Xiaomi vs Oppo nichukue ipi?

Namba 4 hapo
 
Sijajua, mimi sio fan wa caller wala messaging app so sijawahi kufikiria kutumia caller nyingine
Kama unataka MIUI dialler na message app nunua Xiaomi Chinese version
Mkuu hizi chinese versions zinashika network vixuri huku kwetu?
 
Mkuu hizi chinese versions zinashika network vixuri huku kwetu?
Ndio, zinashika network vizuri
Cha msingi kabla hujanunua simu yako Angalia specifications ili ujue hiyo Chinese version ina support band gani za network halafu angalia ni mtandao gani unakubali hizo bands za internet hapa Tanzania
Ningejua bands za Bongo ningekutajia ili uwe unaangalia kama simu hiyo ina support hizo bands
Ila ukimuuliza Chief-Mkwawa anajua bands za network hapa Tz [emoji846]
 
Band 3 (1800), band 7 (2600), band 20 (800) band 40 (2300)

Band 3 - voda, Airtel, Tigo mjini, TTCL
Band 7 - Halotel
Band 20 - Smile na Tigo maeneo yote
Bamd 40 - zamani smart ama sasa TTCL mjini

Kwa 5G to be safe iwepo band 3500mhz (n78)


Hizi ni Band za 5G ambazo TCRA waliuza
 
Nimeona Xiaomi 13 Ultra Chinese version haikubali band 20, hivi kuna uwezekano wa ku unlock network na ikakubali ku support hiyo band?
Au kama simu haina hiyo band ndio basi

Nimesikia watu wana unlock simu zisizo support bands za Bongo. Sasa sijaielewa ni nini haswa wanacho unlock, ni network band au kuna kitu kingine ndio wana unlock?
 
Kuna namna mbili za kulock band, kwa software ama hardware, kama Hardware yaani modem haisuport band husika huna ujanja hakuna fundi atakaekusaidia, ila kama wame lock tu kwa software, ndio inawezekana ku unlock bands, inatofautiana baina ya model na mode.
 
Natumia Xiaomi 13 pro Chinese version. Nina laini ya voda na tigo za 4g na ninapata 4g kama kawaida.
 
hapa nimepata somo zuri
 
User reviews mnazisoma wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…