Kumekucha.
Kwenye droo ya jana,tumeona Simba itakavyopambana na Tout Puissant Mazembe.
Kwakweli sote tunajua historia ya Tout Puissant, ni timu ambayo ina rekodi nzuri sana kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika. Waswahili wa bara wanasema historia haidanganyi. Lakini kiuhalisia sio kila historia itazungumza ukweli wa baadae. Muda ndiyo hakimu wa Haki.
Hata hivyo Kumekuwa na vigelegele vingi mtaani juu ya mageuzi ya soka kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambayo SSC imeweza kuyaonesha, hili ni jambo zuri lakini ni wakati sasa wa kuutazama ukweli kwa Big Picture na kuacha Fantasy zote behind.
----------------------------
UKWELI MCHUNGU KUHUSU SIMBA.
Tumeona jinsi ambavyo simba ilivyopoteza michezo yote ya ugenini. Ni kipigo baada ya kipigo na kufanya jumla magoli kuwa 12 kwa ugenini tu. Simba imeonesha uwezo wa chini sana kwa mechi za ugenini na kitu kikubwa ambacho tumekiona ni wachezaji kushindwa kujiamini wakiwa ugenini.
Na hili linaonekana hata kocha ameshindwa kulipatia ufumbuzi tatizo hili.
Inasikitisha sana kuona wachezaji wanategemea kushinda nyumbani tu, na kuwa kikapu cha mipira ugenini. Tuliona JS Saoura alivyomdindia As Vita pale Kongo na kufungana 2-2, huu ndiyo mpira, mchagua jembe si mkulima.
Tout Puissant ni timu yenye wachezaji wazuri, kasi nguvu na akili en plus Expérience ya michuano hii. Nimesema tunaacha fantasy zote na kuuangalia ukweli uliyo Uchi.
Simba ikicheza na Tout Puissant kama ilivyocheza na Vita ugenini au JS Saoura kule Algérie basi tutegemee kadhaa na aibu kubwa kwa kasi na uchu wa kombe walionao
Tout Puissant.
Simba itaweza kupigwa goli hata kumi kule kongo ikiwa haitobadilika. Huyu kocha wa sasa hajawahi kueleweka kwa mechi zake za ugenini na ikumbukwe kwamba round hii unatakiwa kubalance kati ya ugenini na nyumbani ili uweze kufanikiwa.
Simba itaweza kubadili matokeo na kuandika Historia mpya ikiwa,
1. Atapatikana mwana saikolojia ili awaandae wachezaji kisaikolojia kwamba wanauwezo wa kufanya lolote.
2. Kocha aangalie formula ambayo itazaa goli ugenini, ni lazima kushinda angalau goli ugenini hata akifungwa but awe na goli la ugenini. Formula alizotumia zote kwenye makundi hajafanikiwa kupata goli ugenini hata moja. This is BS.
3. Wachezaji ambao hawana experience na michuano ya kimataifa wasipangwe. Goli ambalo Chama alilifunga linahitaji utulivu wa akili na confidence kubwa kwa dakika kama zile, lakini mtoto Chama alitulia na akaweka mpira wavuni, kwa wachezaji wetu ambao hawana experience wangepaisha juu. Chama huyu huyu ndiyo aliyeipeleka Simba kwenye makundi kwa dakika zilezile. Experience Matters a lot.
4, Mo anatakiwa kusajili wachezaji sio chini ya watatu ambao ni pure international wenye sifa na experience nzuri kimataifa kwa ajili ya michuano ya kimataifa inayokuja. Tumeona faida ya Chama kwenye game zenye namba tasa.
Ninaamini wachezaji wazuri hawawezi kukataa kwa sababu tayari Simba imejiweka kwa position nzuri kimataifa. Kwa muktadha huo timu itaweza kufika mpaka fainali na kutoa fursa kwa klabu nyingine nyumbani.
Imefika wakati sasa tuwekeze kwenye soka.
Tofauti na hapo, Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba
Tout Puissant- Nguvu kama Zote.
Thursday 21, March 2019.
-----------------
MK54