Katika hali isyokuwa ya kawaida baada ya Mwenyekiti wa BML kuwapa nafasi akina Lipiumba, Mbowe, Mbatia na viongozi wa dini na wote kukubaliana na rasimu ya kanuni ghafla aliamuka Mcj Mtikila na kuhoji kwa nini amekuwa hapewi nafasi ya kuongea "Kwa nini sipewi nafasia kuongea? Mi sina neno la baraka kwa nchi yangu? Kwa nini unawapa nafasi ya kuongea watu mnaokubaliana tu? Ni haki yangu kuongea wala si ombi!
Aliendelea kusema Kificho hamuheshimu Mungu kwani haki ni agizo la Mungu, "kwanini huna heshima wewe?" unataka nikuheshimu wakati wewe huniheshimu? Kweli Mtikila ni kiboko maana pamoja na zomea zomea ya wale wenzetu amekomaa na kudai haki yake Mpaka Kificho akajitetea.