Yajue Madhara ya Vipodozi vyenye Kemikali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

Yajue Madhara ya Vipodozi vyenye Kemikali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

attachment.php

Wauaume kuota maziwa kama wanawake
attachment.php


attachment.php

Wanawake kuota ndevu kama wanaume
attachment.php



Idara ya afya manispaa ya Sumbawanga imewaonya wakazi kujiepusha na matumizi ya vipodozi vilivyotengenezwa na viambatanishi vyenye sumu aina ya "Steroids." Vipodozi hivyo vimeshapigwa marufuku nchini na wenye kutumia wapo hatarini kupata athari zilizo kinyume na jinsia ya maumbile yao ikiwa ni pamoja na wanaume kuota matiti na wanawake kuota ndevu.

Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga Dr. Ali Musa Makori alipokuwa anasimamia zoezi la kuteketeza kwa moto tani moja ya vyakula na vipodozi vya thamani ya shilingi milioni nne na nusu. Alisisitiza wakati wanaponunua bidhaa kusoma maelezo, kuepuka kununua bidhaa ambazo muda wake umeisha na kuwa makini kutonunua bidhaa bandia.


Source: Habari Leo
 

Attachments

  • manboobs.jpg
    manboobs.jpg
    15.5 KB · Views: 1,108
  • chinese_natural.jpg
    chinese_natural.jpg
    12 KB · Views: 1,117
  • download.jpg
    download.jpg
    6.1 KB · Views: 1,085
  • Adrienne-Bailon-with-a-Beard--76673.jpg
    Adrienne-Bailon-with-a-Beard--76673.jpg
    84 KB · Views: 1,098
ahsante kwa taarifa. sijui tujipake nini sasa. kila kipodozi kinapondwa.
 
Acha wadada waishie kuota ndevu tu,patakuwa pagumu wakiota madungu
 
ahsante kwa taarifa. sijui tujipake nini sasa. kila kipodozi kinapondwa.

Ukweli wanawake wanahangaika na vipodozi, hali halisi ukiuzoesha mwili kwa vipodozi ndio tatitozo, lakini ukiwa na mazoea ya matumizi ya kawaida kujisafisha na mafuta ya kawaida tu mbona ngozi ya akina mama imeumbika kuwa nyororo? Kwa nini tuhangaike na mambo yanayohatarisha afya?
 
ahsante kwa taarifa. sijui tujipake nini sasa. kila kipodozi kinapondwa.

Angalia kwa mfano matumizi ya madawa kwenye nywele na madhara yake kwa akina mama
10450807_10152479714184857_2415652780596704040_n.jpg


Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia. Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma. "Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids," anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi. Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika. "Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone," anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury). "Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi," anasema. Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani. Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa "Lye Relaxer" ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa "No Lye Relaxer" yana calcium hydroxide na guanidine carbonate. Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer' zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa "Lye Relaxer".

Uvimbe kwenye kizazi ni nini?
Ukuta wa nyumba ya uzazi umejengwa kwa misuli ya tishu. Kwa kawaida uvimbe huu huanza kidogo kidogo na hukua hadi kufikia ukubwa wa tikiti maji. Fibroids kubwa huweza kukua na kutanua nyumba ya uzazi na kuwa sawa na ujauzito wa miezi sita au saba.

Mwanamke huweza kuwa na uvimbe mmoja mkubwa au vivimbe vingi ndani ya kizazi.
Daktari Bigwa wa magonjwa ya uzazi wa Kitengo cha Upasuaji cha Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili, Henry Mwakyoma anauelezea fibroids ni uvimbe ambao upo katika umbile la misuli myembamba na laini linalokua siku hadi siku. "Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya estrogen ambavyo vipo katika miili ya wanawake," anasema.

Dk Mwakyoma anafafanua kuwa, vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi. "Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu, huwa ni wanawake walio katika umri mkubwa au ambao tayari wamevunja ungo, kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogeni," anabainisha mtaalamu huyo.

Dalili za uvimbe wa Kizazi

  • "Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa wake. Wengi hugundulika wakati wa kujifungua au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi, basi huweza kutokwa damu kwa wingi," anasema. Anaongeza: "Hata hivyo, asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,"
  • Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi. Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali.

Anasema wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe. "Nina mifano hai, wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito, wakakosa kabisa siku zao za hedhi, wakaona dalili zote za mimba na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids," anasema.

Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza anasema wamekuwa wakifanya ukaguzi mara kwa mara kuzuia uuzwaji wake.
Isitoshe akasema: "Elimu inatolewa kwa wananchi pia ili kuwafahamisha kuhusu madhara ya vipodozi hivyo kwa sababu wanunuzi wasipokuwepo basi hata biashara haitakuwepo." Pamoja na hayo, adhabu hutolewa ya kuwanyang'anya na kuwapeleka mahakamani wenye maduka makubwa wakiziuza.

 

Wamasai wamekuwa na mazoea ya kujipodoa kwa vitu asili kabisa lakini hatujasikia madhara kwa afya zao. Vipodozi vyao havijawa processed kuchanganywa na steroids ndio maana wako na afya njema.
 
Candid Scope mi nilishaacha na madawa ya nywele kitambo. kwahiyo mafta ya kawaida unayoyasema ni yapi??
 
Last edited by a moderator:
Muwe mnaweka mada za kuwashauri kuhusu vipodozi na vitu mbalimbali ambavyo vinamadhara kwa binadam, mfano wapo ambao walisha athirika hawawezi kuacha mi nawajua lakin mkiwashauri na kuwapa mbadala kwa chakula pia, vinywaji na kashalika
 
Mkuu hawaoleweki ndio maana wanajitahidi kujibadilisha na wengi wao wapo humu
 
Mbona hata nyie wengi tuu asilimia 90 mnatumia


Zaidi ya asilimia 52 ya wanawake hutumia vipodozi vyenye sumu ambavyo huwasababishia matatizo mbalimbali ikiwamo kansa ya ngozi, figo pamoja na kuharibika kwa mimba kwa mama mjamzito. Aidha katika utafiti uliofanywa na Asasi isiyokuwa ya kiserikali Envirocare mwaka jana inaonyesha mikoa ambayo imeathirika zaidi na matumizi ya vipondozi hivyo ambayo ni Tanga, Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Kilimanjaro.

Meneja wa Mradi huo, Elfansia Shayo, alisema Envirocare imeandaa kampeni kwaajili ya kupinga matumizi ya vibodozi hivyo itakayofanyika leo jijini Dar es Salaam. "Envirocare kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imefanya utafiti ulionyesha zaidi ya asilimia 52 ya watumiaji wa vipodozi hivyo ni wanawake na baadhi yao wanajua madhara yake," alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo, Loyce Lema, alisema kampeni hiyo inahusu kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya vipodozi hivyo na ambazo viambato hivi husababisha madhara kwa watumiaji na mazingira. Alisema pamoja na TFDA kuweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia njia mbalimbali ikiwamo usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya biashara, na ukaguzi wa maduka bado mfumo huo unachangamoto kwani vipodozi vimekuwa vikiingizwa nchini kwa kutumia njia zisizo rasmi.

CHANZO: NIPASHE
 
Wanaume wa sikuhizi mnajipendezesha km wanawake...

Wanaume wa siku hizi mnatumia dawa za nywele..

Na si vipodozi tuu hata wapenzi wenye sumu mnatumia..tena sumu ya kuwaua taratibu sababu mnachepuka na kwenda kavu kavu...


Na si hayo tuu hata vyakula mnatumia vyenye sumu...Vinywaji vyenye sumu.....

poison poison poison full poison
 
Wanaume wa sikuhizi mnajipendezesha km wanawake...

Wanaume wa siku hizi mnatumia dawa za nywele..

Na si vipodozi tuu hata wapenzi wenye sumu mnatumia..tena sumu ya kuwaua taratibu sababu mnachepuka na kwenda kavu kavu...


Na si hayo tuu hata vyakula mnatumia vyenye sumu...Vinywaji vyenye sumu.....

poison poison poison full poison

Huyo anayeandika gazeti nae utakuta anatumia sumu..km si ngozini kichwani...Anayetanganza nae vile vile
 
Back
Top Bottom