Yadi ipi inayouza magari mazuri Tanzania na Zanzibar na inachukua muda gani ukilipa kuchukua gari?

Ile security iliyoko pale Jan sidhani kama wanaweza kufanya hivyo...
Hao wanaouziwa parts pengine wanadanganywa kuwa zinatoja Jan kumbe siyo..

Pale Jan ukitaka kuchukua gari na limekuja na hiyo changamoto wanakuambia kabisa..
Pale pana cctv camera kila kona,nimenunua gari pale zaidi ya mara mbili,sijawahi kutana na hizo changamoto.. mara ya mwisho nimenunua mwezi uliopita mwanzoni gari dogo tu kwa ajili ya wife.

Tulicho badilisha ni tires pekee na engine oils,maana gari ilikuwa inaletwa dodoma.
 
Sijafikiria kununua gari kwenye Yard zetu, maana Wabongo tunajijua Kwa janja janja

Kwani kuagiza na kusubiri miezi 2 gari yako ifike Kuna shida gani Chifu?

Kumbuka mwenda pole hajikwai 🤗
Miezi miwili mingi sana mkuu achilia mbali mwezi. Mi mwenyewe siwezi kumudu kusubiri

Bora anunue kwenye Yard ila ahakikishe anamjua Boss husika
 
Trust me, nisingeandika kitu JF kama ningekuwa sina uhakika...

Sometime tunaandika JF kwa kifupi sana ili kufikisha ujumbe, na kujaribu kuficha identity...
Kama huo uhuni wa kubadilisha vitu vidogo vidogo hata gari inapo ingia bandarini kutoka japan,jamaa huwa wanafanya hivyo..siyo kwenye yard pekee..kiufup umakini unahitajika
 
Miezi miwili mingi sana mkuu achilia mbali mwezi. Mi mwenyewe siwezi kumudu kusubiri

Bora anunue kwenye Yard ila ahakikishe anamjua Boss husika
Hadi nimjue boss tena aisee biashara gani hiyo kuwa unaenda kununua kibiriti duka la mangi hadi umjue bosi kujua kuwa atakuuzia kibiriti kilichojaa njiti hakijapunguzwa aiseee
 
Kama huo uhuni wa kubadilisha vitu vidogo vidogo hata gari inapo ingia bandarini kutoka japan,jamaa huwa wanafanya hivyo..siyo kwenye yard pekee..kiufup umakini unahitajika

Sasa mkuu ile ni kampuni ambayo watu wengi wanaiamini kwa sababu ya ukubwa wake...

Inakuwa sio fresh kwa wateja...
 
Nakubaliana na wewe Mkuu...
Security ya pale mgeni mwenyewe ukiingia tu unaogopa

Wale watu kwa upande wa Yard za bongo hawana mpinzani...Na yard nyingi Dar wanachukua magari kwao..
Gari ikiwa na changamoto wanakueleza...
 
Kabisa mkuu..na wana gari nyingi kama uchafu aisee. Na kila siku zinaingia,jamaa walisema pale wanazo wastani wa gari elfu 2..na wanasema kule tegeta wana stock nyingine za magari kama elfu 1.

Wakati yard zingine pale dar unakuta wana gari 30 tu 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…