Yale Yalee! Harmonize kufanya show uwanja wa CCM kirumba

Yale Yalee! Harmonize kufanya show uwanja wa CCM kirumba

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Ukiistaajabu ya uwanja wa CCM Sokoine Mbeya utayaona ya CCM Kirumba.

Nimeskia tangazo redioni kuwa Harmonize atakua na Show ya bure Kirumba tarehe 7 February km sjakosea chini ya udhamini wa Sayona. Baada ya kusikia hili tangazo nilijiuliza maswali mengii sn bila majibu. Hv hawa CCM wanachuliaje mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. Ni juzi tu hapa Dimond na timu yake ya wasafi wametuharibia uwanja wa Sokoine baada ya kufanya tamasha lao hali iliyopelekea uwanja kufungiwa na bodi ya ligi.Ni dhahili watu wa mbeya watakosa burudani ya ligi kuu kwa miezi yote iliyobaki. Km haitoshi wanataka kurudia tena madudu hayo hayo uwanja Kirumba tena huku wakijua dhahili ni msimu wa mvua kubwa ambazo bila ubishi zitapelekea uwanja kuharibika vibaya na kuwa jaruba la mpunga.

Swali langu kwa viongozi wa CCM hv mna lengo gani na soka la nchi hii? Mnaipeleka wapi sekta yetu pendwa ya michezo? Wadau wa michezo hebu naomba tuungane kupinga huu udhalimu tunaofanyiwa wanasoka. Hv viwanja vilijengwa kwa kodi zetu wakajimilikisha kwa mabavu. Na bado wanaendelea kitufanyia mambo ya ovyo! Naomba waziri wa michezo Mwakyembe aingilie kati kuzuia huu upuuzi. Itakua aibu kubwa uzembe wa Sokoine kujirudia Kirumba wakati uwezo wa kuzuia yasitokee bado tunao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni kampeni imeanza bado Shilole hajatumbuiza Sheikh Amir Abeid bure kwa udhamini wa Mo Dewji
 
Si viwanja vyao... Hao wengine wanakodi... Haya kesho kachimbe Mchanga,ntaleta tofari tujenge uwanja ambao ccm watapita kilomita mia mbali.
 
Back
Top Bottom