Yajayo yanafurahisha, Jifunze hii taaluma itakusaidia

Hahaha sawa endelea naye huyo kwanza, mi nitakusubiri uamke tuendelee na mashule mkuu
 
Hii kitu naona ni sawa na mambo ya kufikia ikawa tu, hakuna tofauti na issue ya babu wa loliondo. Watanzania tufanye kazi na kuacha kudanganyika na haya mambo!
Hivi unaelewa lolote juu ya Cryptocurrency!? Tuanzie hapo maana ninaweza kuanzisha mjadala na crack head.
 
Mkuu nmefuata kila ulchoelekeza kwenye airdrop ila nadhan nahtaji maelekezo mengine ya msing zaidi. Nshaingia mpka kwenye group zao za telegram, nakwama sasa jinsi ya kuendelea baada ya kukamilsha hlo au ndio nacheza na link waliyonipatia tu huo kwa ajil ya kupata coins?
 
Muhimu ni wewe kutumia hiyo link vizuri ili upate coins but deadline iko arroud the corner.
 
Hahaha hata hajamaliza kutoa shule umeanza kufanya mtihani?! Uki fail usilalame, shule haijaisha utaibiwa acha haraka,ona sasa ushaanza kutoa macho.
 
Ngoja niendelee kubet nipate hela ya kulisha familia tu maana hapa sielewi kitu
Unaweza kudhani umeelewa, siku ukiingiza pesa utakuwa kama Dr.Shika, utakuwa Tajiri mtandaoni but in real life utakuwa kama matonya.
 
Sikumbuki kama kuna dili la pesa nzuri mtu anapiga pesa hasa Mtanzania akawashirikisha wenzie haraka kiasi hicho tena mitandaoni. Hizi biashara za kizungu hebu tufanye kuwaachia wenyewe.
 
Hahaha hizi pesa za mitandaoni ni kuwa nazo makini
Hahaha tena uwe makini sana usije ukazipoteza, maana utaumia moyo.
Mi naogopa kujilisha upepo, una pesa mtandaoni huwezi kula kwa mamantilie?! Huwezi lipia nauli ya mwendokasi?! Huwezi lipia ada ya shule, sasa nini faida ya kuwa na cryptocurrency?! Bitcoin nitaitoaje kwenye ATM hapa azikiwe crdb?!
 
hiyo tumuulize mtoa mada
 
Samahani Kidogo ndugu Humble African,Hivi wewe na Ontario wa Forex mna Undugu wa Damu?
Maana nimejiridhisha kupitia chagizo zenu mbalimbali yani the way mnavyo jibu hoja na nondo mnazoshusha ni kama kuna mfanano hivi,sorry kwa kukutoa nje ya Mada.
 
Samahani Kidogo ndugu Humble African,Hivi wewe na Ontario wa Forex mna Undugu wa Damu?
Maana nimejiridhisha kupitia chagizo zenu mbalimbali yani the way mnavyo jibu hoja na nondo mnazoshusha ni kama kuna mfanano hivi,sorry kwa kukutoa nje ya Mada.
Wow! My heart has melted kuona maandishi yako mkuu. Very true and inspiring.

Ni kweli kabisa nilikuwa nae group moja la Forex na watu walikuwa wakinifananisha nae kwa uhandishi wangu, naheshimu sana maandishi ya ONTARIO maana anajua kutumia maneno sahihi kulingana na muktadha husika.

Ila kama na wewe umeliona hili basi una jicho la maandishi.

Hugs.
 
Kama ni fursa na ni kitu kizuri...kwanini unatushirikisha?...ha ha ha...hupati mtu hapa
 
Tatizo la hizi cryptocurrency ni hawa ma investor wadogo na wasio na elimu ya kutosha juu ya nini wamewekeza.
Ikiyumba kidogo wanaondoa mitaji yao na pesa ndipo inazidi kuanguka kama ilivyotokea kwa bitcoin yani wao ndiyo wanaishusha thamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…