Yaani Uganda anayetuzidi Kiwango 'Kafa' 2 Kwake Kampala na Algeria, leo tulio Mahututi Kimpira ndiyo tumfunge Algeria?

Yaani Uganda anayetuzidi Kiwango 'Kafa' 2 Kwake Kampala na Algeria, leo tulio Mahututi Kimpira ndiyo tumfunge Algeria?

Vyovyote vile ila kikubwa Uganda Kafa.
Uganda alifungwa hizo goli 2 ugenini, na siyo Kampala! Hivyo unatakiwa kurekebisha andiko lako. Sawa?

Ila kwa upande mwingine, naungana na wewe! Kwa huu upangaji mbovu wa timu, kuna uwezekano wa kufungwa goli za kutosha tu mechi ya leo.
 
Naona kuna dalili ya sisi Watanzania kushinda leo
 
TUNGEPATA SARE NA ALGERIA, TUFANYE MISA YA SHUKRANI.
------------------------

Mechi tatu za michuano tofauti tulizokutana na Algeria hivi karibuni wametufunga jumla ya goal 12. Sisi tumewafunga goal 2 tu. Tukiwa kwenye harakati za kuitafuta tiketi ya kwenda Urusi kwenye fainal za kombe la dunia. Hatua ya pili tulikutana na Algeria.

Mechi ya kwanza kwa mkapa, tulianza kuwafunga goal 2 kisha wakachomoa zote, Full time ubao ukasoma 2-2

Mechi ya marudiano Algeria walienda kutufanyia mauaji ya kimbari. Ilikuwa ni simulizi inayonuka damu kwenye kila herufi iliyoshiriki kukiandika kitabu kile.

Moja ya safari za mateso ya Golgota alizozipitia 'Boniface Mkwasa' akiwa mkufunzi wa timu ya taifa, ni ile safari ya Blida Algeria. Walitupiga goal 7-0. Wakatutoa kwa Aggregate ya goal 9-2.

2019 tulipofanikiwa kwenda Afcon, Algeria tulikutana nao tena tukiwa kundi moja. Hakuna cha maana tulichofanya, zaidi ya kupunguza idadi ya magoal ya kufungwa, tulikufa goal 3-0.

Kwa mara nyingine tena, "ubora ukawa umeshinda dhidi ya maombi na sala."

Algeria wametuacha mbali sana kisoka. Ule ubora walionao hawakuupata kwa bahati mbaya au furukuu. Ni matokeo ya mipango, uwekezaji, na kuiishi sayansi ya mpira kwa vitendo. Vitu ambavyo sisi Tanzania tunavikwepa.

Jana kama tungeweza kushinda itakuwa ni maamuzi ya Mungu sio ubora wa Stars. Sisi tuna timu ya taifa ya kawaida kabisa. Binafsi naamini, hata tungepata sare tungetakiwa kufanya misa ya shukrani.
 
Back
Top Bottom