Ya Argentina yanatimia kwa TISS?

Ya Argentina yanatimia kwa TISS?

Ni Vema tukaanza upya vyote.
Kufutilia mbali mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Kufutilia mbali NGOs zote.
Kufutilia mbali mitandao ya kijamii.
Kufutilia mbali misaada/hisani na mikopo kutoka nje.
Kuunda upya TISS.
 
Yerico achana na usiyoyajua,fanya kile kinachokupelekea mkono wako uingie kinywani huna ushahidi na hata moja uliloliandika hapa zaid ya kusoma kwenye vitàbu,na mitandao mosi ,pili angaika na kesi iliyopo mahakamani kwanza hata wananchi tumekuchoka kwa huu utumbo wako unaondika ukiwa umeshiba makande.
 
Wananchi gani waliomchoka?!

Usipende kusemea watu wengine
 
Tarehe 18 Januari 2015 Idara ya usalama ya Agentina ilituhumiwa kuhusika na mauaji ya mpelelezi binafsi bwana Alberto Nisman aliyekuwa akitaka kuanika madudu ya serikali hiyo ikiwemo ufisadi uliopelekea kulinda ugaidi wa Iran uliofanyika Agentina. Wairani walikuwa wamewahonga usalama wa taifa wa Agentina kwa vipande vya fedha ili wasiumbue Iran katika ugaidi huo uliotekelezwa katika kituo cha Kiyahudi kitwacho AMIA Jewish Community Centre" kilichomo mjini Buenos Aires Agentina.

Alberto Nisman akafanya uchunguzi, akagundua ukweli huo bila kuacha chenga ambapo sehemu ya ripoti hiyo ilimuhusisha rais wa zamani Cristina Fernández de Kirchner na ugaidi huo 1994, na kukazia kuwa rais aliitumia idara hiyo kuendesha mauaji ya raia wapinzani na wanahabari nchini humo. Rais wa Agentina wa miaka ya 2015 bwana Mauricio Macri nae akataka kuifutilia mbali kurugenzi ya ya ndani ya usalama ya Agentina kufuatia kashfa hiyo ambayo ilikaribia kuhatarisha mamlaka yake ya urais na nchi kwa ujumla. Jamaa wa Usalama kuona hivyo, wakamuua mpelelezi siku moja kabla hajawasilisha ushahidi wake bungeni bungeni ili aanike ukweli.

Bunge la Agentina baada ya kuona hali hiyo, likamualika Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Agentina ili awaeleze utendaji wa taasisi hiyo. Ilikuwa afanye kazi hiyo Jumatatu. Naye leo ametekwa, hajulikani alipo. Sasa bunge likavunja Usalama wa taifa wa Agentina kwa sababu ya vitendo vya udhalimu na kuliunda upya kwa weledi kabisa...

Hali ya Agentina haina tofauti na ya Tanzania. Usalama wa Raia umekuwa jambo tete sana Kama ilivyokuwa Agentina ambayo maafisa usalama wanawekea vinasa sauti wanasiasa na kuwahujumu, kuwapiga na kuua wanaharakati, wanasiasa, na wanahabari. Uhuru wa kutoa maoni ulizimwa kabisa. Tanzania nayo iko hivyo (rejea mauaji ya kisiaaa, wanahabari na wanaharakati).

Fundisho kubwa kwa Tanzania ni wakati sasa wa kufanya marekebisho makubwa ya idara ya Usalama nchini na kuhakikisha uhai wa kila Mtanzania na kila mtu unalindwa na kuthaminiwa. Rais na Bunge la nchi yetu simameni mulimlike taifa kwa jicho la tatu.

Kwanini ripoti ya uchunguzi wa mauaji nchini ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Mh Adadi Rajabu mwezi uliopita ilinyofolewa sekundu chache kabla ya kuwasilishwa bungeni? Nani aliratibu unyofoaji wa ripoti hii? Ana maslahi gani na mauaji haya?

[HASHTAG]#KitabuUjasusiwaKidolanaKiuchumi[/HASHTAG]

Na Yericko Nyerere
View attachment 700365
Nasikia hii story imo kwenye kitabu cha ujasusi Wa kidola , bei Tsh 80,000
 
Hahaaa!!

Mbona huwa mnapenda kudanganyana? Wewe YERICKO unajua chochote kuhusu Tiss? Usiwaaminishe watu na kuwajaza ujinga, Nina wasiwasi na vitabu vyako unavyojitungia kuhusu mambo ya kiusalama.

Kwa hiyo na wewe unaamini kuwa mauaji yanayotokea nchini yanatekelezwa na Tiss? Kama ni hivyo unawezaje kuamini jambo usilothibitisha mwenyewe badala yake unatumia cumulative doubts kuihukumu Tiss?

Nimeshadharau na uko shallow sana mkuu,
Kingine nakuomba usitumie Jamiiforum kutafuta sifa kwa jina la idara nyeti hii ya taifa letu,
Je ukiitwa unaweza kulinda hoja zako?

Umeshawahi kuwaona wakuu wa idara hii wakikanusha hizi tuhuma mnazowapaka hadharani ama kwenye media?
Jiongeze, stop that tender of messing, otherwise the deed will retaliate your myths!!
 
Kwanza nikusihi kabla hujajibu hoja yoyote katika andiko langu yakupasa kwanza usome vizuri na kuelewa, ikiwa hujaelewa pita tu kuwa msomaji na mtazamaji tu....

Maandishi yangu hayasemi TISS vile unavyofikiri, jipe muda wa kusoma kwakutulia na kuacha mihemko ya kisiasa...
 
USALAMA WA TAIFA WAMEWAVULIA NGUO CCM .........KINACHOENDELEA KILA MTU ANAJUA.
 
Kwanza nikusihi kabla hujajibu hoja yoyote katika andiko langu yakupasa kwanza usome vizuri na kuelewa, ikiwa hujaelewa pita tu kuwa msomaji na mtazamaji tu....

Maandishi yangu hayasemi TISS vile unavyofikiri, jipe muda wa kusoma kwakutulia na kuacha mihemko ya kisiasa...
Acha kukwepa hoja kijana.
 
Sasa kama katika Jina tu anakosea hivi je tutamuamini vipi katika hayo mambo Nyeti na Muhimu ya ' Kiusalama ' anayojitutumua kutwa kuyajadili humu? Mtu aliyeiva kweli Kiintelijensia / Kijasusi huwa hafanyi makosa katika kila Kitu chake na huongozwa sana na umakini usio na hata chembe yoyote ile ya shaka.
Ujuaji mwingi unamtesa Mkuu acha aendelee kuchamba kwingi mwishowe tutauona
 
Huu Uzi ni uchuro.

Bora nirudi zangu Wellington kula lunch.
 
Back
Top Bottom