Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

Wadau, amani iwe pamoja nanyi.

Nimerudi tena kuwatonya. Ni kwamba, mdau wangu wa habari aliyepo mjengoni namaanisha Bungeni Dodoma amenitonya kuwa, wakati akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha Bunge leo asubuhi, Mchungaji Mtikila amelalama juu ya rafu zilizochezwa bungeni hapo. Amesema kuwa baadhi ya wapinzani wakiongozwa na Mbowe ---------- fedha ili wakubaliane na Kamati ya Kanuni kupitisha vifungu bila ya kipengele cha ufanywaji wa maamuzi kufikia muafaka. Anasema kuwa tangu Mwanzo, Umoja wa Kambi ya Wapinzani (UKAWA) ulikuwa na utaratibu wa kutumiana ujumbe kwa njia ya simu ili wakutane kujadili mambo na kuweka msimamo wa pamoja. Hali niyo alisema kuwa ilifanikisha wabunge wa Kambi ya Upinzani kuwa na msimamo mmoja.

Hata hivyo, Mtikila ameshangaa kitendo cha UKAWA kuendesha mambo yao kimya kimya na kwa utaratibu ambao haukuzoeleka. Mtikila alishangaa kitendo cha Mwenyekiti Kificho kusoma Tangazo la mkutano wa UKAWA ndani ya ukumbi wa Bunge jana jioni hali ambayo aliitafsiri kuwa ni akina Mbowe kukubaliana na matakwa ya CCM na Serikali. Kwa maoni yake alisema kuwa akina Mbowe wamepokea kiasi kikubwa cha fedha ili wabadili msimamo wao na ndo maana kuanzia jana walilegeza msimamo wao.

Nimewatonya tu wakuu. Ni wajibu wetu kutafakari. Tutafakari pia ni nini UKAWA, malengo yake na wanaounda umoja huo.

Nawaaga kwa muda. Nitakuja tena kuwatonya ishu nyengine muhimu
 
Mtikila kama hataki kupiga hela shauri zake.......politics is all about making money.......
 
Mleta mada CCM, anashabikia kauli kuwa akina Mbowe wamepewa fedha nyingi na CCM???????????????!!?!
tukumbuke kuwa yeye kwa kuwasilisha hiki atalipwa 7,000/-
 
Tafadhali. Mbowe tuna kuheshimu sana na tunskitegemea sana chama chako mkitugeuka hakika mtalia na sisi
 
Kuna wakati MTIKILA anakuwa na akili ya kushikiwa kwa nguvu ya pesa ili kuchafua upande wa pili ionekane wote wamekosea.TOKA NIMSHUHUDIE AKITAKA PESA KWA MENGI ILI BIFU LAO LIISHE NILIMDHARAU SANA.
 
 
Mkuu nilijua mlipotimuliwa bondeni umesepea pande za kigali.]:majani7:
 
 
Mbowe kwa pesa ni sawa sawa na sigara na kiberiti, samaki na maji.
 
Mbowe ni mchaga na katumwa pesa piga pesa acha ujinga broo mbowe maana wangepiga kura ingepita tuu
 
Suala la kupewa pesa sidhani.. Ila kukubaliana nadhani ilikuwa ni vema kupitisha kanuni hizo ili bunge liendelee na shughuli zake...
 
Mbowe watanzania tunakutegemea uwe makini sana na hao walafi.
 
ccm hawana pesa ya kumpa mboe mtoa maada nenda kawadanganye watoto wenzio humu kuna watu tunaheshima zetu pia kumbuka humu wote hawategemei buku7 waish
 
Unaonaje ukitutonya Mtikila naye amepewa fedha kiasi gani ili awachafue wapinzani wenzake?
 
kuna ajenda gani kwenye kura ya wazi au siri?izo kamati zimeshindwa kutoa maamuzi au ni uwoga na unafiki wa kuwa na fikra huru?
 
Tunaomba kujulishwa wanaochukua fomu za kugombea nafasi ya mwenyekiti ni kina nani?maana pale wametangaza bungeni kuwa wanachukulia ktk ofisi zilizopo jengo. La bunge so sio siri naamini mtaweza kuwajua
 
Nyie huko dodoma msitengeneze mazingira ya kuanza kuchapana bakora wakati ukifika, tumesha choka na nchi kuifanya ya ukoo wa panya. Tumesha fikia mwisho kuvumiliana!
 
Wakati wa kujumuisha hoja ya rasimu ya kanuni za bunge maalumu leo asubuhi, mjumbe wa kamati hiyo ndugu Jussa Ladhu aliyepewa nafasi za kutoa na kuunga hoja hiyo kwa niaba ya kamati maalumu ya kanuni akusita kutoa pongezi kwa nguli wa sheria wakili na kamanda maarufu Tundu Lissu. Alisema na hapa namnukuu..."HAKIKA SITATENDA HAKI KAMA SITATOA PONGEZI ZA DHATI KWA MHESHIMIWA TUNDU LISSU, HAKIKA AMEKUWA MSAADA MKUBWA SANA KWA KAMATI, KANUNI HIZI ZIMETOKANA NA UHODARI WAKE NA UTUNDU WAKE KWENYE SHERIA, AMEKUWA AKISOMA SANA, NA BILA KUSOMA SANA HAKIKA KAZI HII ISINGEFANIKIWA" Mwisho wa kunukuu.

My take:
Hakuna kama Tundu Lissu.

Source: TBCCM1 wakati wa bunge la katiba
 
JK anajua fika kwamba kwa wanasheria vijana wa sasa Lissu hana mpinzani. lakini hizi itikadi tu ndizo zinazuia vinginevyo ushauri wa Ole Sendeka kwamba jamaa anafaa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria au Mwanasheria mkuu wa serikali ungefuatwa.

CDM mna hazina kubwa sana!!! Hongera Lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…