Aah jamani mpira acheni tu jamani, wakati niko mdogo nilikuwa nawahi kiwanjani saa nane kusubiri wenzangu waje tucheze, km nipo shule lzm ikifika saa tisa na nusu vipindi vikiisha ni uwanjani mpaka saa kumi na mbili ndo nakumbuka kuna nyumbani. ikitokea kuna kipindi mwl wake hayupo, tunatokea dirishani breki ya kwanza uwanjani hiyo ni primary. secondary timu ya shule kila saa saba uwanjani mpaka saa tisa, nikitoka hapo home, ikifika kumi na moja chama langu la mtaani enzi hizo ligi daraja la tatu, mwenyewe mido nnatisha. kwa kweli wake zetu mtuwie radhi ile motto ya coca cola ya eat futbol drink futbol msidhani masikhara, watu tunapenda mpira wacha, msosi weka kando huko. mama watoto wangu hawezi angalia tv peke yake km nipo home, sasa ikifika siku kuna mechi nakimbilia room kuangalia mechi kwenye ka tv kangu ka jicho moja nawaachia wao waangalie tamthilia zao, hawezi kaa peke yake lzm anifuate room, maskini atasinzia hapo mwenzie nafaudu soccer yeye ataulizia bd tu haujaisha. kuna kipindi flani kwenye tv kilikuwa kinaitwa futball mundial, wana msemo wao soccer the game we love kweli i love football