- Thread starter
- #21
Nikitazama vizuri hapa naona kama kuna mgogoro/kutoaminiana kati ya Chebukati na Raila, na hii inakuwa mbaya sana kwasababu inaenda kutengeneza matabaka baina ya wale watendaji wa IEBC, ni kama vile wale wajumbe walikuwa na wagombea wao hii kitu inaharibu sifa ya IEBC kutakiwa kuwa chombo huru.
Hii si ndiyo maana ya uhuru sasa? Kwamba kama mbwai na iwe mbwai? Kwa uhuru kabisa na kila mtu aeleze alikopeleka mboga.
Hatishiwi mtu hapa!
Umoja wa IEBC wa nini mkuu kama ule ukimya wa ZEC ya Jecha nao ulifuzu kuitwa umoja?
Tabia hizi za kamati za ulinzi na usalama kuja na matokeo yao ya kutangazwa na tume ni lazima zikomeshwe.
Yatokeayo Kenya na yatufungue macho haswa!