Reginald12
JF-Expert Member
- Aug 9, 2012
- 264
- 145
Ninashukuru kwa jibu lako lakini bado mimi sioni tatizo la lugha. Hizo unazozitaja ni redio ambazo ni za kitaifa. Lakini akaja mjasiriamali mdogo ambaye anataka kutangaza kizaramo sioni shida ikiwa lengo lake ni kunufaisha wanaotumia lugha ile na pia kuienzi. Wajerumani na wajapani wanatumia lugha moja nchi nzima.
Lugha zile ambazo labda wamekosa uwezo wa kumiliki redio au mtu wa kurusha ujumbe lugha zao, bila shaka zitakufa na ndio kawaida ya lugha ambayo haijahifadhiwa kwa maandishi au matumizi. Tanzania ikiendelea na kuenzi kiswahili bila shaka siku za usoni lugha nyingi zitapotea. Hiyo ni kawaida kabisa.
Ukiingia tovuti ya BBC utakuta kurasa nyingi sana na hata za lugha/lafudhi tofauti hata za uingereza. Kuna Welsh- Newyddion - Hafan na pia Scottish - Naidheachdan - Dachaigh. Lugha hizo za waingereza siyo za kimataifa lakini zinatumika. Ni mawazo ya mtu, vitendo vyake na dhamira zake ambazo zinaweza kueneza chuki hizo. Hamna shida kabisa kuwasiliana lugha hata zile ndogo kabila ikiwa ujumbe wako ni wa amani. Mbona nyimbo za lugha tofauti tunafurahia? Labda Saida Karoli tungempiga stop ili tuimbe Kiswahili tu? TATIZO NI WATU wala siyo LUGHA.