Jibu ni hili. Mdhamini mkuu (wa klabu) huwa anakuwa ni mmoja tu, na ndiye anayewekewa nembo kubwa kifuani. huyu kutokana na ukubwa wake, hata hela anayotoa ni ndefu. Baada ya kupata mdhamini mkuu, klabu inaweza ikawatafuta wadhamini wengine wadogo ambao nembo zao zinakaa pembezoni mwa jezi sawia na nembo ya mdhamini wa ligi (TFF, CAF, FIFA), sio kifuani. Hawa hata hela wanayotoa huwa sio kubwa kama ya mdhamini mkuu
Kwa kujibu swali lako, NBC, Mo Extra, Africarriers, MO29, ATCL, Vunjabei nk kama wanatakiwa kukaa katika jezi, basi ni pembezoni, maana mdhamini mkuu (M-Bet) nafasi yake ni kifuani. Kwa hiyo ndugu, tuondokane na mawazo ya kulalamikia wadhamini eti wanatoa hela ndogo, tena hasa kwa kuziandama bidhaa za MeTL, hawa wote wanaisaidia sana Simba lakini bado kwa heshima M-Bet anayetoa hela nyingi anakaa kifuani. Kuendelea kulinganisha M-Bet na Mo Extra au Vunjabei ni kuendekeza mawazo yaliyofinyika