Ya Mohamed Mwameja na ubora wa Shule za Kayumba katika kuwaandaa watoto na maisha halisi

Ulianza vizuri lakini ulipofika Kayumba umebugi sana. Kayumba hazina vitabu, ukimpeleka mwanao kwa mantiki yako usitegemee atatoboa ng'oo hawezi. Ugumu unaozungumzwa na Mwameja na yule Mjapan ni mazoezi yenyewe. Vifaa vya kufanyia hayo mazoezi vipo. Huko Kayumba hakuna vitabu, walimu hawawajibiki ipasavyo hao ndiyo yanayolalamikiwa.
 
Vitabu unamnunulia mwenyewe anakuwa anajisomea akiwa nyumbani
 
Muda mwingi mtoto anautumia akiwa shuleni usilisahau lakini. Hata hivyo hoja yako ni mashiko..mzazi lazima uwe ndio mwalimu wa kwanza kwa watoto wako.
Ni sahihi mkuu kwamba mtoto muda mwingi anautumia akiwa shuleni,lakini je anautumia akiwa pamoja na nani huko shuleni ?

Muda mwingi mwaafunzi anautumia akiwa shuleni lakini muda mwingi huo anakuwa pamoja na wanafunzi wenzake mara nyingi.

Muda ambao mwanafunzi atakuwa shuleni anaonana na mwaimu ni muda wa vipindi tu.

Imagine mwalimu anaingia kwenye kipindi kinachotumia saa moja na nusu darasani,darasa lina wanafunzi 50.

Je mwalimu huyu atapata wapi muda wa kumcare mtoto mmoja mmoja kwa lmasaa mawili mpaka watimie watoto 50 wote ?

Utaona kwamba mwalimu hana mchango MKUBWA(LABDA 10%)KATIKA KJMKUZA MTOTO KITABIA NA KIMALEZI KWANI HUO MUDA WA KUKAA NA MWANAFUZNI HANA HUKO SHULENI.
 
Yaani maelezo yote hayo lengo kutetea shule St Kayumba.

Yaani maelezo yote hayo kumbe ni kuzipamba St Kayumba. Anyway, ngoja na mimi nianze kuwalaza njaa wanangu siku moja moja ili kuwaandaa ugumu wa maisha!
 
Yaani maelezo yote hayo lengo kutetea shule St Kayumba.



Yaani maelezo yote hayo kumbe ni kuzipamba St Kayumba. Anyway, ngoja na mimi nianze kuwalaza njaa wanangu siku moja moja ili kuwaandaa ugumu wa maisha!
Haya bana Baba Kelvin
 
Usihamishe majikumu ya wazazi ukawapa waalimu,hiyo haipo.

Wanafunzi 70 mwalimu mmoja hawezi kuhandle watoto wote.

Tuache shule iwe na jukumu la kutoa elimu,mzazi nyumbani ndio awe na jukumu la kuwashape watoto vipi wawe.
This means Mwalimu si mlezi! So, wonderful (wachaga wanasema 'ndafu') 🤣
 
Elimu ya Msingi na Awali Mwalimu wa madarasa ya chini (awali, la 1 & 2) Mwalimu Ofisi yake huwa ni humo humo darasani. Hawachanganyiki na Walimu wengine kukaa Ofisi moja labda ishu maalumu kama vile vikao. Umewahi chunguza hili? Ukipata jibu jiulize ni kwa nn.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…