Yajue haya kuhusu sisi wapare mengine yakishujaa mengine yakusikitisha !

Yajue haya kuhusu sisi wapare mengine yakishujaa mengine yakusikitisha !

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
1. Eneo linaloitwa kavambughu.
Hapa tuliwapiga wambugu kwenye vita na eneo hili lipo mpaka leo.

2. Eneo linaloitwa Nkhoma ya mkwavi au fuvu la mmasai.
Hapa wamasai walituvamia ikapigwa vita kubwa tukawauwa wote tukashinda vita na eneo hili lingalipo mpaka leo.

3. Jiwe la mkumbavana.
Hili ni jiwe ambalo lipo mpaka leo ukizaa mtoto mwenye ulemavu au ambae meno anaota kuanzia juu bàsi mtoto huyo hupelekwa kwenye hilo jiwe kileleni na anawekewa chakula mbele kwenye ukingo wa kuangukia bàsi akisikia njaa akikifwata kile chakula hudondoka na kuporomoka kutoka futi zaidi ya mia mbili na kufariki. Eneo hilo lilikuwa na mifupa ya watoto mpaka miaka ya hivi karibuni.
 
kwani mtoto anayeota meno ya juu anakuwa na shida gani?
Jamii nyingi za kiafrika wapare wakiwemo waliamini kuanza kuota meno ya juu ni mkosi na laana kwenye jamii ukoo au familia hivyo watoto wa aina hii waliuwawa kwà njia hii au walitwangwa kwenye kinu.
 
Back
Top Bottom