Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

Naungana na wewe mkuu coz sijaona waziri yeyote wa ccm aliyesimama adharani kuunga mkono
kura ya siri kama walivyofanya akina Ester Bulaya,bali nawaona wakipigania kura ya wazi.Nadhani kuna makubaliano waliyokubaliana,kwani haiwezekani mawaziri wote wakawa na mawazo sawa.Kama ni kweli wana mawazo sawa ndo maana hatuendlei kwani bila changamoto hakuna maendeleo.
 
kiongozi wa kikristo akiendesha maombi hayaitwi dua Bali huitwa MAOMBI jifunze.
 
Kura ya wazi ni kura inayopoteza muda mwingi na ambayo haifai na ni vurugu, Nyie mko wengi mnaogopa nini kupiga kura ya siri?mbona kumpata kificho mlishinda.Acheni kuwahadaa wananchi,dhambi na laana ya pesa zinavyozidi kutumiaka zitawaandama msipobadilika.

kama kweli Mungu yuko kilio hiki cha watanzania hamtabaki salama.kura ya katiba lazima iwe kura ya siri karatasi zihesabiwe.huwezi kupoteza muda wa kumsimamisha kila mjumbe.
 
Maneno yanayotumiwa nuda huu ni mazuri sana na yanaonesha nidhamu ya hali ya juu sana, wito wangu nawaomba wajumbe wote wafuate mtiririko huu katika kuchangia hoja zote ,
 
Mh panya ally abdalla naye anapata fulsa ya kutoa neno naye anaanza kwa kutoa shukrani kwa kamati ya kanuni pamoja na kamati ya mashauriano kwa kazi yao nzuri.

Anaamini hekima amabayo mungu amemjalia mwanadamu ndiyo zituongoze kutekeleza majukumu yaliyombele yetu.
 
shida uvyama umejaa katika bunge la katiba wala si maslai ya wananch waliowengi
 
Habari za asubuhi wajumbe wote wa jf, ndugu wachangiaji, wenye vyama na wasio na vyama bila kumsahau mheshimiwa Chabruma, nipo hewani sasa japo nimechelewa kidogo. Tuko pamoja.

Chabruma nipe mwongozo kwa ufupi sana nini kinaendelea mpaka sasa.
Mkuu Skype, Nakushukuru sana. Kwa ufupi ni kuwa baada ya Dua, Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni amesoma Azimio la kurudhia kanuni hizo. Ndani ya Azimio hilo, imebainishwa kuwa wabunge wamepitisha vifungu vyote 87 isipokuwa vile vya 37 na 38 ambavyo amesema kuwa vinaendelea kushughulikiwa na Kamati ya Mashauriano na vikikamilika vitaingizwa kwenye vifungu husika. Baada ya hapo, wabunge wanaendelea kuunga Mkono Azimio hilo. Waliotangulia kuongea ni pamoja na Lipumba, ambatia, Jenista na wengine. Wote wameunga mkono Azimio hilo. Ni hayo ru mkuu
 
ccm ni wahuni, hakutakiwi kuendelea kitu hapo mpaka hizo zipitishwe.
 
Mkuu siyo wote wanaoweza kupata nafasi za kuchangia tupo wengi mkuu anayepata anawakilisha wengine.
 
Wadau, limelipenda hili jina la mheshimiwa aliyemaliza kuongea hivi punde. Anaitwa Panya Ali Abdallah
 
Namuangaza pinda simuoni,unaweza kunionesha alipo hata kwa kumnyooshea kidole nataka nimwambie katiba ni ya watanzania asinilazimishe nifanye wanavyotaka wao na genge lake
 
Habari za asubuhi wajumbe wote wa jf, ndugu wachangiaji, wenye vyama na wasio na vyama bila kumsahau mheshimiwa Chabruma, nipo hewani sasa japo nimechelewa kidogo. Tuko pamoja.

Chabruma nipe mwongozo kwa ufupi sana nini kinaendelea mpaka sasa.
Pole kwa kuchelewa mkuu ila mungu ni mwema sasa uko online pamoja sana.
 
Maneno yanayotumiwa nuda huu ni mazuri sana na yanaonesha nidhamu ya hali ya juu sana, wito wangu nawaomba wajumbe wote wafuate mtiririko huu katika kuchangia hoja zote ,
Mkuu, hakika kamati ya mashauriano inafanya kazi nzuri sana. Nawapongeza sana wabunge hawa
 
Namuangaza pinda simuoni,unaweza kunionesha alipo hata kwa kumnyooshea kidole nataka nimwambie katiba ni ya watanzania asinilazimishe nifanye wanavyotaka wao na genge lake
Mkuu, sijamuona ila nadhani yupo
 
Swali langu ni ikiwa wanakubaliana kutokukubaliana kimsingi na ikaenda kupitishwa hiyo kura ya wazi nani alaumiwe?
 
Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ameongea naye ameunga mkono Azimio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…