Xi Jinping Mtu wa watu, kwa ajili ya watu

Xi Jinping Mtu wa watu, kwa ajili ya watu

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111426949182.jpg

Rais wa China Xi Jinping amepitishwa rasmi kuiongoza nchi hiyo kubwa inayoendelea kwa awamu ya tatu mfululizo. Tangu alipoingia madarakani mwezi Machi mwaka 2013, Xi Jinping amesisitiza mara kwa mara kutanguliza wananchi mbele katika kila eneo.

Katika hotuba yake aliyoitoa ijumaa baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa China, rais Xi alisema kuwa uaminifu walio nao Wachina kwake ni chachu kubwa inayomwezesha kusonga mbele, na pia ni jukumu kubwa sana analobeba mabegani mwake. Pia kupitia hotuba hiyo, rais Xi ameahidi kuwa, kuanzia sasa mpaka katikati ya karne ya 21, kazi kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Wachina itakuwa ni kujenga China kuwa nchi kubwa ya ujamaa ya kisasa kwa pande zote, na kuendeleza ufufukaji wa taifa la China katika maeneo yote.

Pia rais Xi ameahidi kuwa, atatimiza majukumu aliyopewa kuendana na katiba, huku jukumu lake kubwa likiwa ni kutekeleza mahitaji ya taifa, na maslahi ya wananchi yakiwa ni kipimo chake.

Katika miaka 10 ambayo rais Xi amekuwa madarakani, China imeshuhudia maendeleo makubwa tena ya kasi katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na afya, sayansi na teknolojia, anga za juu, uchumi na biashara, kilimo na sekta nyingine.

Katika kipindi chote alichokuwa madarakani, rais Xi amedumisha dhamira yake ya kuwatanguliza kwanza wananchi, na hili limedhihirika baada ya China kupiga hatua kubwa ya kuondokana na umasikini uliokithiri, miaka 10 kabla ya muda uliopangwa katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030.

Chini ya uongozi wa rais Xi, sekta ya kilimo nchini China nayo imepiga hatua kubwa, kwani uwekezaji katika sayansi na teknolojia ya kilimo umepewa umuhimu mkubwa katika kazi za serikali.

Daima rais Xi amekuwa akisisitiza maendeleo ya vijijini, kama msingi wa maendeleo ya taifa, na katika kutimiza hilo, Waraka N0.1 wa serikali unaeleza kazi zinazohitajika ili kuzidisha mbinu za kuwasaidia wakulima kuongeza mapato yao na kukuza uwezo wao wa kupata utajiri. Kupitia hilo, itakuwa ni rahisi kukuza kithabiti ujenzi wa vijiji vizuri na vyenye maafikiano, ambavyo vinavutia watu kuishi na kufanya kazi, kuboresha mfumo wa usimamizi wa vijijini unaoongozwa na mashirika ya Chama, na kuimarisha uhakikisho wa kisera, na uvumbuzi wa mfumo.

Rais Xi pia amekuwa akisisitiza suala la uvumbuzi katika sayansi na teknolojia kama moja ya chachu ya maendeleo ya taifa la China. Katika Mikutani Miwili iliyomalizika hivi karibuni, suala la sayansi na teknolojia limepewa umuhimu mkubwa, na kutoa ujumbe kuwa, sekta hiyo inachochea juhudi za China za kutimiza maendeleo ya kujitosheleza na yenye ubora wa juu.

Jambo lingine ambalo rais Xi amelifanya katika kipindi chote alichokuwa madarakani (na tunaamini ataendelea kulifanya), ni kutekeleza kihalisi pendekezo la “Kujenga Jamii ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.”

Mwaka 2013, ikiwa muda mfupi baada ya kuingia madarakani, rais Xi alitoa pendekezo hilo, ambalo lengo lake kuu ni kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja ambayo haina umaskini na kuwa na maendeleo ya pamoja.

Hili limejihidhirisha katika ushirikiano na uhusiano kati ya China na nchi nyingine zinazoendelea, zikiwemo za Afrika, katika nyanja mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu, sekta ya afya, elimu, uchumi na biashara na sekta nyingine. Rais Xi ametoa umuhimu mkubwa kwa nchi za Afrika, na miradi mingi mikubwa ya maendeleo imetekelezwa ama inatekelezwa na kampuni za China. Mifano michache ni pamoja na reli ya SGR inayounganisha miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya, reli ya SGR inayounganisha Ethiopia na Djibout, na bandari ya Lamu. Miradi hii yote imekuwa chachu ya maendeleo kutokana na kutoa nafsi za ajira kwa wazawa, kukuza biashara katika maeneo ambayo reli hizo zinapita, na pia kupunguza mzigo mkubwa uliokuwa unaielemea bandari ya Mombasa.

Hivyo, ni wazi kwamba, rais wa China, Xi Jinping, ana nia thabiti ya kujenga nchi ya kijamaa ya kisasa, na kuboresha maisha ya wananchi kwa pande zote, na kuleta ustawi endelevu kwa nchi hii kubwa inayoendelea, pamoja na kutoa mchango mkubwa kwa uchumi na maendeleo ya dunia kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom