Mheshimiwa Sita amesema kuwaitakapofika muda wa kuipigia kura katiba inayopendekezwa, wabunge wa BMK wasiokuwepo bungeni kwa ruhusa au ugonjwa watatakiwa wapige kura kwa njia ya simu. Sitaameweza kunukuu Kanuni ya Bunge inayosema, Akidi maana yakeni idadi ya wajumbe inayoruhusiwa kwa madhumuni ya kuanza kikao cha BungeMaalumu, Kamati au kufanya uamuzi wa Bunge Maalumu au wa Kamatiya Bunge Maalumu. Je mheshimiwaSita ametafsiri sawasawa hiyo kanuni?
Kwa uelewa wangu ni kuwaakidi inaweza patikana kabla ya kuanza kikao na kikao kikaanza kufanyika lakiniinaweza tokea wakati mnaendelea na kikao wajumbe ndani ya kikao wakapungua kwasababu yoyote ile na hivyo akidi ikapungua. Kwa upungufu huo wa akidi wajumbewaliopo hawatakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kwa njia ya kura. Kama tafsiriyangu ni sahihi wajumbe ambao hawapo ndani ya kikao hawahitajiki kutafutwa kwasimu ili wapige kura wakati hawakuwepo kwenye mjadala wa jambo au mamboyaliyokuwa yakijadiliwa hata kama waliwahi kushiriki hapo kabla kwanihawakuweza kushiriki mpaka mwisho ya jambo husika.