mwaikenda
JF-Expert Member
- Mar 26, 2011
- 903
- 143
Wana jamvi.
Nichukue Fursa hii kwanza Kuishukuru Kamati ya Kanuni ambayo imefanya Kazi kubwa sana huku Utundu Mkubwa wa Kujisomea na utaalam wa Hali ya Juu wa Tundu Lissu ukijionesha Bungeni( kauli ya Ismaili Jussa).
Kanuni hizo ambazo Bunge Maalum limepitisha jana CCM walikuwa wakipigia Chapuo baadhi ya Vifungu Ili kulinda Maslahi ya Chama Chao na Si ya Kitaifa. Vifungu hivyo ni Kama vifuatavyo:
1. Upitishaji wa Vifungu kwa Idadi ya "TWO THIRD" kwa upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar.
Chama cha Mapinduzi kilikuwa kinapigia Chapuo kuwa wakati wa kupitisha Ibara za Katiba ni Lazima vipite kwa idadi ya Aslimia hamsini ya Wabunge wote bila kujali pande mbili za muungano jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Mbadiliko ya Katiba na Katiba yenyewe. Hatimaye Kamati ya kanuni ikatoa ufafanuzi mzuri kuwa kila ibara itapigiwa kura na ili ipite ni kwa idadi "two third" ya Tanganyika na "two third" ya Zanzibar na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba na Katiba yenyewe. Kwa msingi huo kanuni mpya zinasema kuwa kila ibara itapigiwa kura na idadi ya two third kwa upande wa zanzibar na Tanganyika ndiyo ibara hiyo itapita na hata kwa rasimu yote pia itapigiwa kura na Bunge Maalum ili ipite ni lazima ipigiwe kura kwa idadi ya two third Zanzibar na "two third" Tanganyika na hata kwa kwa wananchi pia ili katiba ipite ni lazima two third ya wananchi wa Tanganyika na wanachi wa Zanzibar.
2. CCm walitaka pia kila katika Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati kusiwepo taarifa kinzani ambayo ni maoni ya wachache na CCM walitaka pia taarifa hii isiwepo kabisa kwani wajumbe wa katiba ni wamoja. Baada ya Mjadala mrefu hatimaye CCM wakabwagwa pia na position mpya ni kwamba Taarifa ya Kamati itasomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ikiwepo pia taarifa ya wachache baada ya kusomwa ataitwa msemaji wa maoni ya wachache ili kutoa ufafanuzi wa msingi wa maoni yao.
3. Kuhusu muda wa uwaslihaji CCM walitaka kuwa Mwenyekiti wa Kamati atumie saa moja wakati wa kuwasilisha hoja Bungeni na kwa upande wa wajumbe wenye maoni yanayo kinzana na walio wengi( Maoni ya wachache) wapewe dakika 20 lakini hali ikawa tofauti sasa hivi ni kwamba Mwenyekiti wa Kamati atatumia saa moja na na mjumbe atakaye soma maoni ya wachache atatumia dakika 30.
4. Kura ya Siri au wazi. hapa ndipo kuna kaa la moto ccm wanataka kura ya wazi na wengineo wakiwepo wapinzani wanataka kura ya siri kwa kuwa suaala hili lipo pending ngoja tusubiri mpaka hapo itakapo amuliwa vinginevyo.
Kwa kifupi naomba kuwasilisha.