Yabainika Ufaransa ililipa mabilioni ili majasusi wake waliokamatwa nchini Burkina Faso waachiwe

Yabainika Ufaransa ililipa mabilioni ili majasusi wake waliokamatwa nchini Burkina Faso waachiwe

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Imebainika kuwa Ufaransa ililipa kiasi cha Euro Milioni 60 sawa na Shilingi Bilioni 156 za Tanzania ili majasusi wake wanne waliokuwa wamekamatwa na kushikiliwa nchini Burkina Faso waweze kuachiwa.
Majasusi hao walikamatwa nchini Burkina Faso mnamo Disemba mwaka 2023 na kuachiwa mnamo Disemba 2024 baada ya mazungumzo yaliyoratibiwa na mfalme wa Morocco.

Mara baada ya majasusi hao kukamatwa mnamo Disemba 2023, vyombo vya habari vya Ufaransa vilidai kuwa majasusi hao walikuwa "wataalamu wa IT" na kwamba serikali ya Burkina Faso haikuwa na uhalali wa kuwakamata. Vilevile Ufaransa iliilaumu Urusi na kudai kuwa majasusi wa Urusi ndio waliishawishi serikali ya Burkina Faso kuwakamata raia hao wa Ufaransa.

Baada ya kukamatwa kwao, mazungumzo yalianza kufanyika ili majasusi hao waweze kuachiwa. Seríkali ya Ufaransa iliiomba seríkali ya Togo kufanya mazungumzo kwa niaba yao lakini hata hivyo Togo haikufanikiwa kuishawishi Burkina Faso kuweza kuwaachia . Baadae seríkali ya Ufaransa ikaomba msaada kutoka falme za kiarabu ( UAE) ingawa pia UAE ilishindwa kuishawishi Burkina Faso kuwaachia majasusi hao.

Mnamo Januari 2024, seríkali ya Ufaransa ikafikiria kutuma wanajeshi wake kwenda Burkina Faso ili kuwachukua majasusi hao " kwa nguvu" lakini wazo hilo lilitupiliwa mbali kwa sababu za kisiasa .

Hapo ndipo Ufaransa ikaigeukia Morocco ambayo ilionekana kuwa na uhusiano mzuri na Burkina Faso. Morocco ilikubali lakini kwa sharti kuwa ni lazima Ufaransa iitambue Sahara Magharibi kama eneo la Morocco. Ufaransa ilikubali na kutangaza kuitambua Sahara Magharibi kama eneo la Morroco na hapo ndipo Morocco ikakubali kuishawishi Burkina Faso kuwaachia majasusi hao wa Ufaransa.
Hatimaye Disemba 2024 majasusi hao waliachiwa na kwenda nchini Ufaransa kwa kupitia nchini Morocco.
Mnamo Januari 16 2025, France 24 iliripoti kuwa taarifa kutoka Morocco zinadai Ufaransa ililipa Euro Milioni kadhaa ili majasusi hao waweze kuachiwa ingawa shirika la ujasusi la Ufaransa DGSE lilikana madai hayo. Baadae waandishi wa habari wa kujitegemea ndipo wakaripoti kuwa kiasi kilicholipwa ni Euro Milioni 60.

Wakati majasusi hao wakiachiwa, nchini Niger bado kuna jasusi mmoja wa Ufaransa anashikiliwa. Jasusi huyo alikamatwa mwaka 2024 mara baada tu ya kutua katika mojawapo ya viwanja vya ndege vya nchini Niger.


View: https://x.com/Nath_Yamb/status/1879543292750111099?t=RPi8x_QUd6h5FJMItNN1_A&s=19.


View: https://youtu.be/yFNpIpdbvRo?si=ZTaNHxApqs5Sn0PB
 
Asante kwa taarifa lakini hilo ni ngumu kutokea kwasababu serikali za Kiafrica ni corrupt sana.

Ingekua hivyo, wangetumia robo ya hiyo fedha kuhonga maafisa usalama ili watu wao watoroke au ingetumika nguvu.
 
Back
Top Bottom