Yaliyo Nyuma na Mbele ya Simba Sports Club

Umeongea point sana Simba n rahis kufungika nyumbani na rahis kufungika ugenini yaaani accurate 50/50 hi ni mbaya kwake kwa maana karibu mech zote kufungika home and away na ndio huwa timu ya kwanza kufungwa.


Aussen angalia hili jambo hiz mech zijazo ni home and away ukipigwa out hakuna namna mtu anakupiga 3 bila kwake anakuja kwako anatafuta 1 kwisha habar

Ukweli mchungu japo unauma simba anakikosi kizuri lakin kocha hana uwezo wa kupanga kipi kikosi cha away na kipi home.

Na hata ile sub ya nyonzima ilikuwa ni bahatisha tu mana ilkuwa ukidroo unatoka,ukifungwa unatoka ilikuwa 50/50 akachukua maamuzi magumu kabisa ya kumuwek niyo
 
Mleta mada, katoa ushauri mzuri sana! Tatizo, kama isemavyo mara kwa mara, WATU WENGI HUZIPENDA TIMU SANA, KULIKO KUUPENDA MCHEZO WENYEWE. Kila mtu atoapo ushauri, hata uwe wa maana kiasi gani, wao humuona mtu huyo ni ADUI wa timu yao wanayoipenda.
Hatua waliyoifikia Simba, wanastahili pongezi. Lakini kwenye hatua hii, bila kujali itakutana na timu gani, kwa mbinu ile iliyokuwa ikitumika kusubiri ushindi nyumbani tu, ni hatari sana, hasa ukizingatia matokeo mabaya ya ugenini. Lakini, ukiwaangalia Simba walipokuwa wakicheza ugenini, walikuwa wanacheza KINYONGE sana. Ukifanyiwa kazi ushauri wa mleta mada, Simba inaweza kufika mbali!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu mnalalamika, mnataka nini? Lengo la simba ilikua kufuzu robo fainali. Kwanini tusiwapongeze na kuwaombea mafanikio pamoja na kuwatia moyo? Tumepata nafasi mbili mwakani vyura mkaonyeshe mnavyojua kukata mauno ugenini.



Nawaona simba wakichukua ndoo. Hoyooooooooooooooooooooooo.

not but pray.
 
Hapa ndipo mnapokosea nyinyi washabiki wa Simba....mtu akifanya analysis mnamuona adui??
 
Porojo tupu.

Waacheni vijana wa Simba wakifanya even mambo yao na wataalam wao.

Hatua waliyopo ni nzuri sana na hakuna cha mazembe wala mazombe.

Sijawahi kuona Mkenya akiitakia mema Tanzania.
Na ww upo kwenye kapu la Simba!!?
subirini kichapo kikali kutoka kwa hao unaowaita mazombi
 
endeleeni tu kutuombea mabaya
sasa hivi mmekuja na historia,mlinunua kanzu za mtumba ili kushangilia waarabu
Mpaka simba inaqualify kuingia group stage ilicheza mechi za ugenini nhapi? Na matokeo yake?
 
Hatutaki ushauri wenu, mnataka eti Simba ikifanikiwa mseme "walizingatia ushauri wetu". Peleka huko takataka, mwambie Zahera akawashauri TP Mazembe, sio Simba. Wataalamu waliopo Simba wana akili kuliko nyie, sasa mnashauri kitu gani?
 

Ni kweli kabisa. Simba inapaswa kuangalia yote haya. Kiufupi ikiwa kocha unashindwa kupata goli hata moja ugenini hilo ni tatizo. Ukiangalia game ya al ahly ugenini , unaona kabisa wanafungwa lakini tabu tumeipata. Simba ugenini kufungwa ni kama wajibu vile , and they don’t take time to figure out this .

Sasa tumeingia Kwenye hatua ya uchu wa kombe, ni game ambazo full kukomoana, hivyo Simba lazima ishike adabu zake ugenini. Vinginevyo itakuwa fedheha.
 
Takwimu za uongo hizi. Simba ameshashinda ugenini na ameshapata mabao 5 ugenini katika michuano hii ya CAF Champions League 2018/2019. Tena amezifunga na kuziondoa mashindanoni timu zilizoshiriki hatua ya makundi katika michuano ya CAF msimu uliopita. Sijui hizo takwimu zako umetoa wapi
 
...Sasa tumeingia Kwenye hatua ya uchu wa kombe, ni game ambazo full kukomoana, .
Hamjaingia, sema Simba wameingia. Hii ni sifa kwa Simba, wala si kwa nyie wengine. Hata hizo dola 650,000/= (Tsh. bilioni 1.5) atapewa Simba, wala si klabu nyingine. Mbona mnataka kujiingiza kwenye mafanikio ya Simba? Cha ajabu, Yanga mna mechi na Alliance Academy kabla ya mechi ya Simba vs Mazembe, lakini mnazungumzia mechi ya Simba tu na kutoa ushauri uchwara. Tokeni hapa, nendeni mkajadili uchaguzi wa viongozi na ligi ya Bara. By the way tumeshavuka malengo tulioiwekea, hii ni ziada tu na wala hatuna papara nayo. Changishaneni hela za usajili huko
 
Ndio hvyo mkuu Tatizo ushabiki mwingi kuliko uhalisia wa mambo na mchezo wa mpira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…