Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Hapa duniani kuna watu wanaishi maisha ya ajabu sana. Watu hao ni wale wanaokiri kwamba wametubu dhambi zao, wanaamini kuwa Yesu ni Bwana, na wanaishi maisha matakatifu. Wanaowabeza na kuwadharau watu hao huwaita “walokole.” Haya ndiyo maajabu 20 ya maisha ya “walokole:”
Kama ulidanganyika na kuamini kwamba kuokoka ni ujinga basi leo umeujua ukweli. Kuokoka ni faida na wala sio hasara.
Those are the tangible and experiential benefits of salvation. If you were previously misled into believing that surrendering to Christ is folly, today you have encountered the undeniable truth. Welcome to the sanctified family of the redeemed in Christ.
- Hawalogeki. Wachawi wakijaribu kuwaloga ili waugue au wapate mikosi, uchawi wao unafeli. Isa 54:17
- Wakifanya biashara, pesa yao haiibiwi na 'chuma ulete.' Mungu analinda kazi zao. Kum 28:8
- Hawaugui magonjwa ya zinaa kama vile Syphilis, Gonorrhea, Chlamydia, Genital Herpes - HSV-2, Human Papillomavirus - HPV, Trichomoniasis, Chancroid... kwakuwa uasherati na uzinzi ni marufuku kwao. 1 Kor 6:18
- Wana amani tele hata katikati ya dhoruba za maisha. Yn 14:27
- Maombi na dua zao zinajibiwa. Yer 33:3
- Wana furaha ya kweli isiyoyumbishwa na hali za dunia. Neh 8:10
- Mungu huwalinda dhidi ya maadui zao. Zab 91:7
- Wana ujasiri wa kipekee. 2 Tim 1:7
- Wanaona miujiza mingi katika maisha yao. Mk 16:17-18
- Wanapokumbwa na majaribu, wanashinda kwa kishindo. 1 Yoh 5:4
- Wanaongozwa na Roho Mtakatifu katika maamuzi yao. Rum 8:14
- Hawafi mapema kabla ya wakati wao. Zab 118:17
- Mungu huwafungulia milango ya fursa na neema. Ufu 3:8
- Hawana hofu wanapolala usiku. Wanalala usingizi wa amani. Zab 4:8
- Wanapotoa, wanabarikiwa maradufu. Lk 6:38
- Wanapata ushindi bila wao kupigana kwa kuwa Mungu huwapigania. Kut 14:14.
- Wanakwepa mitego ya adui kwa ufunuo wa Mungu. Amo 3:7; Mt 10:26
- Wanapitia magumu, lakini wanatoka wakiwa na ushindi. Yk 1:12
- Mawazo yao yamejaa amani na si hofu. Isa 26:3
- Hawadanganywi kirahisi na mafundisho potofu, kwa sababu wana Roho wa Mungu. 1 Yoh 2:27