Yah: Pesa za usajili & mishahara ya wachezaji wa Ligi Kuu ya Tanzania

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Sitoi ufafanuzi ila naomba kufahamu, ni kwa nini taarifa hazijulikani au hazipo wazi kuhusu pesa za usajili + mishahara ya wachezaji wa ligi kuu ya Tanzania? Au ni mimi tu ndio sifuatilii?

Ni vibaya kulinganisha nchi tajiri na nchi maskini, lakini ni vizuri tuige mazuri ya nchi tajiri kama England. Hapa namaanisha, huko England inatangazwa wazi kabisa mchezaji fulani kasajiliwa kwa bei fulani, na mshahara wake ni kiasi fulani kwa wiki. Jana FA ya England imetoa jumla ya pesa za usajili kwa timu zote za ligi.

Sasa kama ni mimi peke yangu sina taarifa, basi naomba mnisaidie wachezaji angalau wa kigeni wawili wawili kutoka Simba, Yanga, Azam, na Singida Big Stars, wamesajiliwa kwa TSH ngapi na mishahara yao ni kiasi gani kwa mwezi!
 
Ukishajua mishahara Yao na pesa za kusajiliwa itasaidia nini?
 
Ukishajua mishahara Yao na pesa za kusajiliwa itasaidia nini?
Sisi kama wadau wa soka si vibaya kufahamu, ili kujua tunatoka wapi na tunaenda wapi katika suala la maslahi ya wachezaji, mapato na matumizi ya timu zetu.

Kama hakuna umuhimu, mbona timu zinatuomba michango na kutaka mashabiki tununue jezi na kuingia viwanjani?

Kwani hao England kuweka hadharani taarifa za usajili ni wajinga? Ndio maana nimesema kuna ubaya gani kuiga mazuri katika nchi zilizoendelea?

Sasa na wewe nakuuliza, kuna ubaya gani mashabiki kufahamu taarifa za gharama za usajili + mishahara ya wachezaji?

Angalia taarifa za usajili wa Englad, wala siyo siri, zipo google tu!
 

Attachments

  • Screenshot_20220903-103211.png
    44.6 KB · Views: 23
  • Screenshot_20220903-103228.png
    27.8 KB · Views: 28
Kiuhalisia Tanzania hakuna uwazi kwenye mambo mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…