Yaliojiri VPL 12.04.2015, Yanga vs Mbeya City

Yaliojiri VPL 12.04.2015, Yanga vs Mbeya City

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Leo ni leo.

Wale jamaa wataalamu wa kupiga mtu kwa kufata tar huku wafungaji wao wakitupia kwa kufuata mwezi watakua taifa jioni ya leo kupambana na wagonga nyundo wa nyanda za juu kudini(MCC) Tuwe pamoja bila kukosa.

kuhusu viwanja vingine matakoe wekeni hapa pia. Mwenye ratiba ya viwanja vingine aiweke hapa pia!!!
=====================

UPDATES:
Mechi ilikuwa tamu dakika 45 za kwanza. Zimekamilika huku wenyeji Yanga wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara imekuwa tamu kutokana na timu zote kucheza vizuri na kushambuliana kwa zamu.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Mliberia, Kpah Sherman na Salum Telela aliyepiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya Haruna Niyonzima.

Bao la Mbeya City limefungwa na mkongwe Themi Felix aliyewatoka mabeki Nadir Haroub na Oscar Joshua kabla ya kufunga kiufundi kabisa

Timu zimekwenda mapumziko Yanga ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1.

Dk 46, Yanga wanaanza mashambulizi kwa kasi wakionyesha wamepania kiuongeza bao.

Dk 47, Msuva anapiga shuti akiwa nje kidogo ya lango la Mbeya City, mpira unatoka.

GOOOOO Dk 49, Cannavaro anaunganisha krosi safi ya mpira wa faulo wa Niyonzima na kufunga kwa kichwa safi

Dk 52, kipa Mbeya City anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa faulo wa Niyonzima

Telela KADI NYEKUNDU Dk 53, Themi Felix anapigwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi .

DK 56, Nonga napiga shuti kali, lakini Barthez anadaka kwa mbwembwe kabisa.

Dk 59, Peter Mapunda anaingia kuchukua nafasi ya Deus Kaseke upande wa City

Dk 60, anaingia Salum Telela kuchukua nafasi ya Salum Telela kwa Yanga

Dk 61&64, Yanga wanaonekana kutawala zaidi mpira huku wakifika langoni mwa City mara nne na City wanaonekana kujilinda zaidi.

Dk 69, krosi safi ya Joshua, MSuva anapiga kichwa cha kuparaza, kinagonga mwamba na kurejea uwanjani

Dk 78, Yanga wanaonekana kumiliki mpira zaidi huku Mbeya City wakiwa wanaathirika kutokana na kuwa pungufu.

Dk 83, Ngassa anaingia vizuri na kushindwa kufunga akiwa hatua chache

Dk 87, Mwagane Yeya anajaribu kuwatoka mabeki wa Yanga lakini Barthez anakuwa mwepesi kuwahi

Dk 89, Ngassa tena anaingia eneo la hatari lakini mabeki wanambana vizuri.

MPIRA UMEKWISHAAA...!!


Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiwatika Mabeki wa Timu ya Mbeya City wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara unaoendelea kwenye Uwanja wa Taifa hivi sasa.Yanga inaongoza Bao 3 - 1. Picha na Othman Michuzi.

Kiungo Mchezeshaji wa timu ya Yanga, Haroun Niyonzima akiangalia kwa kupeleka mpira wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara unaoendelea kwenye Uwanja wa Taifa hivi sasa.Yanga inaongoza Bao 3 - 1.

Kipa wa Timu ya Mbeya City, Hanington Kalyesubula akiangalia mpira wavuni huku washabiki wa Yanga wakishangilia ushindi.

Wachezaji wa timu ya Yanga wakisangilia ushindi ushindi na washabiki wao.


attachment.php

Mashabiki wa yanga
attachment.php

Mashabiki wa Mbeya. Picha kwa hisani ya presstz

Full time:

Yanga 3 - 1 Mbeya City.


Matokeo ya Mechi za leo 2015-04-12


STAND UNITED 1 : 0 POLISI MORO


YANGA 3 : 1 MBEYA CITY



http://ww.jamiiforums.com/sports/834828-mwambusi-tunaweza-kufungwa-na-yanga-lakini-si-nane.html
 

Attachments

  • yanga.JPG
    yanga.JPG
    48.7 KB · Views: 2,757
  • mbeya.JPG
    mbeya.JPG
    61.6 KB · Views: 2,258
Kikosi cha Yanga kinachoanza leo dhidi ya Mbeya city;
1.Ally Mustapha "Barthez"
2.Juma Abdul Mnyamani
3.Oscar Fanuel Joshua
4.Nadir Haroub Cannavaro
5.Kelvin Yondan "Vidic"
6.Mbuyu Junior Twite
7.Simon Happygod Msuva
8.Salumu Abo Telela
9.Amiss Jocylin Tambwe
10.Kpah Sean Sherman
11.Haruna Hekizimana Niyonzima.

SUB---
Deogratius Munishi "Dida"
Rajabu Zahir
Nizar Halfan
Hassan Dilunga
Hussein Javu
Mrisho Halfan Ngassa

Kocha mkuu-
Hans van der Pluijm

Kocha msaidizi-
Charles Boniface Mkwasa

Daktari wa timu-
Juma Sufian

Meneja wa timu-
Afidh Saleh.

Kila la kheir dar young africans.

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
 
Kikosi cha Yanga kinachoanza leo dhidi ya Mbeya city;
1.Ally Mustapha "Barthez"
2.Juma Abdul Mnyamani
3.Oscar Fanuel Joshua
4.Nadir Haroub Cannavaro
5.Kelvin Yondan "Vidic"
6.Mbuyu Junior Twite
7.Simon Happygod Msuva
8.Salumu Abo Telela
9.Amiss Jocylin Tambwe
10.Kpah Sean Sherman
11.Haruna Hekizimana Niyonzima.

SUB---
Deogratius Munishi "Dida"
Rajabu Zahir
Nizar Halfan
Hassan Dilunga
Hussein Javu
Mrisho Halfan Ngassa

Kocha mkuu-
Hans van der Pluijm

Kocha msaidizi-
Charles Boniface Mkwasa

Daktari wa timu-
Juma Sufian

Meneja wa timu-
Afidh Saleh.

Kila la kheir dar young africans.

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.

Asante Jerry Muro
 
nawashauri mcc kwamba safari hii wasifukuze kipa tena bali wakubali tu kuwa yanga wapo vizuri kwa sasa kuliko timu nyingine kwenye ligi hii.
 
Kikosi cha Yanga kinachoanza leo dhidi ya Mbeya city;
1.Ally Mustapha "Barthez"
2.Juma Abdul Mnyamani
3.Oscar Fanuel Joshua
4.Nadir Haroub Cannavaro
5.Kelvin Yondan "Vidic"
6.Mbuyu Junior Twite
7.Simon Happygod Msuva
8.Salumu Abo Telela
9.Amiss Jocylin Tambwe
10.Kpah Sean Sherman
11.Haruna Hekizimana Niyonzima.

SUB---
Deogratius Munishi "Dida"
Rajabu Zahir
Nizar Halfan
Hassan Dilunga
Hussein Javu
Mrisho Halfan Ngassa

Kocha mkuu-
Hans van der Pluijm

Kocha msaidizi-
Charles Boniface Mkwasa

Daktari wa timu-
Juma Sufian

Meneja wa timu-
Afidh Saleh.

Kila la kheir dar young africans.

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.

heee!!...tambwe tena yupo ,sasa si wajisalimishe mapema ili yasiwakute ya waliowatangulia
 
Kikosi cha leo kizuri sana, hawa viungo salum telela na niyonzima ni hatari sana. Leo utabiri wangu mbeya city anakula 3 - 0. Kama mbeya city akipata goli basi la penati. Tambwe atatupia 2, msuva atatupia 1, sherman atakosakosa kama 7 hivi za hatari hasa za kugonga mwamba. Yeye atawafunga etoil du sahel
 
Leo nipo njia panda. Huku Yanga, huku vijana wa nyumbani. Baada ya kuweka kwenye mizani, Yanga lazima ashinde.
 
Pamoja wadau ngoja nioge nijisogeze kideoni mccty akifungwa,
Daima mbele
 
Back
Top Bottom