Katafute refurb ya samsung note 10, s10, iphone 8 n.k hizi simu ni balaa na nusu.
Mkuu serious unamwambia anunue iPhone 8, kasimu kadogo vile, kana home button, display yake ni LCD, tena hakakai na chaji, kamera yake inazidiwa na midrange nyingi za sasa, sio full screen, halafu kama sikosei ni iOS 11 na sasahivi wenzake wapo iOS 16. Kumbuka iPhone 8 ukiupgrade kutoka ilipo hadi iOS 16 inakuwa slow, display inaanza kuwa less responsive, kamera inaanza kuzingua, battery ndio inazidi kupungua zaidi uwezo wake wa kutunza haji, hiyo simu ya 2017 haifai kabisa kwa matumizi ya 2023.
Halafu unamwambia anunue refurbished phones, unaijua risk yake wewe? Jamaa anataka simu inayokaa na chaji unamwambia anunue refurb za Samsung note 10 na S10, hizo simu kwa standard ya 2023 hazikai na chaji, tena ukijumlisha imekuwa refurbished, itabidi awe anatembea na powerbank. Akifuata huu ushauri atajuta aisee.
Bora anunue simu mpya tu kwenye boksi lake yaani simu ambayo haina mbambamba.
Simu bora zaidi kwa bei hiyo kwa hapa Bongo ni
* Xiaomi Redmi Note 10S
Lakini kwa kuwa mkuu unaichukia Xiaomi, basi ungemshauri hata anunue
* Samsung Galaxy A32 mpya kabisa kwenye boksi lake
Ingawa Redmi Note 10S ndio bora zaidi, kwanza inaweza kurekodi 4K videos wakati A32 inaishia 1080p, Redmi Note 10S inatumia chipset ya MediaTek Helio G95 wakati Galaxy A32 inatumia MediaTek Helio G80 ambayo ni dhaifu kulio ya G95. Redmi Note 10S inatumia Bluetooth version 5.1 wakati A32 inatumia version 5.0. Redmi Note 10S display yake inafika hadi 1100nits hiyo Galaxy A32 inaishia 814nits, Redmi Note 10S inatumia 33W fast charger wakati Galaxy A32 inatumia 15W na bado Redmi ni cheap ukicompare na Samsung
Zote zina Android 11, 5000mAh battery, AMOLED display, 64MP rear cameras na mambo mengine huko, siwezi yataja yote
Hapo anunue simu mpya ili aenjoy recent Android version, kioo kikubwa, muonekano wa kisasa, usalama wa 100% na aepuke kuwa outdated. Usitake kumrudisha nyuma mkuu. Simu hapo ni
- Xiaomi Redmi Note 10S
- Samsung Galaxy A32
Tena anunue Redmi kama anataka simu bora zaidi tena kwa bei iliyotulia au anunue Samsung kama tu anaangali brand ila asinunue hizo refurbished ulizomtajia[emoji41][emoji41]