Yajue maajabu 20 ya maisha ya "walokole"

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
Hapa duniani kuna watu wanaishi maisha ya ajabu sana. Watu hao ni wale wanaokiri kwamba wametubu dhambi zao, wanaamini kuwa Yesu ni Bwana, na wanaishi maisha matakatifu. Wanaowabeza na kuwadharau watu hao huwaita “walokole.” Haya ndiyo maajabu 20 ya maisha ya “walokole:”
  1. Hawalogeki. Wachawi wakijaribu kuwaloga ili waugue au wapate mikosi, uchawi wao unafeli. Isa 54:17
  2. Wakifanya biashara, pesa yao haiibiwi na 'chuma ulete.' Mungu analinda kazi zao. Kum 28:8
  3. Hawaugui magonjwa ya zinaa kama vile Syphilis, Gonorrhea, Chlamydia, Genital Herpes - HSV-2, Human Papillomavirus - HPV, Trichomoniasis, Chancroid... kwakuwa uasherati na uzinzi ni marufuku kwao. 1 Kor 6:18
  4. Wana amani tele hata katikati ya dhoruba za maisha. Yn 14:27
  5. Maombi na dua zao zinajibiwa. Yer 33:3
  6. Wana furaha ya kweli isiyoyumbishwa na hali za dunia. Neh 8:10
  7. Mungu huwalinda dhidi ya maadui zao. Zab 91:7
  8. Wana ujasiri wa kipekee. 2 Tim 1:7
  9. Wanaona miujiza mingi katika maisha yao. Mk 16:17-18
  10. Wanapokumbwa na majaribu, wanashinda kwa kishindo. 1 Yoh 5:4
  11. Wanaongozwa na Roho Mtakatifu katika maamuzi yao. Rum 8:14
  12. Hawafi mapema kabla ya wakati wao. Zab 118:17
  13. Mungu huwafungulia milango ya fursa na neema. Ufu 3:8
  14. Hawana hofu wanapolala usiku. Wanalala usingizi wa amani. Zab 4:8
  15. Wanapotoa, wanabarikiwa maradufu. Lk 6:38
  16. Wanapata ushindi bila wao kupigana kwa kuwa Mungu huwapigania. Kut 14:14.
  17. Wanakwepa mitego ya adui kwa ufunuo wa Mungu. Amo 3:7; Mt 10:26
  18. Wanapitia magumu, lakini wanatoka wakiwa na ushindi. Yk 1:12
  19. Mawazo yao yamejaa amani na si hofu. Isa 26:3
  20. Hawadanganywi kirahisi na mafundisho potofu, kwa sababu wana Roho wa Mungu. 1 Yoh 2:27
Mwisho wao ni wa utukufu kwa sababu Mungu anawaandalia makao ya milele(glorious eternal homes prepared by God!) Yn 14:2-3

Kama ulidanganyika na kuamini kwamba kuokoka ni ujinga basi leo umeujua ukweli. Kuokoka ni faida na wala sio hasara.

Those are the tangible and experiential benefits of salvation. If you were previously misled into believing that surrendering to Christ is folly, today you have encountered the undeniable truth. Welcome to the sanctified family of the redeemed in Christ.
 
Hawa ndo husema ukimbariki mwisrael na ww unabarikiwa lakini cha ajabu unakuta wako hoi bin taaba
 
Haya mama mchungaji naomba uniongoze sala ya TOBA
 
Kama mkeo mlokole jua ameolewa na wanaume wawili
Mmoja mchungaji wake
 
magonjwa ya zinaa kama vile Syphilis, Gonorrhea, Chlamydia, Genital Herpes - HSV-2, Human Papillomavirus - HPV, Trichomoniasis, Chancroid...
Duh, watu wanapigwa na magonjwa ya zinaa, lakini hawataki kutubu dhambi ya uasherati na uzinzi. Mbaya zaidi, wasipotubu, watapata tena kipigo cha milele.
Ufunuo 21:8 SRUV
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Ulipoanza ku-quote vifungu nikajua hii ni hadithi ya kutunga "fiction"!
"Those are the tangible and experiential benefits of salvation..."
Nime-quote vifungu ili na wewe usome ujiridhishe kuwa hayo ninayokuambia ni ahadi za Mungu kwa wanaomcha. Kama unafikiri ni hadithi za kutunga, nenda kwa wachawi unaodhani ndio mabingwa duniani - wape mamilioni ya pesa kisha uwaambie waniloge, uone kama uchawi wao utafanikiwa. Nenda sasa hivi ndio ujue kuwa ahadi hii sio hadithi za kutunga:
Hesabu 23:23 SRUV
Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
 
Ila hawa ndo watu maskini kabisa! Wanakunywa soda ngumu Sana kuwaomba soda akanunua tofauti na Sisi wanywa bia na matajiri na sii maskini
 
Ulokole ni kiwango cha uchizi stage 5 kufikia ya saba.
kuna ndugu yetu alishwai kusimamisha msiba kusema marehemu hata fufuka aliomba siku nzima akiwa na maiti sebuleni
 
Wale wanaouziwa maji, udongo, chumvi na vitambaa nao wapo kundi hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…