Yajue baadhi ya mambo ya Upagani yaliyoingizwa na kufuatawa katika Ukristo.

Krismasi
  • Ni kweli hakuna mtu mwenye uhakika wa tarehe aliyozaliwa Yesu
  • Uhakika ni kwamba Yesu aliwahi kuzaliwa duniani
  • Sio dhambi kuchagua tarehe maalum kwa kumbukizi ya kuzaliwa Yesu
  • Ni kumbukizi ya tukio sio tarehe ya tukio, hata kama tungekuwa na uhakika Yesu kazaliwa Machi sio dhambi kufanya kumbukizi maalum ya tukio hilo Disemba.
Siku ya Ibada
  • Msisitizo wa Biblia ni kwa waliomwamini Yesu ni kukutana sio siku gani au saa ngapi kukutana
  • WAKOLOSAI 2:16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Utatu, Pasaka na Kuzimu
  • Kufanana kwa wanachokiamini wengine haina maana unachoamini wewe sio sahihi. Binadamu wote tuna asili ya kuabudu ndani yetu, kwa hiyo sio ajabu kuona baadhi ya mambo ya kiibada yakifanana fanana. Yote ni katika jitihada za watu kumtafuta Mungu.
  • Siku za mwisho pia Shetani atafunua utatu wake; Nabii wa Uongo, Mpinga Kristo na Shetani mwenyewe.
Mengine labda ni mambo ya dhehebu moja tu katika ukristo hayo wenye ujuzi nayo watakujibu
 
Wewe kama una hasira meza wembe!
 
Ukilristo na wakristo uhukumiwa kwa matendo ya kiroho
Hizo ibaada na taratibi za maisha hazihusu ukristo

Kwa maana hiyo ukristo ni universal faith lakini watu wanaweza kuwa na tamaduni zao bila kuathiri ukristo


Mchanga anaweza endeleza tamaduni wake bila kuathiri ukristo vivyo hivyo kwa mhaya na msukuma

Yesu hakufundisha ukristo uendeshweje katika Maida mbalimbali

Yeye alifundisha Upendo kuacha dhambi na ufufuo wa wafu na uzima wa milele hayo mengine ya kula, siku miaka, mtajiju kuvaa,
 
Duh!
 
Huyu ndiye mungu wenu [kwa mujibu wa kitabu chenu/Qur'an]mtizame vizuri,na uthibitisho wa maandiko yenu upo hapo.
Hadith imekuja sahih ila sio kama hapo pichani , umbile lake linaendana na utukufu wake hapo ni maelezo tu lakini uhakika anajua yeye mwenyewe maana hata paka ana miguu lakini haifanani na yako.
 
Nijikite katika hoja ya sanamu katika ibada.Ikiwa Mungu ni roho,wenye hekima hukiri kwamba:ni vigumu kumfundisha mtu mambo ya kiroho pasipo kielelezo.Sidhani kama hapa duniani kuna imani ya kuabudu sanamu bali uwepo wa sanamu mahali pa ibada ni kutakasa(sanctify) ili pawe patakatifu na ndipo roho wa mungu hufika.Jiulize kwa haya:wakati Mungu ananena na Musa wakati akiwa machungani kwa nini alijidhihirisha kupitia kijiti kinachoungua bila kuteketea?Kwa nini hakunena moja kwa moja?Wakati Mungu anamwambia Musa achonge sanamu ya shaba ili wana wa Israeli waumwapo na nyoka wamtazame nyoka wa shaba ili wapone,je sanamu ya shaba iliwaponya au ni Mungu mwenyewe kajidhihirisha kupitia sanamu?Unayekataa kielelezo Mungu wako anajidhihirishaje?Huu ugonjwa wa akili(exemplary tantrum) unaomfanya mtu abwatuke ndivyo roho wa Mungu anavyojidhihirisha kwenu?Ni vema uzi ukabaki ili tutokapo mihangikoni tuukute na tuendelee kubabadua kwani mleta mada anahitaji kuelimishwa kwa mengi,akiachwa ataathiri jamii kwani ana kundi kubwa atakalolifundisha ujinga wake.
 
Kwanini Mungu mwenye nguvu alishindwa kuwazuia wapagani kuharibu neno lake la kweli?

Je anapenda hali hiyo au Hana uwezo wa kuzuia au pengine Hayupo kabisa ni hadithi tu?
 
huo wote ni upangani
 
Na ninyi hamkufanya juhudi yoyote kukeep records ya dini yenu??
 
ata ukimpenda sana demu wako pia ni upagani{ushirikina]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…