Yahusu magonjwa ya moyo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Vitu usivyoweza kuviepuka katika magonjwa ya moyo ni
Umri, Vinasaba, Jinsia na Asili yako

Vitu vinavyoepukika ni;
Uzito wa mwili, aina ya chakula unachokula,
Mazoezi ya mwili
Uvutaji wa sigara
Unywaji wa pombe

Umri:
Umri unavyozidi kusonga mbele ndiyo hatari ya magonjwa ya moyo inavyoongezeka. 60+ ni umri wa kujiangalia sana.

Vinasaba.
Kama mzazi wako anasumbuliwa au alisumbuliwa na magonjwa ya moyo, una nafasi kubwa ya kurithi.

Jinsia;
Wanaume wana hatari zaidi ya kusumbuliwa na magonjwa ya moyo kuliko wanawake. Wanawake walio katika umri wa kuzaa homornes zinawasaidia. Baada ya menopause hatari huwa sawa kwa wanawake na wanaume.

Asili:
Magonjwa ya moyo husumbua sana Waafrika, Wahindi na Waarabu na Wahispannia kuliko Wazungu, Wachina na Wajapan.
 
Hapo kwenye asili, Nahisi Wazungu, Wachina na wajapani tamaduni zao za kuishi zinawafanya wasiathiriwe mno na maradhi ya moyo.
Kuna haja ya kuwaiga mfano ufanyaji mazoezi waafrica wengi tumekua wavivu.
 
Hapo kwenye asili, Nahisi Wazungu, Wachina na wajapani tamaduni zao za kuishi zinawafanya wasiathiriwe mno na maradhi ya moyo.
Kuna haja ya kuwaiga mfano ufanyaji mazoezi waafrica wengi tumekua wavivu.
Wanasayansi wamebaini na genes zetu zinachangia. Ukiwa kutoka Afrika, India, Arabuni na Hispania ukifikisha miaka 40 nenda kafanye check up.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…