Yahusu: X-RAY ya Kifua

Fabian the Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
756
Reaction score
751
Habari zenu ndugu zangu, Nimeenda hospitali juzi kwa kuwa nilihisi maumivu hapa katikati kabisa ya kifua kwa ndani, sio maumivu makali ya kunifanya nisifanye kazi na yanasikika tu kwa kufanya movements flani ivi au kubeba vitu vizito.

Daktari akashauri tufanye X - ray ya kifua pamoja na vipimo vingine kama vitatu then tutajua shida ni nini. Kwakweli kwa namna ninavyoifahamu X-ray niliyoisoma form 4 na form 6 nilimuomba daktari aniruhusu kwanza nijipange ki saikolojia ndo niende. Ninachofahamu ni kwamba hii kitu ina madhara makubwa sana, na kwamba hata wagunduzi wake walikufa kwa sababu ya hiyo hiyo X-ray.

Naomba mwenye uelewa na hii kitu, au ambae ashawahi kuifanya anisaidie kunijuza, maisha yanakuwaje baada ya kufanya hiyo X - ray ya kifua. Ahsanteni
 
Acha uoga mkuu.

Mimi hapa nimeshapiga X-RAY zaid ya tatu na maisha yanaendelea bila shida.
 
hahahaha chagua bora miale ya x ray ama maumivu, kifupi ujaumwa vzr mbona huta omba ruhusa ufikirie madhara ya iyo x ray
 
x ray inashida sio kila sehemu hasa sehemu za reproduction ndo tatizo kwahyo wee piga tuu hiyo ya kifua
 
Watu wanapiga mpaka x ray 6 kwa ugonjwa mmoja we kamoja tu unaogopa, madhara kawaida maana hata panadol yenyewe ina madhara
 
ila kama unamimba pia sio nzur utasababisha mutation ya multiplying cells za mtoto
 
huna haja ya kuhofia chochote, haina madhara yoyote... Kwasababu unakuwa exposed to only a small amount of radiation for a short period of time.

Inaweza kuleta madhara pale tu utakapo kuwa exposed to large amounts of radiation... Na hicho ndo kilicho muua Marie Currie... Kwasababu over time her exposure to xray radiation ilikuwa kubwa....

So mkuu for the benefit of your health we kapime to hiyo xray kwasababu haitaku affect chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…