Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Lakini, chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Umuhimu wa chumvi katika maisha
Ndio kiungo pekee kinachotumiwa na na asilimia 99.99 na wanadamu wote duniani.. Ndio kiungo kwenye chakula muhimu zaidi kinachonogesha na kuleta ladha kwenye chakula.
Chumvi haiharibiki. Lakini, ikiharibika inafanywa nini?
Haifai tena kabisa bali hutupwa barabarani na kukanyagwa na watu. Je, kwenye maisha yako umeshawahi kuona chumvi iliyoharibika na kutupwa? Jibu laweza kuwa hapana kwakuwa chumvi haiharibiki.
Mojawapo ya kazi za chumvi ni kuzuia kuoza na kuharibika
Kama vile chumvi ilivyo na umuhimu kwa wanadamu, ndivyo hivyo hivyo huweza kukufanya kiroho ukawa na umuhimu wa wengine
Waswahel hawasemi fulani kala sukari nyingi la hasha bali husema kala chumvi nyingi! Ni kwasababu ya umuhimu wake mwilini.
Unaweza ukamaliza siku bila kula sukari lakini sio chumvi. Watu wenye umri mkubwa huambiwa wamekula chumvi nyingi kwa maana ya kwamba katika umri wao wameona mengi na mengine mengi.
Ukila sukari nyingi Maisha yako yatakuwa mafupi sana, lakini sio chumvi!
Maisha ni changamoto na changamoto ndio chumvi inayokujenga na kukufanya imara zaidi. Ukomavu wa akili hauletwi na shangwe na karamu(sukari) bali changamoto na mitikisiko ya maisha.
Vidole vyako ndio changamoto zako za maisha. CHUMVI na kucha zako ndio starehe zako katika maisha!SUKARI..!! Si unaona ilivyo rahisi kukosa ukucha kuliko kukosa kidole?
Ulemavu wa kukosa kucha hauwezi kufanana kamwe na ulemavu wa kukosa vidole! Unajua ni kwanini? Kucha ziko kwenye vidole kama vile tu shangwe zilivyo kwenye changamoto na chumvi inavyotumika zaidi kuliko sukari.