Yajayo yanafurahisha, Jifunze hii taaluma itakusaidia

Yap yap...siku wahusika wakipata faida ya kutosha wakizima "System" hizo hela si ndio tayari mshalizwa??
Hahaha hakuna hela, zile number tu. Mi sina haraka na utajiri nitasubiri nianze kuziona Bitcoin uswahilini nami nitazinunua.
 
my brother bitcoin na other crptos' zitaishia kutumika kwenye deep web pekee, huku kwenye dunia ya vipofu sidhani kama ita survive.
mfano kama mimi vile sina shida ku invest, ila nataka free bitcoin kwanza ni invest nione zikipanda nitoe afu ndo niwe na uhakika nazo. maana mi najua haziko stable hizo. mwisho wa siku tusamehe tu sisi waafrika wenzako wenye akili za kuku [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi kuna tofauti gani kati ya hii na Forex?
Samahani nauliza tuu sifukui makaburi.
Usijali Kasie nazijua busara na hekima zako na naamini unataka kujifunza kitu kipya.

Iko hivi Forex ni kifupi cha "foreign exchange" yaani maana yake ni soko la ubadilishaji wa fedha lililowekwa katika muktadha wa digital global foreign exchange yaani soko la dunia la ubadilishaji wa fedha hivyo hii ni biashara sawa kabisa na bureau de change isipokuwa Forex imekiwa advanced na unauza na kununua kwa kitu kitaalamu wanaita "leverage" kutoka kwa broker yaani ile hela ya broker anakuazima uongezee kufanyia biashara ya kuuza na kununua fedha. Na hapa ndipo risk kubwa na faida kubwa zinakuandama maana kwa mtaji wa dola $100 unaweza kupata faida ya dola hata $700 at the same time analysis zako zisipoenda sawa unaipoteza hiyo dola $100 haraka sana. Ni leverage pekee ndio inaitofautisha bureau de change za mtaani na hii bureau de change ya mtandaoni "digitalized" yaani Forex.

Na ukubali ukatae ushafanya hii biashara kwa namna moja au nyingine fikiria umesafiri na kulazimika kununua fedha za nchi husika ili utumie utakapoingia nchi hiyo then baada ya kununua na kuingia nchi husika then unatumia kiasi kidogo na unarudi border kubadilisha unakuta thamani ya tshs imepanda dhidi ya fedha ya Kenya unaondoka na kafaida ka tshs kadhaa. Hapo unakuwa umefanya Forex bila kujua. So Forex its not a scam as watu wanaclaim its legal online digital foreign exchange market.

Hii ilikuwa Forex but Cryptocurrency haina ushabiianisha hata kidogo na Forex maana Cryptocurrency ni digital virtual money used for transaction and investment. Hizi ni fedha za mtandaoni ambazo zimetengenezwa kwa only code number kwa kutumika kwa ajili ya manunuzi na uwekezaji. Baba yao akiwa Bitcoin alietengenezwa mwaka 2009 na mjapan anaeitwa Satoshi nakamoto kwa lengo la kuondoa urasimu katika taasisi za kifedha kwa kuondoa middle man mtu wa kati amabe huwa anakula kamisheni zetu tukituma na kununua vitu mbali mbali kupitia mabenki. That's why mfumo wa hii sarafu ya mtandaoni ni decentralized na sio centralized ukisika centralized ina maanisha uchumi ulio na center inayogovern na kuregulates fedha zote za dunia au nchi husika..mfano USA wana Federal reserve then Tanzania tuna BOT. But dhumuni la Cryptocurrency ni kuwa decentralized ukiona "de" kwenye neno la kiingereza ni ukanusho ina maana Mimi na wewe tunakuwa benki na kutokuwa na centralized inayokula kamisheni zetu kirahisi kwa kututunzia hela zetu na kutusaidia kufanya miamala sasa Bitcoin na virtually digital money zote zinafanya haya yote bure.

Nafikri hata Bitcoin wamechelewa maana sisi huku tayari tulikuwa na digitally Money ya mpesa tangu zamani sana na hii ni digitalized codes tu kwani kuna mtu alishashika mpesa hapa? Hapana!? Its just virtual money tu haishikiki Bali ina thamani na pia hii mpesa hii yetu inatumika pekee kwa miamala na sio investment kama vile Bitcoin inavyotumika kwa sasa. Store of value at the same time transaction money.

Experts and scholars wa masuala ya virtually money and Cryptocurrency wanasema hadi 2020 half population ya dunia watakuwa wana smartphone hivyo wataadapt huu mfumo mpya wa digital money na kufanya paper money kitaalamu zinaitwa "fiat Money" zote zitumike pamoja na kuexist peaceful within monetary social world though watu watapoteza imani haraka na paper money kutokana na nature yake ya urasimu wa hizi centralized institutions na imani itaongezeka kwenye decentralized hizi Bitcoin and other Cryptocurrency kutokana na kutokuwa na urasimu.

I hope it make sense kwa haya maandishi.
 
Yap yap...siku wahusika wakipata faida ya kutosha wakizima "System" hizo hela si ndio tayari mshalizwa??
Hawawezi kuzima system maana hizi hela zinatengenezwa katika mfumo wa block chain technology inayoifanya hii pesa iwe ngumu hata kuwa hacked maana inakulazimu uzime kompyuta za dunia nzima na kuzima internet ya dunia ili kuzima hizi hela ndio maana hata USA wameshindwa kuzizima Bali wanajitahidi kuzipiga marufuku maana ni mwiba kwa uchumi wao sababu wanakosa Yale meno ya kucontrol uchumi wa dunia.

Na wakizima internet ina maana hata nuclear zao hawawezi kuzirusha maana ni computerized.
 
mmiliki au mwanzilishi wa bitcoin ni nani
 
Kama ni fursa na ni kitu kizuri...kwanini unatushirikisha?...ha ha ha...hupati mtu hapa
Unadhani ni wote watadharau kama wewe mkuu!? Unajua wapo watu wanaoheshimu na kufuatilia fursa hadi mwisho at least watafuatilia na kujua hii hata zaidi yangu. Suala la wabongo kutokushirikisha fursa ule ni uzamani vijana wa kisasa ...hatuko hivyo.

Na hizi hela sio zangu ni za ulaya kwa hiyo nakushangaa Mimi nawaingizaje sasa mkenge maana sio hata kwamba natanza darasa la kuwafundisha..hapana. Ninajaribu tu kushare knowledge and experience yangu.

Kila siku jifunze ukikataa kujifunza utakuwa funza. Nahisi hata common sense yako sio common that's why huko negative hata kwenye ideas zako.
 
Tatizo la hizi cryptocurrency ni hawa ma investor wadogo na wasio na elimu ya kutosha juu ya nini wamewekeza.
Ikiyumba kidogo wanaondoa mitaji yao na pesa ndipo inazidi kuanguka kama ilivyotokea kwa bitcoin yani wao ndiyo wanaishusha thamani.
Huu ndio ukweli..small investors bado hawajatrust this technology enough but big investors wao hawana shida ndio maana utoana kuna strong support ya Bitcoin hii ni ile pesa kubwa iliyowekezwa na akina Bill gate na wale jamaa mapacha. Wanaamini dunia ukibali ikate this is the future money.

Na ukitaka kuamini hili Leo Venezuela wamelaunch pesa yao inaitwa perso na unakuwa nchi ya kwanza kuingia kwenye huu ulingo wa Cryptocurrency kaka nchi. Hii ni green light kwa hii technology ya block chain kukubalika na kupiga jeki chini za nchi zilizokufa. Hata Zimbabwe angekuwepo Mugabe watu wangeahamia Cryptocurrency.

Its safe, autonomous, reliable, independent and convenient economy.
 
mmiliki au mwanzilishi wa bitcoin ni nani
Mmiliki wake ni mjapan anaitwa satoshi nakamoto ni mtaalamu wa cryptography and algorithm coding. Jamaa ni genius sana ametengeneza kitu ambacho kimekuja kuweka uchumi wa dunia huru dhidi ya makucha ya mabepari. Maana if you can be your own bank? sasa Benki unakuwa na kazi gani? Mabenki yatakufa in the near future..tuombe tu uzima lakini maandishi yangu haya..kuna watu watarudi 2023 kuja kujisomea tena na watakiri na kuhisi I'm prophet kwa namna ninavyo prophecy future ya virtual monetary system.

Na punde tu baada ya yeye kulaunch hii pesa akatoweka na Mara ya mwisho kuonekana ilikuwa kwenye forum moja ya masuala ya cryptography alikuwa anaidiscuss na wenzie juu ya hili wazo lake then hakuonekana tena hadi Leo hii na wala hajajitokeza kusema Bitcoin ni yangu but hili na yeye haibe inatakiwa ahack kompyuta zote duniani hivyo hata yeye hana mamlaka na Bitcoin na hadi Leo hajaonekana maana anajua USA alichowafanya wakimpata wanamla nyama maana kadhoofisha kabisa uchumi wao. But yeye ameasisi wazo na kutengeneza sarafu yake ambayo kwa sasa ndio dola ya mtandaoni inayoheshimika sana na ukitaka kufanya manunuzi mengi mtandaoni inawezekana ukiwa na Bitcoin pekee na hata unaweza kuitoa na kutumia kama shilling tu. Ila kwa sasa kuna sarafu zaidi ya 1500 na zote zinafanya kazi na watu wanazitumia kama transaction na investment at the same time.

No excuse huku ndio dunia inakoelekea wale mambumbu wasiotaka kujifunza vitu vipya dunia itakuwa jehanamu kwao kwa jinsi wenye nguvu ya elimu na ufahamu watakavyoiteka. Jifunze sasa maana elimu haina mwisho.
 



Ahsante Mkuu,nimetosheka na ufafanuzi wako Mkuu
 
We subiri ugeuzwe Deci atakwambia lipia semina kama yule jamaa wa forex
 
We subiri ugeuzwe Deci atakwambia lipia semina kama yule jamaa wa forex
Kwa negative mentality kama hizi zako Wabongo tutaendelea kurithishana umaskini vizazi hadi vizazi.

Nilitegemea umepata kusikia idea kama hii at least ungetumia muda wako kujifunza na kujua how you can benefit from this technology hata kwa kusafiri mbali kujua hili mswahili unaponda na kutoa tahadhari ya kitu usichokijua.

Mimi wazo la kuanzisha semina ndio hata alipo kichwani maana sipendi kero za kiswahili na sipendi ubabaishaji. Maana ukisikia nimeanzisha semina nitakuwa nababaisha maana sina resources wala enough capital ya kuifanya biashara yangu iwe modern and high quality.
 
Ni mtu na binamu yake yaani kitu damdam
Unajibu kitu usichokijua na kuendelea kuonesha jinsi ulivyo mjinga na mpuuzi wa mambo, yaani kweli kwa hilo swali hapo juu unaweza kulijibu kwa mstari mmoja kama huo?

Yaani umekubali kazi ya kichwa chako iwe kufugia nywele tu na sio kuhifadhi masuala muhimu ya kitaaluma. Inasikitisha sana.
 
Nimekuelewa ila hujasema namna ya kupata hz hela zetu za madafu nikihitaji toka huko kwenye account ya crypto currency kama tufanyavyo mpesa?
 
Tatizo umekuja kama bwana yule wa forex aliyeaminika sana, same tactics ila mwisho wa siku yakatokea yaliyotokea, kipindi kile kauli mbiu ilikuwa fx ain't for everyone sasa wewe sijui kauli mbiu yako ni ipi?
 
Sawa sawa Boss
 
Nimekuelewa ila hujasema namna ya kupata hz hela zetu za madafu nikihitaji toka huko kwenye account ya crypto currency kama tufanyavyo mpesa?
Its very simple kuzigeuza kuwa tshs ingawaje dhumuni ni kutoa hizi paper money na kusisitiza matumizi ya hizi Cryptocurrency maana kwa sasa hadi be forward unaweza kununua magari kwa Bitcoin.. Lamborghini magari yao wanauza kwa Bitcoin...Microsoft wanauza bidhaa zao kwa Bitcoin.. Ulaya nchi nyingi zina ATM za kutolea Bitcoin kama hardcash so kwa ulaya wamefikia pazuri.

Ila kwa huku kwetu kuna njia mbili njia ya kwanza ni kupitia kuzibadilisha kutoka Cryptocurrency kuwa paper money kwa kuziuza mtandaoni kwa wateja walioko lukuki mtandaoni wanafanya kugombea wakisikia unauza maana ni adimu muda huu Mimi hapa nauza baadhi ya hizi sarafu za mtandaoni hizi Cryptocurrency mteja wangu alieko Vietnam anaitwa Nguyen angalia hizi screenshot za mazungumzo yangu na yake.
its very simple, convenient and faster muda huu nauza kama za laki mbili za kupigia mtungi jioni. Sasa wewe kabebe rumbesa kariakoo ukidhani utajiri unapatikana kwa maguvu..utajiri unapatikana kwa kufanya kazi kwa akili ukitumia nguvu utadeki bahari. Ndio maana wanaotumia akili wanalipwa kingi kuliko wanotumia nguvu..rejea malipo ya majeshi..wanaosonga mbele wapiganaji wanalipwa posho tu..wanaotumia akili wanalipwa mshahara kabisa. Japo wote wanaamini wanalipwa mshahara.

Pale mikocheni kuna sehemu wanachukua Bitcoin kwa manunuzi ya vitu mbali mbali. Mkuu tuna bahati kuvijua hivi vitu in its early stage..tujifunze kwa wakati wetu ukitegemea nitaleta semina elekezi Mimi sileti ng'o..nachofanya ni kuraise awareness tu basi ili wenye macho waone na wenye masikio wasikie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…