Sitoi ufafanuzi ila naomba kufahamu, ni kwa nini taarifa hazijulikani au hazipo wazi kuhusu pesa za usajili + mishahara ya wachezaji wa ligi kuu ya Tanzania? Au ni mimi tu ndio sifuatilii?
Ni vibaya kulinganisha nchi tajiri na nchi maskini, lakini ni vizuri tuige mazuri ya nchi tajiri kama England. Hapa namaanisha, huko England inatangazwa wazi kabisa mchezaji fulani kasajiliwa kwa bei fulani, na mshahara wake ni kiasi fulani kwa wiki. Jana FA ya England imetoa jumla ya pesa za usajili kwa timu zote za ligi.
Sasa kama ni mimi peke yangu sina taarifa, basi naomba mnisaidie wachezaji angalau wa kigeni wawili wawili kutoka Simba, Yanga, Azam, na Singida Big Stars, wamesajiliwa kwa TSH ngapi na mishahara yao ni kiasi gani kwa mwezi!