Yafuatayo ni mauaji tisa (9) ya halaiki makubwa zaidi kuwahi kutokea Duniani

Yafuatayo ni mauaji tisa (9) ya halaiki makubwa zaidi kuwahi kutokea Duniani

AL SADY OLPLANER

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Posts
294
Reaction score
211
YAFUATAYO NI MAUAJI TISA (9) YA HALAIKI MAKUBWA ZAIDI KUWAHI KUTOKEA AMBAYO HAYAZUNGUMZWI SANA.

Ukisikia mauaji ya Halaiki (genocide) akili inakimbilia Rwanda , Soweto na Holocaust (waisrael walivyouliwa na WANAZI). Leo tunakupa Mauaji yaliyosahaulika lakini nayo ni makubwa mno.

1. WAJERUMANI WALIVYOSAFISHA KABILA LA WAHERERO.

Baada ya kusikia fununu ya madini Namibia, Wajerumani walikuja na kutawala pwani ya nchi hiyo na kukaa katikati ya kabila la waherero. Kosa kubwa wenyeji walipojifanya wabishi. Walizungukwa pande zote, Upande uliobaki ulikuwa ni jangwa ambalo visima vyote vya maji mjerumani alivitia sumu. Ukimbie unywe maji ya sumu au ufe na kiu jangwani au ukutane na risasi. Asilimia 80 ya wenyeji wote waliuwawa kikatili sana bila huruma.

2. WASOVIETI/USSR WALIPOHAMISHA JAMII NZIMA YA WACHECHNYA.

Kulizuka fununu kuwa Wachechya na Wainguish walikuwa wanawasaliti warusi wenzao vita ya pili ya dunia. Kuwapa adhabu serikali iliamuwa kubeba wote kwenye magari na kuwafukizilia maporini bila kumsamehe hata mmoja. Kila aliyebisha alikutana na Risasi . Wachechnya waliuwawa karibu 50% kutokana na sakata hili lililoitwa “Operation Lentil.”.

3. (HAITI) MAUWAJI YA PARSLEY/EL CORTE AU (KUKATWA).

Ukabila usikie tu redioni. Hii ilikuwa ni vita ya Kikabila, Wadominika walipanga kuwauwa Wahaiti karibu wote nchini mwao chini ya dikteta Rafael Leonidas Trujillo. Njia pekee ya kumtofautisha Mdominika na Muhaiti kwa walioleta utata kuwatambua ilikuwa matamshi ya hili neno "PARSLEY". Wahaiti walikuwa hawawezi kulitamka vizuri kutokana na Lugha yao. Wote walioshindwa waliuwawa kinyama. Kuepusha risasi zisiishe mapema, Hapa ilikuwa ni Mapanga na marungu asubuhi na mchana.

4. (TAIPEI REBELION) CHINA WATU ZAIDI YA 20 MILLION WALIPOTEZA MAISHA.

Hapa ilikuwa ni vita kati ya jamaa aliwaaminisha watu kuwa yeye ni Mdogo wake YESU. Akitawala karibu 1/3 ya nchi yote Hong Xiuquan. Akiongoza jeshi dhaifu kabisa kwa nia ya kuondoa kamali, uonevu, ndoa za wake wengi nk, China ilijikuta chini aya vita vya miaka 10 na kuacha raia zaidi ya 200 million wakifa na mamia kupotea.

5. UTURUKI DHIDI YA WANAVIJIJI WAASI.
Wanakijiji wa eneo la Dersim , walipoleta ubishi kuwa chini ya serikali ya Uturuki badala yake wakang'ang'ania sheria na taratibu zao, Jeshi lilitumwa, Makabila matatu yaliyojisalimisha yaliuliwa wote, Wakina mama na watoto waliokimbilia kwenye Mapango, Yalifunikwa na mawe, moto ukawashwa na wakafa kwa moshi. Inakadiliwa kwa siku moja watu karibu 2 MILLION waliuliwa na wengine kutekwa.

6. DICTETA WAKIRUSI STALIN ALIPOUA MAMILIONI UKRAIN KWA NJAA.

Waukraini walipata upenyo baada ya kuanguka utawala wa Czar Urusi wakataka kujitawala. Jenelali Stalin alipochukua Madaraka akaliona hilo. Pia Vradmil Lenin alikuwa kaishaweka mikakati ya kurudisha maeneo yote. Wao wakambishia na kuendelea na Harakati. Kwanza alikamata wasomi waliokuwa wanahojihoji 5000 na kuwaua wote, Akachukua mashamba ya raia yote. Akawapa adhabu ya njaa hadi nchi nzima isalimu amri kwake. Inasadikiwa kwa sababu ya njaa kila siku watu 2500 walikuwa wanakufa, na walifika watu karibu million 5.

7. MAUAJI YALIYOFANYA NA WAZUNGU DHIDI YA WAMAREKANI ASILIA (WAHINDI WEKUNDU).

Mamilioni ya hawa jamaa waliuliwa bila huruma. Ila hapa tutazaungumzia kabila dogo tu la MOQUI katika mji ulioitwa AWATOVI huko ALIZONA. Wahispania Makasisi walifika wakawalazimisha kuwa wakristo wakagoma. Ikabidi liitwe jeshi, maana wakazi waliwachukia wahispania na wachache waliobadili dini. Wanaume wakiwa kwenye sherehe Walivamiwa na kuuliwa. Wanaume wote. Wanawake na watoto wakachukuliwa mateka. Wakiwa njiani wakabishana wawapeleke wapi, wakaamua kuwaua woote ili kujipunguzia mizigo.

8: JEAN JACQUES DESSALINES ALIPOIGEUZA HAITI KUWA TAIFA LA WATU WEUSI ASILIMIA MIA.

Kile alichoshindwa kinjekitile wa Maji maji Haiti iliwezekana. Mzungu alikimbizwa na watumwa nchi ikapatia uhuru chini ya mkono wa watu weusi. Baada ya kiongozi wa mapinduzi kuuawa aliyemfuatia alipinga idea zake za kuwavumilia wazungu na machotara. Amri ilitolewa Kuua wazungu wote nchi nzima. Hakuishia hapo tu alipita kila mji kuhakikisha agizo linafuatwa. Katika mji mkuu tu wazungu zaidi ya 800 waliuawa kama wanyama na wengine kukimbia. Ilikuwa revenge ya aina yake. Hadi kesho haiti ni nchi ya watu weusi tu asilimia karibu mia kwa baara la Barani Amerika.

9: VITA VYA BIAFRA - NIGERIA.

Tofauti na tanzania tunamakabila mengi yanayopendana, na Nyerere alisaidia kikubwa, Hii haikuwa hivyo Nigeria. Wanamakabila zaidi ya 300 na yalikuwa karibu karibu kilichosababisha ugomvi mara kwa mara.Tatizo lilianza pale Kabila/kundi kubwa la IGBO walipojikatia nchi na kutengeneza nchi yao ya BIAFRA eneo tajiri kwa mafuta. Serikali haraka ikataka kuwarudisha. Kwa mbinu katili kabisa hata kuzuia chakula na maji yasielekee BIAFRA. Inasemekana kila siku walikuwa wanakufa watu zaidi ya 5000 wengi wao IGBO. Watu zaidi ya Milioni 3 walikufa hadi vita kuisha.

[HASHTAG]#FOLLOW[/HASHTAG] UKURASA HUU WA #HABARI_FORUMS KWA HABARI MAKINI ZAIDI
 
Kumbe wamarekani walikuwa wakristo kwa mtutu wa Bunduki kwa mujibu wa no.7, sasa si warud kwenye dini ya asili? halafu wanakumbuka zaid sept.11 kuliko mauwaji haya!!!
 
Aksante lakini sijaona mauwaji ya Kimbali kule Rwanda ilikua ni tishio kwa hapa East Africa, huwezi sahau hilo.
 
Mauaji ya tanganyika kwenye vita ya majimaji. Mauaji kwa mkwawa. Mauaji ya Syria. Iraq. Yugoslavia. Yemen. Kuwait. Kashmir. Soweto. Sudani kusini. Gaza. Sudan (magharibi). Afghanistan (×2). Libya. Na pia mauaji kwa wajerumani mwishoni mwa vita ya pili na BAADA YA VITA YA PILI KUMALIZIKA.

Maana baada ya WWII kuisha ulaya ilikumbwa na njaa na magonjwa na mjerumani hakupata msaada kama waliopatiwa wengine kwani alichukiwa na kila mmoja.

Inasemekana zaidi ya nusu ya wajerumani waliokufa walikufa BAADA YA VITA KUISHA kwa njaa. Magonjwa. Kubakwa na hasa kujinyonga kwa kutovumilia manyanyaso waliyofanyiwa na WASHINDI wa vita.
 
Kumbe wamarekani walikuwa wakristo kwa mtutu wa Bunduki kwa mujibu wa no.7, sasa si warud kwenye dini ya asili? halafu wanakumbuka zaid sept.11 kuliko mauwaji haya!!!

Mkuu
Marekani anayoiongelea hapa sio hii ya sasa,,hapo ana refer marekani ya around 1500 or 16th century. Hapo ni kabla waafrika hatujaanza kupelekwa Marekani kwa biashara ya utumwa,hao red indians ndo indigineous society ya bara la amerika before watu mchanganyiko unaouona sasa

Hii america ya sasa walioipa uhuru ni wazungu wenyewe Kina George Washngton na Benjamin Franklin,there is no way wanaweza kuwakumbuka hawa red indians coz their destruction made a way for a new great United States we see today
 
Mauaji ya Haiti hadi leo na kesho yanawagharimu.
Wazungu wanaifanyia figisu figisu vya kila namna.
Haiti ilipigana vita na Britain, Spain na France na kushinda zote.
Haiti ni ushahidi wa nguvu za mtu mweusi na siku sii nyingi tutawakaribisha AU.
 
Back
Top Bottom