Yaliojiri VPL 12.04.2015, Yanga vs Mbeya City

Na iwe hivyo mkuu Makoye Matale!

Usijali Mkuu nifah, matokeo hayo ni ya kweli na ni hakika. Ingawa Simba wangependa kuona Yanga ilikwaa kisiki, maombi yao yatayeyuka kama umande unavyoyeyuka jua litokapo maana Mungu ameamua kutuinua Yanga katika zamu yetu, zamu ya Simba iliisha mwaka 1993 kwenye kombe la CAF (Abiola Cup).

Tuombe: Ee Mwenyezi Mungu sisi Wanayanga tusamehe dhambi zetu, ikiwa tumetanga mbali tukategemea uchawi mfano mataulo, maglovu na hata machupa ya maji katika mechi zetu, tusamehe sana. Bariki timu yako ya Yanga, ubariki wachezaji, viongozi, wanachama na mashabiki wote. Timu inapoingia kambini hapo kesho, ponya majeraha ya Telela, Sherman na Coutinho. Wapatie maarifa walimu wetu Pluijm na Mkwassa ili wakiandae kikosi cha mauaji. Hao waarabu wasipate hata goli moja ugenini huku ukisaidia Yanga tupate magoli manne hapa nyumbani. Tazama Bwana tunavyokutegemea wewe tu, usikubali timu yetu ifungwe maana maadui wetu watalitukana Jina lako takatifu wakiuliza yuko wapi mliyemtegemea? Asante kwa kuwa utawezesha ushindi mnono upatikane kwa heshima ya Jina lako, Amina.
 
Last edited by a moderator:

AMINA! Hakika hii itakua sala yangu ya kila siku kabla na baada ya mechi ya kwanza hapa nyumbani na ugenini.
Na tuungane wote katika hili..... mito Wonderful mnyepe Watu8 Bantu lady Zamaulid Sibonike Matola na wanaYanga woooote!
 
Last edited by a moderator:
AMINA! Hakika hii itakua sala yangu ya kila siku kabla na baada ya mechi ya kwanza hapa nyumbani na ugenini.
Na tuungane wote katika hili..... mito Wonderful mnyepe Watu8 Bantu lady Zamaulid Sibonike Matola na wanaYanga woooote!

Zama za kuwaogopa waarabu zimeishapita. Nina imani tukafanya vizuri home and away.Kimpira sasa tupo vizuri,limebaki suala la kisaikologia zaidi kwa wachezaji.Goli la Sherman lipo, Tambwe, Ngasa as usual. Mwaka wetu huu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…