Yajue magonjwa kumi hatari zaidi duniani

Bitoz

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
30,823
Reaction score
126,553
Kuna usemi kwamba afya ni uhai pia mtaji wa maskini ni nguv zake ikimaainisha afya njema huchangia mtu kuwa na maendeleo maana ukiwa na afya mgogoro basi utapoteza muda na pesa nyingi kujiuguza
Basi leo nawaletea magonjwa 10 hatari zaidi duniani kwa kupeleka watu wengi makaburini
NB:
Mimi siyo daktari wala mtu wa kada ya afya maana niliishia darasa la 5 hivyo nimejitahidi tu kutumia lugha ya kitabibu ingawa naweza kuwa nimekosea hivyo ni jambo la kawaida tu
...................... .................................................


10/Malaria
Huu ugonjwa huenezwa na mbu jike aitwaye Anopheles
Unashambulia zaidi bara la Afrika kutokana na hali ya kijiografia ambayo ni ya kitropiki
Mnakumbuka serikali ilianzisha kampeni ya kugawa vyandarua vya dawa....watu wailiishia kuvulia kambale tu maana hakikueienea kitandani
Kama unaishi Dar na hujawahi kuugua malaria basi labda una seli mundu

Husababisha vifo takribani Milioni 1 kila mwaka
 
Hiyo picha ya kwanza sio waziri kweli huyoo???
 
9/Kifua Kikuu

Aliyefananisha penzi na kikohonzi hayuo serious
Huu ugonjwa huenezwa na bacteria kwa njia ya hewa...huathiri zaidi mapafu lakini pia huweza kuenea hadi katika viungo zingine
Mgonjwa hupoteza uzito kwa kiwango kikubwa
Kuna uhusiano mkubwa kati ya Kifua Kikuu na mtu kuwa na VirusiVya Ukimwi

Husababisha vifo 1.4 Milioni kwa mwaka
 
8/Saratani Saratani kutokea pale seli zinaposhindwa kufanya kazi(kufa}..ikumbukwe viungo vyote kwenye mwili wa binadamu vimeumbwa kwa seli hivyo basi kila kiungo kina saratani yake, wanawake hushambuliwa na saratani ya matiti na kizazi wakati wanaume ni tezi dume(hii inamtesa mzee Majuto)
°saratani ya ubongo
*saratani ya ngozi
*saratani ya kibofu
*saratani ya shingo ya kizazi
*saratani ya damu
*saratani ya utumbo
*saratani ya kinywa
n.k
Saratani husababishwa na sababu za kibaolojia. uvutaji sigara n.k
Ugonjwa huu ndo ugonjwa uliowaua Kambarage Nyerere,Daudi Balali,Samwel Sitta huku Jakaya Kikwete akiponea chupuchupu kwa saratani ya tezi dume baada ya kuwahi matibabu

Husababisha vifo 1.5 milioni kwa mwaka
 
Nikuulize ww maana hakuna sehemu nimeandika haugui
Mimi sijaona picha yoyote ya Waziriila kama ipo itauwa ya kawaida tu maana nao ni binadamu
 
7Ukimwi

Ferouz alikiri wazi kwamba starehe zimemponza ila MwanaFA kwa umbea akasema marehemu alikufa kwa ngoma
Siku hizi kila mtu ni bonge sasa sijui utamtambuaje
Ugonjwa huu huenezwa zaidi kwa kujamiiana(hatuachi ng'o)
Hadi sasa ugonjwa huu hauna tiba/dawa bali una kinga(kondomu)....
Zamani mtu akiugua hili gonjwa ilikuwa ni rahisi kumjua ila siku hizi ARV zimewafanya watu wanenepe na kupunguza vifo vya mapema

Huua watu 1.8 Milioni kwa mwaka.
 
6/Kuhara Kuhara kwa kawaida humshambulia mtu kwa siku 1 hadi 2...
Gonjwa kuu la kuhara ni kipindupindu
Sisi tunaoishi uswahilini kuharisha siyo kesi ni kama fasheni tu...tunaharisha siku mbili tatu kisha tunaendelea tu kudunda
Kuhara husababishwa na kunywa maji yasiyochemshwa,kula vyakula vichafu n.k
Ukiumwa kipindupindu ujue umelishwa kinyesi na nzi au mikono yako mwenyewe


Huua watu 2.5 Milioni kwa mwaka
 
5/Vifo vitokanavyo na uzazi
Kuna usemi kwamba ujauzito ni nusu ugonjwa
Kilichomtokea mke mdogo wa Mzee Yusuf juzijuzi hapa kila mtu anakijua...inasikitisha sana
Vifo vinavyoongelewa ni vya mama wajawazito pamoja na vya watoto wachanga wakati wa kujifungua
Huathiri zaidi nchi maskini kutokana na huduma mbovu za afya na elimu duni ya masuala ya uzazi

Kina mama nusu Milioni na watoto zaidi ya 2.5 milioni hufariki kila mwaka jumla ni vifo 3+ milioni
 
4/Ugonjwa wa Mapafu
Mwana vuta tu sigara maana mapafu ni mali yako pia sigara unanunua kwa pesa yako ila elewa tu huo sio ujanja na mapafu yako yamejaa masizi kama sufuria la maharage kwenye jiko la kuni
Unafahamika zaidi kitaalamu kama CORD..Unaweza kuwa wa muda mfupi au muda mrefu
Uvutaji sigara huchangia kwa kiasi kikubwa mtu kuugua huu ugonjwa

Unaua takribani watu 3.3 milioni kwa mwaka
 
3/Maambukizi katika njia ya upumuaji Hakuna mswahili asiyeujua ugonjwa wa pumu
Pia juzijuzi kuna mwanaJf mwenzetu kapoteza maisha kutokana na maradhi ya upumuaji{RIP Ibra)
Huu ushambulia mfumo wa upumuaji...Unaweza kuwa pneumonia au bronchitis
Tunasisitizwa kufanya mazoezi,kula vyakula salama kwa afya,kuishi kwenye nyumba zenye hewa swaafi yaani madirisha yanayoruhusu hewa kupita,pia tupandikize miti nyumbani,kuepuka kazi za vumbi n.k
Ndiyo ugonjwa uliowaondoa mapacha maarufu na vipenzi vya watu Afrika Mashariki akina Maria na Consolata Mwakikuti

Husababisha vifo 3.5 milioni kwa mwaka
 
2/Kiharusi
Huu ugonjwa ni janga bora tu uitwe kimsiba badala ya kiharusi
Kitaalamu unaitwa Stroke kwa Lugha rahisi ni kupoozaIkumbukwe ili ubongo iweze kufanya kazi unahitaji hewa ambayo husafirishwa kupitia kwenye damu hivyo chakula cha ubongo ni damu sasa kiharusi hutokea pale damu inapofeli kufika ubongoni au kufika chini ya kiwango kwa sababu mbalimbali mfano mishipa kupasuka, shinikizo la juu la damu n.k
Mgonjwa wa kiharusi sio tu hupooza mwili bali pia akili{kupoteza kumbukumbu)

Ugonjwa huua watu takribani 6.1 milioni kwa mwaka
 
1/Ugonjwa wa Moyo Moyo ndo injini ya mwili na waswahili husema kazi ya moyo ni kusukuma damu ..kupenda ni kiherehere
Huu ndo ugonjwa mbaya zaidi duniani..huweza husababishwa na sababu mbalimbali km vile,.. kisukari, shinikizo la jyu la damu na uzito uliopitiliza
Kwa kugundua uzito wa tatizo hili serikali imeanzisha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pale Muhimbili
Ndio ugonjwa unaomsumbua yule tajiri wa Yanga ila bwana yule na jamaa yake hawamwonei huruma wamekomaa tu na Mhindi wa watu na kufikia hatua kumpa kesi ya kubwia unga

Huua watu takribani milioni 7.2 kwa mwaka
.
.
................ ....................... ........... .. ...............
Baada ya kufuatilia nimegundua list ina upungufu kwa kutoutaja ugonjwa mmoja uitwao Kisukari ambao unatajwa kusababisha vifo vya watu takribabi 1.5 milioni kwa mwaka
Pia ugonjwa wa kisukari husababisha watu wengi kuisji na vilema kutoana na kukatwa miono au miiguu na viungo vingine kaa vile vidole
.........................................................................
.
.
.
.
.
Mwisho
The Bitoz
................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…