Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Alhamisi Tarehe 13 Machi 2014 - Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Alhamisi Tarehe 13 Machi 2014 - Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti

Wakuu hili zoezi limekwisha ni Samia Suruhu sasa kifuatacho ni kiapo tu.
 
Hawa 7 ni wapu...uuu.zi gani hawaa,kila uchaguzi wanaharibu kura,yaani majitu yamevaa suti,yapo smart lakini ovyoooo!!!Kwetu Upangwa Ludewa tunawawekea ”tego“,ukiharibu kura tego linawapitiiia ukoo mzima,ni kuja...amba tu,ukihema kij.a.mbo,ukicheka kijaaambo...wa..shenzi.sana hawa,unaharibu kura??

Tobaaaahhh...!!!
Mambo gani tena haya.?
 
...mkuu' una maanisha Suluhu?

MEMBER OF PARLIAMENT CV GENERAL Salutation Honourable Member

First Name: Samia
Middle Name: Hassan
Last Name: Suluhu

Member Type: Constituency

Member Constituent: Makunduchi

Political Party: CCM

Office Location: P.O. Box 3*21, Dar Es Salaam

Majina ya Zanzibar sio ya kutamka mbele ya wakwe, sasa huyu mbunge wa Zanzibar office yake ipo Dar
 
Kama sio kuachika asilia zingepanda na pengine angekuwa mshindi
 
Hawa 7 ni wapu...uuu.zi gani hawaa,kila uchaguzi wanaharibu kura,yaani majitu yamevaa suti,yapo smart lakini ovyoooo!!!Kwetu Upangwa Ludewa tunawawekea "tego",ukiharibu kura tego linawapitiiia ukoo mzima,ni kuja...amba tu,ukihema kij.a.mbo,ukicheka kijaaambo...wa..shenzi.sana hawa,unaharibu kura??
Mkuu, hakika kwenye uchaguzi, idadi ya kura zinazoharibika huwa hazikwepeki. Kuna wengine wanaharibu kwa makusudi kwa vile hawataki wagombea wote au wanawataka wite hivyo inawawia vigumu kufanya maamuzi
 
...Asanteni Wadau wa JF: Chabruma, Skype, Kayoka, Simiyu Yetu, na wengine wote waliofanya jamvi livutie kwa taarifa na wote waliotuletea UPDATES.
 
Kificho anamalizia kusema kua utaratibu wa kuapishwa utakua kesho na orodha ya wajumbe ipo kwenye order paper.
 
Shughuli za leo zimefikia tamati na kificho anasoma dua ya kushukuru
 
Wadau, kwa vile Mwenyekiti Kificho anamalizia kutoa matangazo, nami nitumie fursa hii kuwaaga kwa muda. Hadi hapo tutakapoungana tena, alamsiki
 
Matokeo ya Makamo Mwenyekiti mteule

Wajumbe wote wapo 629

Waliopiga kura wapo 523

Zilizoharibika ni 7.

Mh. Amina Abdalah Amour kapata kura 126.

Mh. Samia Hassan kapata kura 390.

Kwahiyo makamo mwenyekiti wa bunge maalumu la katiba ni Mh Samia Hassan
 
Pongezi zenu kwenu tunategemea Katiba ya Viwango na Kasi kwa uongozi wenu Japo nyoote ni MAGAMBA TUU.
 
Samia anampongeza Amina kwa ujasiri, kisha anaanza kumshukuru kificho, anamshukuru na kumpongeza Sitta, na anawaahidi wajumbe kua atakua mwadilifu, amemaliza ila vinyimbo vinaendelea kusikika hapa
Mkuu uwe unaweka na baadhi ya hivyo vinyimbo ili tusikose lolote kwa ajili ya kumbukumbu
 
Kikao kimeahirishwa hadi kesho saa 10 jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Kutoka hapa Jukwaa la Katiba, kwa niaba ya wana jf wote hususani Chabruma, mimi ni Skype, niwatakieni jioni njema.
 
Last edited by a moderator:
Wadau, kwa vile Mwenyekiti Kificho anamalizia kutoa matangazo, nami nitumie fursa hii kuwaaga kwa muda. Hadi hapo tutakapoungana tena, alamsiki

Pamoja sana mkuu..! Nisalimie Skype
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom