Habari ya leo wana JamiiForums wenzangu na waTanzania wenzangu,
Napenda kuwaletea habari hii inayuhusu kampuni moja inayoitwa Agiza Kimchina ambayo ipo maeneo ya Salasala katika jengo la Kimchina Dar es Salaam, Mke wangu aliagiza simu kutoka china kupitia kampuni hiyo toka mwaka jana mwezi wa sita na mpaka mwaka huu simu hazijafika, mke wangu alitake trouble ya kufuatilia baada ya kufika ofisini kwao wakamuambia kuwa simu zilikuja lakini zikawa mbovu so zikarudishwa China
Wakamuahidi baada ya mwezi watampigia cha kushangaza ukiwapigia simu hawapokei na hawana ushirikiano wowote
Naomba kutoa angalizo kwa waTanzania wenzangu hawa watu ni matapeli na maamuzi nilichukua ni kwenda ofisini kwao na Polisi, kwa sasa naelekea kituo cha Polisi kwa ajiri ya kuchukua RB na kufanya utaratibu wa kwenda ofisini kwao ili nipate kurudishiwa pesa zangu ambayo ilikuwa 200,000/= ya simu pamoja na 98,000/= ya usafiri.
Naomba mnisaidie kusambaza hii taarifa.