1. Iniesta
kama mpira ungekuwa ni mapenzi huyu jamaa angekuwa Romeo .,ukimtazama utadhani mchezo mrahisi kuliko neno lenyewe , Pengine mie nitaoneka namsifu sana angali sijawahi hata mtia,Machoni muulize hata yule dogo Fundi wa Dunia mwenye Tuzo za Ballon d or nyingi kuliko mchezaji yoyote duniani aliezaliwa kule Rosario Argentina, atakujibu.
2. Xavi , anakupa hapa pasi alafu anaomba pale, alafu anakupa tena pale, yupo kama anautaka mpira halafu kama hautaki ..1 & 2 lazima upoteane ukiwa middle ya timu pinzani .,Masimulizi haya watakusimulia kina Alonso.,Raul., Ramos., Modric., na wengine waliobahatika kuwa wapinzani wake
Akiwemo timu itapiga pasi million 5.6 hiyo ni first half tu.
3. Pirlo , Italia pale kuna mamido ambao washazoea kula sakramenti katika viunga vya Watakatifu wa Rome,Papa na wenzie.
Mamido wa namna hii , Ni nadra sana Kumkuta na Dhambi....Hivi unaelewa unapoambiwa hana 'DHAMBI' basi majibu mengi wanayo Waitaly na Wale mabibi kizee wa Turin, anapiga Pasi kwa kuamisha uwanja toka kanaan mpaka Syria na Misri dhambi anazitoa wapi ,
Wakati akimaliza kuwanyanyasa mabeki na mamidfilder wachovu , huungama dhambi zake.
Waitalia wengine watakatifu ni Jorginho na Marco Verrati