Yafahamu magonjwa 20 ya mlipuko mabaya zaidi katika historia ya dunia

Mkuu, nakubali kabisa kuwa smallpox ilikuwepo tangu zamani za kale. Lakini ilianza kushambulia kwa Kasi hivi juzi juzi tu, Kama nukuu kutoka Wikipedia inavyosema - iliua watu millioni 500 miaka 100 zilizopita kabla ya kidhibitiwa 1980.

Halafu smallpox ilikuwa si inauwa tu, ukipoona inakuacha mlemavu na kuharibu maumbile kabisa!!! Ilikuwa ni ugonjwa mmoja hatari kabisa na hoja yangu ni kwamba inastahili kupewa namba yake maalum (pamoja na majina yake tofauti) kwenye listi ya magonjwa ya mlipuko!
 
OK nashukuru kwa kwenda sawa kwenye historia kwamba smallpox sio ya juzijuzi it is dated as far from 3rd century BC........
Sasa tusonge mbele kwenye swala lao kwamba kwa nn baujapewa upekee wa kulielezea?
Ukiingia mitandaoni kuna quite different classifications za pandemics na epidemics. Hiyo orodha yangu imejiweka zaidi kwenye time sequence tangu mlipuko wa zamani zaidi mpaka mlipuko wa sasa..... Sababu moja wapo ya kutoiweka smallpox ni historia yake kua ugonjwa ulianza lini hivo kuwa mgumu kuuweka kwenye orodha yangu....

Check👇👇
Thousands of years ago, variola virus (smallpox virus) emerged and began causing illness and deaths in human populations, with smallpox outbreaks occurring from time to time. Thanks to the success of vaccination, the last natural outbreak of smallpox in the United States occurred in 1949. In 1980, the World Health Assembly declared smallpox eradicated (eliminated), and no cases of naturally occurring smallpox have happened since.


Ndio maana pia hujaona historia ya ugonjwa km Hepatitis ambao uliathiri zaidi ya watu milioni 500 na kuua watu milioni 1 kila mwaka
 
Mkuu, kama historia ya smallpox haijaeleweka, kwa nini usiiweke kwenye prehistoric kama ulivyoweka ile Nr.1 ya China au kwenye fungu ya magonjwa yenye utata kihistoria? Kumbuka maada inazungumzia "Yafahamu magonjwa 20 ya mlipuko mabaya zaidi katika historia ya dunia"
 
Ahsante kwa mawazo ndio maana pia nimezunhumzia Hepatitis ambayo ilikua so deadly lkn haipo kwenye orodha yangu kwa mujibu wa muktadha wa namna niliyochagua kuwasilisha. Huwezi kuweka prehistoric km ilivo kwa PREHISTORIC EPIDWMIC:3000B.C. Kumbuka kua miaka ya B.C inahesabika kurudi nyuma which means 3000B.C is from 1B.C to 3000B.C hayo sio makadirio bali ni exact years. Sasa smallpox hizo thousands of years B.C utaandika ilianza 1B.C mpaka lini hapo ndipo shida ilipo mkuu....
 
Hivi kati ya Ebola na corona mpaka sasa kipi kilichokua na athari zaidi mpaka sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Covid-19 ina athari zaidi lkn bado hatujafikia kufanya angalau conclusion ya maambukizi na vifo yaani tunavoongea ndio imepemba moto....huko ulaya na marekani ni vifo vya kutisha kila siku......
 
Bado nipo tu, samahani kwa kuchosha!

Unasema "Sasa smallpox hizo thousands of years B.C utaandika ilianza 1B.C mpaka lini hapo ndipo shida ilipo mkuu", lakini mbona kwenye historia wamegawa timeline kabla ya BC vizuri tu katika Stone Age, Bronze Age, Iron Age, nk. Kwa hiyo kama umeweka listi yako kwenye timeline, unaweza kusema smallpox ilianza kwenye Bronze Age na inaeleweka kuwa ni zamani sana.

Hepatitis sio ugonjwa wa mlipuko, lakini kama imeuwa watu wengi, inatakiwa kuorodheshwa kwenye listi ya magonjwa hatari!
 
Ok sawa Kaka na ahsante kwa mawazo Ila unalazimisha sn kitu ambacho sio sahihi..........km kuna kitu unataka ni ruhusa kuandaa orodha nyingine km ipo na kwa muktadha utakaokua umeuzingatia.....hiyo hapo huwezi kuchomekea km ww unavoshauri....
 
Conspiracists watasema yalikiwa ni bio weapons au yalisababishwa na Babu yake Bill Gates.
 
Swali: Vipi kuhusu lockdown kipindi hicho....Hayo maradhi yaliondokaje duniani....Athari zake kwa Afrika ilikuaje?
 

Nilichojifunza : Time interval ya ugonjwa mmoja kwenda mwengine inapungua kila miaka inavyozidi kupanda
(Uartificial unatutafuna)
 
Nilichojifunza : Time interval ya ugonjwa mmoja kwenda mwengine inapungua kila miaka inavyozidi kupanda
(Uartificial unatutafuna)
Asante kwa kutafiti......kwa hiyo ina maana miaka ya mbeleni tutaanza kupata mangonjwa ya mlipuko mara kwa Mara?
 
Ok sawa Kaka na ahsante kwa mawazo Ila unalazimisha sn kitu ambacho sio sahihi..........km kuna kitu unataka ni ruhusa kuandaa orodha nyingine km ipo na kwa muktadha utakaokua umeuzingatia.....hiyo hapo huwezi kuchomekea km ww unavoshauri....
Nia yangu ilikuwa si kukukwaza bali kuelimishana!
Unaleta mada isemayo "Yafahamu magonjwa 20 ya mlipuko mabaya zaidi katika historia ya dunia" na ina maelezo ambayo ni factually incorrect! Mara unasema :
"Kwa hiyo kwenye andiko langu ugonjwa wa hapo juu Antonine Plague na American Plagues yalikuwa related na smallpox...." na "Hiyo orodha yangu imejiweka zaidi kwenye time sequence tangu mlipuko wa zamani zaidi mpaka mlipuko wa sasa"!

Hakuna ugonjwa wa mlipuko hatari iliyowahi kutokea duniani kama smallpox, na haijatajwa kwenye orodha lako!

Samahani kama nimekukwaza! I'll ignore you from here on!
 
JF ni sehemu ya kuelimishana na kujifunza mkuu japo sio ubishi sio wa lazima kwa hiyo usihofu tuendelee kujadili. Kuhusu swali lako tena maana wewe unaamini small pox ni mlipuko wa hatari uliowahi kutokea duniani. Kwa taarifa yako ili mlipuko uonekane ulikua hatari hauangaliwi kwa idadi ya watu waliokufa bali inaangaliwa rate ya kuua watu wengi kwa muda mfupi. Mfano wako wa wikipedia ni kua smallpox iliua watu 500mil kwa muda wa miaka 100 (ikiwa na maana watu mil 5 kwa mwaka, sasa kwa taarifa yako magonjwa km Heart Disisese (iliyoua watu 9mil kwa mwaka mmoja) na Stroke (iliyowahi kuua watu 6.5mil kwa mwaka) ndio most deadly. Hata death rate ya Black Death ilikuwa kubwa by far kuliko hiyo smallpox ambayo ilikuwepo "thousands of years". Karne ya 18 death rate ye smalpox was just watu 400,000 kwa mwaka.
 
Conspiracists watasema yalikiwa ni bio weapons au yalisababishwa na Babu yake Bill Gates.
Watu hawapendi wala hawataki kabisa kujihangaisha.......Hawataki kuchanganya na za kwao!!
 
Swali: Vipi kuhusu lockdown kipindi hicho....Hayo maradhi yaliondokaje duniani....Athari zake kwa Afrika ilikuaje?
Ni swali pana sana maana kila ugo0njwa walideal nao kulingana na jinsi ulivokua except hiyo Prehistoric Epidemic ambayo iliua kijiji kizima... lkn kwa sehemu kubwa magonja mengi either miji iliwekwa lockdown au walikua wanawatenga wagonjwa husika.

Mifano:
1. Plague of Justinian: Watu walikua wanawakimbia waliokua wanaumwa maana iliua nusu ya population ya dunia. Inasemekana waliopona ni wale tu waliokua na immune ya kutosha kukabiliana na maradhi yale.

2. The Black Death: Pamoja na lockdown, Wageni walilazimishwa kuwekwa kwenye isolation kwa muda wa mpaka siku 40 au quarantino (ndio chimbuko la neno Quarantine) ili kuprove kua hawakua na maambukizi.

3. The Great Plague of London: Hawa walipiga marufuku public gatherings na entertainments alafu waliwekeza sana kwenye utaratibu wa separate and isolate lakini walienda mbele zaidi kwa kuziwekea alama fulani nyumba zote ambazo zilikuwa na waathirika wa ugonjwa, madirisha yaliwekwa alma ya msalaba mwekundu yakiwa na maandishi "MUNGU UTUREHEMU". Kama ilipolazimika mtu kutoka nje ya nyumba kwa dharura basi alilazimika kushika fimbo nyeupe ili kuonyesha jamii kuwa ni mwathirika wa ugonjwa ili wakae nae mbali.

4. Smallpox: Inasemekana watu wa mexico na marekani ambako ndiko chimbuko la ugonjwa hawakua na immunity kabisa ya kupambana na gonjwa hili hivyo kufagia watu wengi sana. Kilichonurusu watu ni baada ya kupatikana chanjo na inasemekana huu ndo ugonjwa wa kwanza kudhibitiwa kwa chanjo.

5. Chorela: Hii ni maswala ya usafi zaidi, kuweka mifumo mizuri ya maji taka, kuwa na maji safi na salama ya kunywa nk ndio udhibiti wa Chorela.

Mkuu yapo mengi unaweza kufuatilia zaidi lkn angalau unaweza kupata picha namna gani walipambana na HALI ZAO
 
Pampja na kwamba Covid-19 inatisha na bado hatujamaliza hata mwaka lkn speed yake ni ya kawaida. Kwa muda wa miezi sita sasa tangu ilipuke, waliothirika ni milioni 3 tu huku vifo vikiwa 350,000 duniani kote
 
Bado imbombo ngafuu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…