Weston Songoro
JF-Expert Member
- Feb 17, 2014
- 2,793
- 1,085
Wadau, amani iwe pamoja nanyi.
Nimerudi tena kuwatonya. Ni kwamba, mdau wangu wa habari aliyepo mjengoni namaanisha Bungeni Dodoma amenitonya kuwa, wakati akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha Bunge leo asubuhi, Mchungaji Mtikila amelalama juu ya rafu zilizochezwa bungeni hapo. Amesema kuwa baadhi ya wapinzani wakiongozwa na Mbowe ---------- fedha ili wakubaliane na Kamati ya Kanuni kupitisha vifungu bila ya kipengele cha ufanywaji wa maamuzi kufikia muafaka. Anasema kuwa tangu Mwanzo, Umoja wa Kambi ya Wapinzani (UKAWA) ulikuwa na utaratibu wa kutumiana ujumbe kwa njia ya simu ili wakutane kujadili mambo na kuweka msimamo wa pamoja. Hali niyo alisema kuwa ilifanikisha wabunge wa Kambi ya Upinzani kuwa na msimamo mmoja.
Hata hivyo, Mtikila ameshangaa kitendo cha UKAWA kuendesha mambo yao kimya kimya na kwa utaratibu ambao haukuzoeleka. Mtikila alishangaa kitendo cha Mwenyekiti Kificho kusoma Tangazo la mkutano wa UKAWA ndani ya ukumbi wa Bunge jana jioni hali ambayo aliitafsiri kuwa ni akina Mbowe kukubaliana na matakwa ya CCM na Serikali. Kwa maoni yake alisema kuwa akina Mbowe wamepokea kiasi kikubwa cha fedha ili wabadili msimamo wao na ndo maana kuanzia jana walilegeza msimamo wao.
Nimewatonya tu wakuu. Ni wajibu wetu kutafakari. Tutafakari pia ni nini UKAWA, malengo yake na wanaounda umoja huo.
Nawaaga kwa muda. Nitakuja tena kuwatonya ishu nyengine muhimu