JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Rushwa ni fedha au kitu chochote chenye thamani kinachotolewa na kupewa mtu mwenye madaraka juu ya jambo Fulani ili mtoaji apate upendeleo.
Kwa mujibu wa Sheria ya kuzuia na kupambana na Rusha (PCCB Act) ya mwaka 2007 imeharamisha makosa kadhaa ya Rushwa na kuyataja kuwa ni makosa ya jinai makosa hayo ni pamoja na :-
Kupokea rushwa, kushawishi/kulazimisha kupewa rushwa, kutoa rushwa au kuahidi kutoa rushwa na kifungu hicho kimetaja adhabu kuwa ni faini isiyopungua shilingi 500,000/= na isiyozidi shilingi 1000,000 /= au kifungo kisichopungua miaka mitatu (3) na kisichozidi miaka mitano(5) au faini na kifungo kwa pamoja.
Aidha Mahakama yaweza kufanya yafuatayo :-
i) Kumwamuru mtuhumiwa kumlipa mtu au mwajiri wake kiasi chote au nusu ya pesa au mali aliyopewa rushwa; au
ii) Kutaifisha pesa au mali iloyopokelewa kama rushwa na kuwa mali ya serikali.
Kutumia nyaraka kwa lengo la kudanganya na kujipatia fedha au faida kwa ufisadi na adhabu yake yeweza kuwa faini isiyozidi shilingi 7000,000 /= kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.
Kujipatia faida au vitu vya aina yoyote kutoka kwa mtu huku mpokeaji wa faida hiyo akijua fika kwamba atatoa maamuzi katika jambo linalomhusu mtoaji wa faida au vitu hivyo. Adhabu yake ni faini isiyozidi shilingi 10,000,000 /= kifungo kisichozidi miaka saba (7) au faini na kifungo kwa pamoja.
Aidha Mahakama yaweza kuamuru fedha au vitu vilivyopokelewa na mtuhumiwa kutaifishwa na kuwa mali ya serikali.
Upvote
0