Ya wahenga..

Ya wahenga..

briophyta plantae

Senior Member
Joined
Feb 18, 2017
Posts
117
Reaction score
132
MAMA NA BABA

MAMA: anakupenda mpaka ukimtazama machoni unauona upendo wake.
BABA: anakupenda bila kuonesha dalili yoyote machoni.

MAMA: amekutambulisha duniani.
BABA: ameitambulisha dunia kwako.

MAMA: amekuonesha thamani ya uhai.
BABA: amekuonesha thamani ya kuishi.

MAMA: anahakikisha haupati njaa.
BABA: anahakikisha unajifunza kutokana na njaa.

MAMA: anakulinda usianguke.
BABA: anakufunza kunyanyuka baada ya kuanguka.

MAMA: alikufunza kupiga hatua na kutembea utotoni.
BABA: anakufunza kupiga hatua za kimaisha.

MAMA: anahakikisha unajifunza kutokana na uzoefu aliopitia yeye.
BABA: anahakikisha unajifunza kutokana na uzoefu unaopitia wewe mwenyewe.

MAMA: anakufunza kwa tafakuri.
BABA: anakufunza kwa uhalisia.

MAMA: kupitia kwake unajifunza kujali.
BABA: kupitia kwake utajifunza kuwajibika.

Imeandikwa na Maundu Mwingizi (MwanaBalagha).
 
Back
Top Bottom