Yajue Maeneo ya kanuni za Bunge ma ambayo CCM walikuwa wanayapigia Chapuo lakini wamedondokea Pua.

Yajue Maeneo ya kanuni za Bunge ma ambayo CCM walikuwa wanayapigia Chapuo lakini wamedondokea Pua.

mwaikenda

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2011
Posts
903
Reaction score
143
Wana jamvi.
Nichukue Fursa hii kwanza Kuishukuru Kamati ya Kanuni ambayo imefanya Kazi kubwa sana huku Utundu Mkubwa wa Kujisomea na utaalam wa Hali ya Juu wa Tundu Lissu ukijionesha Bungeni( kauli ya Ismaili Jussa).

Kanuni hizo ambazo Bunge Maalum limepitisha jana CCM walikuwa wakipigia Chapuo baadhi ya Vifungu Ili kulinda Maslahi ya Chama Chao na Si ya Kitaifa. Vifungu hivyo ni Kama vifuatavyo:

1. Upitishaji wa Vifungu kwa Idadi ya "TWO THIRD" kwa upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar.
Chama cha Mapinduzi kilikuwa kinapigia Chapuo kuwa wakati wa kupitisha Ibara za Katiba ni Lazima vipite kwa idadi ya Aslimia hamsini ya Wabunge wote bila kujali pande mbili za muungano jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Mbadiliko ya Katiba na Katiba yenyewe. Hatimaye Kamati ya kanuni ikatoa ufafanuzi mzuri kuwa kila ibara itapigiwa kura na ili ipite ni kwa idadi "two third" ya Tanganyika na "two third" ya Zanzibar na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba na Katiba yenyewe. Kwa msingi huo kanuni mpya zinasema kuwa kila ibara itapigiwa kura na idadi ya two third kwa upande wa zanzibar na Tanganyika ndiyo ibara hiyo itapita na hata kwa rasimu yote pia itapigiwa kura na Bunge Maalum ili ipite ni lazima ipigiwe kura kwa idadi ya two third Zanzibar na "two third" Tanganyika na hata kwa kwa wananchi pia ili katiba ipite ni lazima two third ya wananchi wa Tanganyika na wanachi wa Zanzibar.

2. CCm walitaka pia kila katika Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati kusiwepo taarifa kinzani ambayo ni maoni ya wachache na CCM walitaka pia taarifa hii isiwepo kabisa kwani wajumbe wa katiba ni wamoja. Baada ya Mjadala mrefu hatimaye CCM wakabwagwa pia na position mpya ni kwamba Taarifa ya Kamati itasomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ikiwepo pia taarifa ya wachache baada ya kusomwa ataitwa msemaji wa maoni ya wachache ili kutoa ufafanuzi wa msingi wa maoni yao.

3. Kuhusu muda wa uwaslihaji CCM walitaka kuwa Mwenyekiti wa Kamati atumie saa moja wakati wa kuwasilisha hoja Bungeni na kwa upande wa wajumbe wenye maoni yanayo kinzana na walio wengi( Maoni ya wachache) wapewe dakika 20 lakini hali ikawa tofauti sasa hivi ni kwamba Mwenyekiti wa Kamati atatumia saa moja na na mjumbe atakaye soma maoni ya wachache atatumia dakika 30.

4. Kura ya Siri au wazi. hapa ndipo kuna kaa la moto ccm wanataka kura ya wazi na wengineo wakiwepo wapinzani wanataka kura ya siri kwa kuwa suaala hili lipo pending ngoja tusubiri mpaka hapo itakapo amuliwa vinginevyo.

Kwa kifupi naomba kuwasilisha.
 
CCM walitaka!? Mbona mimi nilishuhudia baadhi ya wana CCM pale bungeni wakisimamia kuwepo na kusomwa kwa taarifa kinzani? After all, CCM ndio wengi bungeni hivyo taarifa hiyo kinzani imewekwa kwa kuamini kuwa CCM inaweza kuikubali na kuipitisha.

Mengine sijaweza kusoma kwa kuwa nimeona pumba tu.
 
hayo ni mavijijambo madogo sana kwenye katiba lililo kubwa ni muungano wa serikali 1,2au3 hapo ndipo kwenye mziki wote
 
CCM walitaka!? Mbona mimi nilishuhudia baadhi ya wana CCM pale bungeni wakisimamia kuwepo na kusomwa kwa taarifa kinzani? After all, CCM ndio wengi bungeni hivyo taarifa hiyo kinzani imewekwa kwa kuamini kuwa CCM inaweza kuikubali na kuipitisha.

Mengine sijaweza kusoma kwa kuwa nimeona pumba tu.
Sio umeona pumba hata ulichojibu ni pumba,kama wao ni wengi kwa nin wameshindwa..
 
CCM walitaka!? Mbona mimi nilishuhudia baadhi ya wana CCM pale bungeni wakisimamia kuwepo na kusomwa kwa taarifa kinzani? After all, CCM ndio wengi bungeni hivyo taarifa hiyo kinzani imewekwa kwa kuamini kuwa CCM inaweza kuikubali na kuipitisha.

Mengine sijaweza kusoma kwa kuwa nimeona pumba tu.
Nilisha kuzoea kwa dharau toka upo pale Udsm tunasoma wote ukiwa Mc wa moot court na hatimaye mtangazaji wa sherehe za nanenane.
Ukiziona pumba ujue ndiyo uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo una akili kama za Dovutwa.
 
Amesema CCM wametaka, sababu ni msimamo wa chama. Ndiyo maana hao waliokataa msimamo wa chama wamewatishiwa kunyanganywa kadi. Vilevile hadi sasa ndiyo tumeona CCM pekee ndiyo inataka kushinikiza misimamo yao ya kichama ikubalike, wakati mh. Rais alisema ni vyema tukajadili mambo kwa hoja na kukubaliana kwa pamoja ama kupiga kura.
 
CCM hawawezi kupinga wananchi waliowachagua na wakabaki salama!
Shukrani ya punda ni mateke
 
Nilisha kuzoea kwa dharau toka upo pale Udsm tunasoma wote ukiwa Mc wa moot court na hatimaye mtangazaji wa sherehe za nanenane.
Ukiziona pumba ujue ndiyo uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo una akili kama za Dovutwa.

Umempa bonge la tusi! Akili kama za Dovutwa? Aisee mi nisingekubali!
 
ccm walitaka!? Mbona mimi nilishuhudia baadhi ya wana ccm pale bungeni wakisimamia kuwepo na kusomwa kwa taarifa kinzani? After all, ccm ndio wengi bungeni hivyo taarifa hiyo kinzani imewekwa kwa kuamini kuwa ccm inaweza kuikubali na kuipitisha.

Mengine sijaweza kusoma kwa kuwa nimeona pumba tu.
wewe uwezo wako wa kusoma mambo na kuyaelewa vizuri ni mdogo sana, maana hata sura yako ya kwenye avatar inaonyesha ulipata matatizo wakati wa kuzaliwa.
 
CCM walitaka!? Mbona mimi nilishuhudia baadhi ya wana CCM pale bungeni wakisimamia kuwepo na kusomwa kwa taarifa kinzani? After all, CCM ndio wengi bungeni hivyo taarifa hiyo kinzani imewekwa kwa kuamini kuwa CCM inaweza kuikubali na kuipitisha.
Mengine sijaweza kusoma kwa kuwa nimeona pumba tu.

Halafu wewe una mawazo ya ajabu sana,jifanye kama una hati miliki na Watanzania
 
Back
Top Bottom