yako

- Debit card wewe mwenyewe ndiye unalipa unapofanya manunuzi , Credit card wewe unalipa kwenye kampuni ya credit card husika halafu hiyo kampuni ya card yako wanalipa kwa yule uliyefanya manunuzi kwake.

- Debit card hakuna taarifa ya bili au miamala uliyofanya ila kwa credit card kila mwezi unapatiwa bill na miamala uliyofanya.

- Debit card hamna malipo unayofanya kwa vile unatumia hela zako , Credit card huku lazima ulipe bill kila mwezi kwa sababu ya zile hela ulizoazima kwa kampuni husika ya kadi yako.

- Debit card ina makato machache ya kila mwaka na PIN , Credit card yenyewe ina makato mengi kama vile ada ya usajili,ada ya kila mwezi,ada ya kuchelewa kulipa deni na ada ya cheki mbalimbali.

- Debit card hakuna riba , Credit card ina riba tena huwa juu hasa pale unapochelewa kulipa deni lao.

- Debit card haina ukomo wa matumizi ya hela inategemeana na kile kiasi ulichoweka kwa akaunti yako , Credit card yenyewe unaruhusiwa kutumia kile kiwango kilichosetiwa tu kwenye akaunti yako kulingana na makubaliano uliyofanya awali wakat unajiunga na ukitaka kutumia zaidi inabidi ukope kwa kampuni husika ya kadi yako.

- Debit card zawad ni chache kulinganisha na credit card.

- Debit card haina privileges nyingi , Credit card ina privileges nyingi kulingana na aina ya kadi uliyonayo kama vile dining, burudani ,travel na nyinginezo.

- Debit card ina ulinzi mdogo kwenye upotevu au kuibiwa,wizi , Credit card ni kinyume chake.

- Debit card huku unatoa hela popote kwa ATM japokuwa kuna makato

- Debit card approval ni rahisi na haraka zaidi tofauti na credit card.
FB_IMG_1645515345546.jpg
FB_IMG_1645515169359.jpg
 
Expiry Date Vs Best Before Date

- Expire date hii huonesha siku ya mwisho kutumika kwa bidhaa husika yaan usalama wa kiafya wa hiyo bidhaa kwa binadamu.

- Best Before Date hii huonesha siku ya mwisho ya ubora wa bidhaa husika mfano kama ni chakula basi baada ya hiyo siku au tarehe itaanza kupoteza ile ladha yake au harufu kama ilikuwa laini basi itakakamaa.
download (1).jpg
download.jpg
 
ZIP Code Vs Postal Code

*Hivi ni vitu viwili ambavyo vinafanana sana vyote vikiwa na lengo moja kumrahisishia mtu kujua eneo husika pale anapotaka kwenda au kutuma mzigo *

- ZIP Code kwa kirefu chake ni Zonal Improvement Plan ni mfumo wa namba ambao husaidia kutambua eneo husika na kurahisisha mzigo au mtu kufika eneo hilo husika bila ya kupotea na kwa urahisi zaidi , Postal Code huu ni muunganiko wa namba ambao huunda namba maalum ya utambuzi wa maeneo hutumika kutrack maeneo kwa ajili ya kusambaza barua au nyaraka na mizigo mbalimbali kwa urahisi.

- ZIP Code ilianzishwa na inatumika huko Ufilipino na USA Postal Code hii ilianzishwa na inatumika huko United Kingdom na nchi nyingine isipokuwa USA na Ufilipino.

- ZIP Code ilianzishwa mwaka 1963 wakat Postal Code ilianzishwa mwaka 1959.

- ZIP Code hii inaundwa kwa namba wakat Postal Code inaundwa kwa namba au muunganiko wa namba na herufi.

- ZIP Code hutumika katika kutambua na kutanabaisha yale meneo ndani ya nchi , Postal Code hii hutumia kutanabaisha yale meneo yaliyopo ndani ya miji kwa ajili ya usambazaji wa nyaraka.

- ZIP Code tarakimu zake huwa 5 hadi 9 , Postal Code zinaweza zikawa fupi au ndefu.

- ZIP Code husaidia kupata reference na utambuzi wa eneo , Postal Code husaidia kupata reference,utambuzi wa eneo,sensa na kwenye kupanga ruti.

Huku kwetu Bongoland ndiyo naona tunaanzaanza haya mambo.View attachment 2114759View attachment 2114760View attachment 2114761
Nzr
 
Tablet (iPad) Vs Smartphone (iPhone)

- Tablet zina saizi kubwa ya kioo kuanzia nchi 7 hadi 10 na kuna baadhi ya matoleo huzidi tofaut na smartphone yenyewe kioo chake ni kidogo.

- Tablet kuna baadhi ya apps ambazo hufanya kazi kwenye tablet tu japokuwa zote zinatumia OS moja na hii ni kutokana na saizi yake kubwa sio kama kwenye smartphone haziwezi kufanya kazi hapana saizi yake ndiyo kikwazo.

- Tablet inabid ununue Bluetooth headset utaonekana wa ajabu sana ukaweka sikion Tablet yenye kioo cha nnchi 10.

- Smartphone zenyewe ni portable kwa mfuko tu unaiweka unasepa zako tofaut na tablet ambao ni mzigo na mara nyingi hutumiwa pale mtu ametulia.

- Smartphone ina wigo mpana zaid wa matumizi kifupi inaweza kureplace tablet lakin tablet haiwez kureplace smartphone mfano tu kuna tablet nyingine huwezi tuma sms au kupiga simu japokuwa siku hizi wanaweka sehemu ambayo unachomeka sim card.

- Smartphone zote zina wifi na 3G lakini kwa tablet sio zote zenye zote ni baadhi yenye nazo zote japokuwa siku hizi wanatengeneza zenye zote kwa sababu wameona watu wanaoenda.

- Tablet ni komputa ndogo isiyo na keyboard [emoji3491] kwa maana nyingine kaz nyingi za pc zinafanywa kwenye tablet kwa raha zote japokuwa kuna tablet nyingine unaweza unga keyboard ya nje na mausi pia tofaut na smartphone ambayo pia waweza fanya ila screen yake itakunyima uhuru.

- Tablet ilianzishwa 1994 na IBM wakat smartphone zipo tokea 1989.
FB_IMG_1646314293772.jpg
FB_IMG_1646314219348.jpg
 
Back
Top Bottom